KUHIFADHI ULIMI
Ulimi ni kiungo muhimu katika mwili wa mwanadamu. Ulimi ni neema kubwa miongoni mwa neema alizo neemeshwa mwanadamu na Allah Subhaanahu wa Taala. Kiungo hiki ni silaha yenye makali mawili, silaha ya kusababisha mwanadamu kufaulu hapa duniani na kesho Akhera, au ni silaha ya kumuangamiza mwanadamu hapa duniani na kesho akhera.
Ulimi ni neema aliompa Mwenyezi Mungu mja wake.Asema Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Ta'aala.
[أَلَمْ نَجْعَل لَّهُ عَيْنَيْنِ وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ} [البلد:8-10}
"Kwani hatukumpa macho mawili? Na ulimi, na midomo miwili? Na tukambainishia zote njia mbili? " [Al-Balad:8-10]
Maiti wangapi wamesababisha vifo vyao kwa ajili ya ndimi zao. Je hawatatupwa watu motoni isipokuwa kwa mavuno ya ndimi zao. Inapasa kwa muumini kuhifadhi ulimi wake kwa hali yoyote ile na kujiepusha na kila ambalo linapingana na sheria, mfano wa kusengenya. Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
{وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۚ إِنَّ اللَّهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ} {الحجرات:12}
"Wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo!" [Al-Hujuraat:12]
Imepokewa na Barzah al-Aslamy Amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam :[Enyi mlioamini, kwa ndimi zenu, wala imani haijaingia katika vifua vyenu msiwasengenye Waislamu, wala msichunguze aibu zao na mwenye kuchunguza aibu ya muislamu Mwenyezi Mungu atafunua aibu yake na kumfedhehesha mbele ya watu].
Kuhadharishwa juu ya Fitna:
Hadithi imepokewa na Ibn ‘Abass kuwa Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam alipita katika makaburi mawili akasema: [ Maiti hawa wawili wanaadhibiwa wala hawaadhibiwi kwa jambo kubwa, mmoja wao alikuwa hajisafishi anapokojoa na mwengine alikuwa akieneza fitna].
Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam Kutilia umuhimu kuhifadhi Ulimi
Kuhifadhi ulimi ndiko kumiliki kheri zote. Amepokea hadithi Mu’adh Ibn Jabal kuwa Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)Amesema: [Je nisikujuze kwa mambo yote hayo zuia ulimi wako(chunga ulimi wako).] Akasema. Mu’adh: Je tutahisabiwa kwa tunachokizungumza. Mtume akashangaa na kumuambia: [Je hawatupwi watu motoni ila kwa mavuno ya ndimi zao”.]
Na alikuwa Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)akiwahimiza wake zake kujihifadhi na maneno yasiomridhisha Mwenyezi Mungu. Imepokewa na ‘Aisha nimemuambia Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)tosheka na bibi Safia kwa jambo kadha na kadha akimaanisha ya kuwa ni mfupi Mtume akamuambia:[Umetamka neno ambalo kwamba likichanganywa na maji ya baharini litachanganyika].
Hali ya Waislamu Leo kupuuza kuhifadhi Ndimi Zao
Inapatikana katika hali zifuatazo:
Ushahidi wa mambo yaliyopita amehutubu na akarefusha maneno yake mbele ya ‘Umar akasema ‘Umar kurefusha maneno ni ya shetani. Na imepokewa hadith’ kutoka kwa Abu Hureira, Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam Amesema: [Muislamu bora ni yule asiyeingilia mambo ya watu, na kuingilia heshima za Waislamu ni katika sifa za wanafiki].
Amesema Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam):[Ni haramu kwa ndugu yako Muislamu damu yake, heshima yake na mali yake, Muislamu ndugu yake ni Muislamu hamdhulumu wala hamkhini na akashiria katika kifua chake taqwa ni kwenye moyo].
Maneno machafu yaliyoenea katika jamii ya kiislamu leo huenda kuwa sababu kubwa ni vyombo vya habari. Amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam : [ Hapana kitu kizito katika mizani siku ya kiyama kama tabia nzuri na Mwenyezi Mungu anachukia maneno mabaya].
Ama kuomboleza katika msiba ni jambo la kijahilia ambalo limekatazwa, na tumeamrishwa tusubiri pindi tu tunapopatikana na msiba. Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)alipita kwenye kaburi na akamuona mwanamke analia akamuambia muogope Mwenyezi Mungu na usubiri, mwanamke akajibu hujali kilichonisibu wala hakujua kwamba anayejibizana nae kuwa ni Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam akamwambia hakika ya subira ni katika tukio la Mwanzo.
Tahadhari Kueneza Uongo kwa Watu
mepokewa hadithi kutoka kwa Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam akisema:[Tahadharini na muongo, kwani uongo unapeleka kwa uovu, na uovu unapeleka mtu kuingia motoni, na mtu anasema uongo mpaka anaandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni muongo].
Na Akasema tena Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam:[ Uongo haufai hata kwa dhihaka]. Wala kuahidi mtu mtoto wake wala asimtimizie.
Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala kuamrisha waumini kuwa imara katika kupokea habari:
{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَن تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ} الحجرات:6
"Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na
mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.