DUA YA KUMUOMBEA ULIYE FUTURU KWAKE
[ أَفطَر عِنْدَكُم الصائِمونَ ، وأكل طعامَكُمُ الأبْرارُ ، وصلت عليكُمُ الملائِكَةُ ]
سنن أبي داود 3/367، وابن ماجه 1/556 ،والنسائي
[Wafuturu kwenu waliofunga na wale chakula chenu watu wema, na wawaombee rehema malaika.] [Imepokewa na Abuu Daud, na Ibnu Maajah,na Al-Nnasai.]
SIKILIZA DUA YA KUMUOMBEA ULIYE FUTURU KWAKE
KINGA YA MUISLAMU
[ اللهُمَّ أَطْعِمْ مَنْ أطْعَمَني وأَسْقِ مَنْ سْقَاني ]
مسلم3/ 26
[Ewe Mwenyezi Mungu mlishe aliyenilisha na mnyweshe aliyeninywesha] [Imepokewa na Muslim.]
SIKILIZA DUA HII HAPA
DUA YA BAADA YA KULA
[الحمد لله الذي أطعمني هذا ، وزرقنيه ،من غير حول مني ولا قوة]
أخرجه أصحاب السنن إلا النسائي
[Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambae amenilisha mimi chakula hichi na akaniruzuku pasina uwezo wangu wala nguvu zangu.] [Imepokewa na wapokezi wa hadithi ila Al-Nnasaai.]
[ الحمدُ لله حمداً كثيراً طيباً مباركاً فيهِ، غيْرَ [مَكْفيٍّ ولا] مُوَدَّع، ولا مُستَغنَى عَنْهُ ربّنا ]
البخاري 6/214 والترمذي
[Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, sifa nyingi nzuri, zenye baraka ndani yake, zisizo toshelezwa wala kuagwa, wala kutoshwa nazo mtu. Ewe Mola wetu.] [Imepokewa na Bukhari na Al-Ttirmidhiy.]
DUA YA BAADA YA KULA
DUA YA MGENI KWA ALIYEMKARIBISHA CHAKULA
[اللهُمَّ بَارِكْ لَهُم فيما رَزَقتهْمْ، واغْفِر لهم وارحَمْهُم]
مسلم3/ 1626
[Ewe Mwenyezi Mungu wabariki katika ulichowaruzuku na uwasemehe na uwarehemu.] [Imepokewa na Muslim.]
DUA YA MGENI KWA ALIYEMKARIBISHA CHAKULA
DUA KABLA YA KULA
:إذا أكل أحدكم الطعام فليقل
Atakapo kula mmoja wenu chakula basi aseme:
[ بِسْمِ الله ]
[Kwa jina la Mwenyezi Mungu]
Na akisahau mwanzo wake basi aseme:
[بِسمِ الله في أوله وآخره]
[Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzo wake na mwisho wake] [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy]
Amesema Mtume ﷺ:
من أطعمه الله الطعام فليقل
Yeyote ambae Mwenyezi Mungu amemruzuku chakula aseme:
[اللهم بارك لنا فيه وأطعمنا خيراً منه]
[Ewe Mwenyezi Mungu tubariki katika chakula hichi na tulishe bora kuliko hichi.]
ومن سقاه الله لبناً فليقل
Na yoyote ambae amemruzuku maziwa basi aseme:
[اللهم بارك لنا فيه وزدنا منه]
[Ewe Mwenyezi Mungu tubarikie kinywaji hichi na utuzidishie] [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy.]
DUA KABLA YA KULA
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.