Menu

HATARI YA KUTEMBEA UCHI KWA WANAWAKE 

 

Miongoni mwa misingi ya kisheria ni kufunga mlango wa fitna. Na miongoni mwa Rehma za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni kufunga mlango wa shari, basi mwenye kufungua mlango huo atapata madhambi. Amesema mshairi:- Ikiwa mja hatovaa vazi la ucha Mungu, atakuwa uchi hata kama amevaa nguo. Na mja mwema ni yule amchaye Mola wake, wala hakuna ubora kwa anaye muasi Mola wake.

Ndugu Muislam, Leo tunashuhudia wazi kabisa namna wanawake wanavyo dhihirisha mapambo yao, na kutovaa hijabu. Na bila shaka, kitendo hiki ni katika madhambi makubwa, na ni sababu ya kuteremshwa adhabu duniani, na kupata adhabu kali siku ya kiama. Ndugu zangu Waislamu, kuweni na adabu ya Mwenyezi Mungu na muwalazimishe wake zenu kuvaa hijabu na kusitiri miili yao kama alivyo amrisha Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala  katika Qur’an tukufu.

Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

[يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا}   [الأحزاب:59}

"Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."     [Al-Ahzaab:59]

 

JUKUMU LA KILA MUISLAMU KUPIGA VITA FITNA YA WANAWAKE

Ndugu Muislamu tumcheni Mwenyezi Mungu na tuwakatazeni wanawake wetu na binti zetu kudhihirisha mapambo yao. Ni lazima kila Muislamu abebe jukumu la kuamrisha mema na kukataza mabaya. Kwani, tukiacha kufanya hivyo, tutalaaniwa na Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala)kama walivyo laaniwa watu waliotangulia. Amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam: [Watu wakiona uovu na wasiukataze uovu huo huhofiwa kuwateremkia adhabu ya Mwenyezi Mungu].

Amesema Mwenyezi Mungu (SW ):

{لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ  كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ }  المائدة:78-79

"Walilaaniwa walio kufuru miongoni mwa Wana wa Israili kwa ulimi wa Daud na wa Isa mwana wa Maryamu. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakawa wanapindukia mipaka. Walikuwa hawakatazani maovu waliyo kuwa wakiyafanya. Hakika ni maovu yalioje mambo waliyo kuwa wakiyafanya!    [Al-Maaida:78-79]

 

Na amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam :[Atakaye uona uovu na auzuie kwa mkono wake, asipoweza kwa ulimi wake, asipoweza kwa moyo wake na ni udhaifu wa imani].

Ndugu katika imani, Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Amewaamrisha wanawake kuvaa hijabu na kubakia majumbani mwao, na kutolegeza sauti zao. Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala

 

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا  وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ ۖ وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا

 

"Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha Mungu basi msiregeze sauti zenu, akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mema. Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara."       [Al-Ahzaab:32-33]

 

MASHARTI YA HIJABU

 

 

1. Kufunika mwili wote isipokuwa uso

2. Hijabu isiwe na mapambo juu yake

3.Hijabu iwe nzito wala isiwe yenye kuonyesha mwili

4. Hijabu iwe pana wala isiwe yenye kubana mwili

5. Hijabu isiwe na manukato

6. Hijabu isifanane na vazi la mwanamume

7. Hijabu isifanane na vazi la makafiri

8. Hijabu isiwe ni vazi lenye kujulikana

Ushahidi wa masharti yaliyopita, Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

{يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا}  الأحزاب:59

"Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."  [Al-Ahzaab:59]

Na Akasema tena Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ}   النور:31}

 

"Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao,"     [ An-Nuur:31]

Amesema Mtume Subhaanahu wa Taala:  

[Watu wawili ni watu wa motoni, mmoja wao ni mwanamke aliyevaa nguo lakini yuko uchi].

Na Amesema katika Hadithi nyingine  Swalla Llahu ‘alayhi wasallam  [Mwanamke yoyote atakaye jitia manukato na akapita mbele ya watu, ili watu wasikie harufu ya mafuta yake, basi mwanamke huyo ni mzinifu].

Na Amesema tena Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam [Amemlaani Mtume wa Mwenyezi Mungu mwanamke mwenye kuvaa vazi la mwanamume, na mwanamume mwenye kuvaa vazi la mwanamke].

Na amesema tena Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam : [Atakaye jifananisha na watu basi ni katika wao].

Na amesema tena Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam :[ Atakae vaa vazi la kujionyesha, Mwenyezi Mungu Atamvisha vazi la udhalili siku ya kiyama].

Ndugu katika imani, ni wajibu juu kila mwanamume kuhakikisha masharti ya hijabu wakati anapo mnunulia mke wake au binti yake vazi la kuvaa. Amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam [Nyinyi wote ni wachunga, na kila mmoja ataulizwa juu ya kile alichokichunga].

Inatupasa kumuogopa Mola wetu na kutekeleza majukumu yetu kama alivyo tuamrisha Mwenyezi Mungu.



LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6574771
TodayToday2838
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 17

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68290a2f1370218026091221747520047
title_68290a2f137e516932781351747520047
title_68290a2f138c116944031101747520047

NISHATI ZA OFISI

title_68290a2f14ea08529256381747520047
title_68290a2f14f816963601971747520047
title_68290a2f1505e12331659831747520047 Add content here

HUDUMA MPYA

: 9 + 2 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com