Menu

Sehemu ya Tabia

FADHLA YA KUSUBIRI

show 2



Ikiwa subira ni chungu mwisho wake ni tamu. Subira ndio silaha ya Muislamu ya kupambana na mitihani ya ulimwengu. Bila ya subira Muislamu hawezi kufaulu katika kufanya ibada na mambo ya akhera. Ombeni msaada kwa kusubiri na kuswali. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) yuko pamoja na wanaosubiri. Subira huvuta kheri. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)katika Qur’an tukufu:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ}    آل عمران:200}

 

"Enyi mlio amini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa."     [Al-Imaan:200]

Jueni waja wa Mungu kuwa subira ni ukarimu usiokwisha, na ulinzi usioshindwa, na ngome isiyovunjika, subira na nusra ni ndugu wawili na asie vaa vazi la subira basi hushindwa na nafasi na sheitwani.

Subira ni ndugu yake muumini wala hana Imani kwa asie kuwa na subira, na akiwa nayo basi Imani yake ni ndogo na mtu asiekuwa na subira ni kama anavyosema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): 

 

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَعْبُدُ اللَّهَ عَلَىٰ حَرْفٍ ۖ فَإِنْ أَصَابَهُ خَيْرٌ اطْمَأَنَّ بِهِ ۖ وَإِنْ أَصَابَتْهُ فِتْنَةٌ انقَلَبَ عَلَىٰ وَجْهِهِ خَسِرَ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ    الحج:11

 

"Na katika watu wapo wanao muabudu Mwenyezi Mungu kwa ukingoni. Ikimfikia kheri hutulia kwayo, na ukimfikia msukosuko hugeuza uso wake. Amekhasiri dunia na Akhera; hiyo ndiyo khasara iliyo wazi."     [Al-Haaj:11]

Subira ni tabia za waumini waliokamilika, hawezi kuwa nayo mtu ila baada ya kujaaliwa na Mwenyezi Mungu. Amesema Imam Ahmad; Mwenyezi Mungu ametaja subira katika Qur’an mara tisini (90) katika sehemu tofauti.

FAIDA YA KUSUBIRI

 

Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) atawapa malipo yao bila ya hesabu. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

{إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ}             الزمر:10

 

"Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu."   [Al-Zzumar:10]

Mwenyezi Mungu yuko pamoja nao katika kuwaongoza na kuwanusuru. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ ۖ وَاصْبِرُوا ۚ إِنَّ اللَّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ}    الأنفال:46 {

 

"Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri."   [Al-Anfaal:46]

Mwenyezi Mungu kuifanya subira ni jambo la mtu Kupata uongozi. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

 

{وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا ۖ وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ}   السجدة:24

 

"Na tukawafanya miongoni mwao waongozi wanao ongoa watu kwa amri yetu, walipo subiri na wakawa na yakini na Ishara zetu."      [Al-Ssajda:24]

Subira ni bora kwa aliyekuwa nayo. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

 

{وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُم بِهِ ۖ وَلَئِن صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِّلصَّابِرِينَ}    النحل:126

 

"Na mkilipiza basi lipizeni sawa na vile mlivyo adhibiwa. Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanao subiri."     [An-Nahl:126]

Subira na Taqwa ni kinga ya vitimbi vya maadui. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

 

إِن تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِن تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُوا بِهَا ۖ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا ۗ إِنَّ اللَّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ}       آل             عمران:120

"Ikikupateni kheri huwaudhi. Na ikikupateni shari wanafurahia. Na nyinyi mkisubiri na mkajizuilia, hila zao hazitakudhuruni kitu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyazunguka yote wayatendayo."    [Al-Imraan:120]

Subira inaleta manufaa. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ}      آل عمران:200

 

"Enyi mlio amini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa."     [Al-Imraan:200]

Kuwabashiria Mwenyezi Mungu wenye subira kwa kheri tatu. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

 

وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ  الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ  أُولَٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ        البقرة:155-157}

 

"Na wabashirie wanao subiri, Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka."    [Al-Baqara:155-157]

Subira hutia mtu peponi na humuokoa kutokana na moto. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

 

إِنِّي جَزَيْتُهُمُ الْيَوْمَ بِمَا صَبَرُوا أَنَّهُمْ هُمُ الْفَائِزُونَ}     المؤمنون:111 {

 

"Hakika Mimi leo nimewalipa kwa vile walivyo subiri. Bila ya shaka hao ndio wenye kufuzu."  [Al-Muminun:111]

 

UHAKIKA WA SUBIRA

 

Subira katika lugha ya kiarabu ina maana kuzuia, na maana inayokusudiwa ni kufunga nafsi kutokana na huzuni, kuzuia ulimi kwa kushtaki, viungo kwa kupiga makofi na kupasua mifuko. Na akasema Nun Misri: “Ni kujiepusha na makosa na kutulia pindi unapopatwa na balaa na kudhihirisha utajiri pindi unapofikwa na umaskini”.

 

AINA ZA MASHTAKA

Mashtaka yasiyopingana na subira, kama alivyosema Mtume Yaakub. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

 

   قَالَ إِنَّمَا أَشْكُو بَثِّي وَحُزْنِي إِلَى اللَّهِ وَأَعْلَمُ مِنَ اللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ}      يوسف:86}

 

"Akasema: Hakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu sikitiko langu na huzuni yangu."     [ Yusuf:86]

Na akasema Mwenyezi Mungu  (Subhaanahu wa Taala)

 

{فَصَبْرٌ جَمِيلٌ}    يوسف:83

 

"Subira ni njema!"   [Yusuf:83

Mashtaka ya saa zote na ya kusimulia

 

VIGAWAYO VYA SUBIRA

 

1. Subira katika maamrisho ya Mwenyezi Mungu

2. Subira katika makatazo ya Mwenyezi Mungu

3. Subira kutokana na kudra zake Mwenyezi Mungu.

Na kama alivyosema Sheikh AbdulKadir Jeilani: hapana budi kwa mja kufanya jambo, na kukatazika kwa jambo na kusubiri kwa Qadar.

Mambo haya matatu Luqman amemuusia mwanawe akisema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

 

{يَا بُنَيَّ أَقِمِ الصَّلَاةَ وَأْمُرْ بِالْمَعْرُوفِ وَانْهَ عَنِ الْمُنكَرِ وَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا أَصَابَكَ ۖ إِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ}   لقمان:17

 

"Ewe mwanangu! Shika Sala, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa."     [ Luqman:17]

Muumini hatamani matatizo na anasubiri pindi anapopatwa na balaa. Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)siku miongoni mwa siku alipokutana na adui akimnyemelea mpaka kupinduka jua akamsimamisha akasema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)[Enyi watu musitamani kukutana na adui na muombe Mwenyezi Mungu afya na mukikutana nao subirini na jueni kuwa pepo iko chini ya upanga].

Na Abubakar Sidiq (R.A.)  amesema “Napenda kuwa na afya nishukuru ni bora kuliko kupatwa na mitihani nisubiri, na muumin anajua lolote linalompata ni kheri. Kama alivyopokea hadithi kutoka kwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) [Ajabu ya muumin ni kuwa mambo yake yote ni kheri, akipata furaha hushukuru na akipata msiba husubiri na yote ni kheri].

Maisha yote ni mitihani. Anasema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) 

 

{كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَنَبْلُوكُم بِالشَّرِّ وَالْخَيْرِ فِتْنَةً ۖ وَإِلَيْنَا تُرْجَعُونَ}   الأنبياء:35

 

"Na tunakujaribuni kwa mtihani wa shari na kheri. Na kwetu Sisi mtarejeshwa"    [Al-Anbiyaa:35]

Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) anawaonya waja wake wakati wowote ili apate kujua alie na subira na wakweli.

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَيَعْلَمَ الصَّابِرِينَ}   الأنبياء:142 {

 

"Je! Mnadhani mtaingia Peponi na hali Mwenyezi Mungu hajawapambanua wale miongoni mwenu walio pigana Jihadi, na hajawapambanua walio subiri?"    [Al-Imraan:142]

Na akasema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

 

{وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ حَتَّىٰ نَعْلَمَ الْمُجَاهِدِينَ مِنكُمْ وَالصَّابِرِينَ وَنَبْلُوَ أَخْبَارَكُمْ}     محمد:31

 

"Na bila ya shaka tutakujaribuni mpaka tuwadhihirishe wapignao Jihadi katika nyinyi na wanao subiri. Nasi tutazifanyia mtihani khabari zenu."     [Muhammad:31]

Na akasema Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala):

 

إِن يَمْسَسْكُمْ قَرْحٌ فَقَدْ مَسَّ الْقَوْمَ قَرْحٌ مِّثْلُهُ ۚ وَتِلْكَ الْأَيَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيْنَ النَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَتَّخِذَ مِنكُمْ شُهَدَاءَ ۗ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَوَلِيُمَحِّصَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَمْحَقَ الْكَافِرِينَ        آل عمران:141-142

 

"Kama yamekupateni majaraha, basi na hao watu wengine yamewapata majaraha mfano wa haya. Na siku za namna hii tunaweletea watu kwa zamu, ili Mwenyezi Mungu awapambanue walio amini na awateuwe miongoni mwenu mashahidi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhaalimu; Na pia ili Mwenyezi Mungu awasafishe walio amini na awafutilie mbali makafiri"    [Al-Imraan:140-141]

Na akasema mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

إِنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ ۚ وَاللَّهُ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ}     التغابن:15 {

 

"Hakika mali yenu na watoto wenu ni jaribio. Na kwa Mwenyezi Mungu upo ujira mkubwa."     Al-Ttaghabun:15

 

 



 

HATARI YA KUTEMBEA UCHI KWA WANAWAKE 

 

Miongoni mwa misingi ya kisheria ni kufunga mlango wa fitna. Na miongoni mwa Rehma za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni kufunga mlango wa shari, basi mwenye kufungua mlango huo atapata madhambi. Amesema mshairi:- Ikiwa mja hatovaa vazi la ucha Mungu, atakuwa uchi hata kama amevaa nguo. Na mja mwema ni yule amchaye Mola wake, wala hakuna ubora kwa anaye muasi Mola wake.

Ndugu Muislam, Leo tunashuhudia wazi kabisa namna wanawake wanavyo dhihirisha mapambo yao, na kutovaa hijabu. Na bila shaka, kitendo hiki ni katika madhambi makubwa, na ni sababu ya kuteremshwa adhabu duniani, na kupata adhabu kali siku ya kiama. Ndugu zangu Waislamu, kuweni na adabu ya Mwenyezi Mungu na muwalazimishe wake zenu kuvaa hijabu na kusitiri miili yao kama alivyo amrisha Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala  katika Qur’an tukufu.

Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

[يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا}   [الأحزاب:59}

"Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."     [Al-Ahzaab:59]

 

JUKUMU LA KILA MUISLAMU KUPIGA VITA FITNA YA WANAWAKE

Ndugu Muislamu tumcheni Mwenyezi Mungu na tuwakatazeni wanawake wetu na binti zetu kudhihirisha mapambo yao. Ni lazima kila Muislamu abebe jukumu la kuamrisha mema na kukataza mabaya. Kwani, tukiacha kufanya hivyo, tutalaaniwa na Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala)kama walivyo laaniwa watu waliotangulia. Amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam: [Watu wakiona uovu na wasiukataze uovu huo huhofiwa kuwateremkia adhabu ya Mwenyezi Mungu].

Amesema Mwenyezi Mungu (SW ):

{لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ  كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ }  المائدة:78-79

"Walilaaniwa walio kufuru miongoni mwa Wana wa Israili kwa ulimi wa Daud na wa Isa mwana wa Maryamu. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakawa wanapindukia mipaka. Walikuwa hawakatazani maovu waliyo kuwa wakiyafanya. Hakika ni maovu yalioje mambo waliyo kuwa wakiyafanya!    [Al-Maaida:78-79]

 

Na amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam :[Atakaye uona uovu na auzuie kwa mkono wake, asipoweza kwa ulimi wake, asipoweza kwa moyo wake na ni udhaifu wa imani].

Ndugu katika imani, Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Amewaamrisha wanawake kuvaa hijabu na kubakia majumbani mwao, na kutolegeza sauti zao. Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala

 

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا  وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ ۖ وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا

 

"Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha Mungu basi msiregeze sauti zenu, akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mema. Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara."       [Al-Ahzaab:32-33]

 

MASHARTI YA HIJABU

 

 

1. Kufunika mwili wote isipokuwa uso

2. Hijabu isiwe na mapambo juu yake

3.Hijabu iwe nzito wala isiwe yenye kuonyesha mwili

4. Hijabu iwe pana wala isiwe yenye kubana mwili

5. Hijabu isiwe na manukato

6. Hijabu isifanane na vazi la mwanamume

7. Hijabu isifanane na vazi la makafiri

8. Hijabu isiwe ni vazi lenye kujulikana

Ushahidi wa masharti yaliyopita, Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

{يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا}  الأحزاب:59

"Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."  [Al-Ahzaab:59]

Na Akasema tena Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ}   النور:31}

 

"Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao,"     [ An-Nuur:31]

Amesema Mtume Subhaanahu wa Taala:  

[Watu wawili ni watu wa motoni, mmoja wao ni mwanamke aliyevaa nguo lakini yuko uchi].

Na Amesema katika Hadithi nyingine  Swalla Llahu ‘alayhi wasallam  [Mwanamke yoyote atakaye jitia manukato na akapita mbele ya watu, ili watu wasikie harufu ya mafuta yake, basi mwanamke huyo ni mzinifu].

Na Amesema tena Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam [Amemlaani Mtume wa Mwenyezi Mungu mwanamke mwenye kuvaa vazi la mwanamume, na mwanamume mwenye kuvaa vazi la mwanamke].

Na amesema tena Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam : [Atakaye jifananisha na watu basi ni katika wao].

Na amesema tena Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam :[ Atakae vaa vazi la kujionyesha, Mwenyezi Mungu Atamvisha vazi la udhalili siku ya kiyama].

Ndugu katika imani, ni wajibu juu kila mwanamume kuhakikisha masharti ya hijabu wakati anapo mnunulia mke wake au binti yake vazi la kuvaa. Amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam [Nyinyi wote ni wachunga, na kila mmoja ataulizwa juu ya kile alichokichunga].

Inatupasa kumuogopa Mola wetu na kutekeleza majukumu yetu kama alivyo tuamrisha Mwenyezi Mungu.



DHANA MBAYA

753 5020tumblr m31vck1bKD1qcejh9o1 500

 

Miongoni mwa maafa yaliyowasibu watu na jamii ni dhana mbaya, jambo ambalo linakata mapenzi kati ya watu, na mwenye dhana mbaya huwaangalia watu kwa jicho ovu, na bila shaka dhana mbaya ni kinyume na sheria ya kiislamu.

Ili mafungamano baina yetu na watu yabaki kuwa ni imara ni kuwakabili watu hali ya kuwa nyoyo zetu zimesalimika pia kuwa safi na nyuso kuwa na bashasha na kuwadhania watu kwa dhana nzuri pindi tunaposalimiana nao. Tunapozingatia mafungamano ya Waislamu yamesambaratika kutokana na dhana mbaya. Unaposikia maongozi ya Waislamu tunasikia wakisema fulani amekusudia hivi, na fulani ametaka jamabo hili. Yote yanapelekea kupatikana kwa chuki na mwisho ni kuvunjika au kusambaratika kwa mafungamano. Dhana mbaya inapeleka kufuatilia aibu za watu na kuchunguzana kwa ajili hiyo utasikia kwa mwenye dhana mbaya akisema ‘Nitajaribu kuhakikisha’ basi atachunguza na kusengenya na kumtaja mwenzake kwa uovu. Kuenea kwa dhana mbaya kunakosekana uaminifu kati ya watu na kukatana jambo ambalo kwamba linapelekea kutofaulu katika mambo yetu.

Anasema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ ۖ وَاصْبِرُوا ۚ إِنَّ اللَّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ}     الأنفال:46}

 

"Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri."      [Al-Anfaal:46]

Dhana mbaya haileti kheri na ni njia ya kuenea kwa uadui na kupatikana kwa madhambi hayo duniani ama kesho akhera ni majuto. Tazama watu waovu walivyo wakejeli Waislamu na kuwadhania maovu pindi Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Aliposema:

{وَقَالُوا مَا لَنَا لَا نَرَىٰ رِجَالًا كُنَّا نَعُدُّهُم مِّنَ الْأَشْرَارِ  أَتَّخَذْنَاهُمْ سِخْرِيًّا أَمْ زَاغَتْ عَنْهُمُ الْأَبْصَارُ}        ص:62-63

"Watasema: Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ndio katika waovu?  Tulikosea tulipo wafanyia maskhara, au macho yetu tu hayawaoni ?"     [Sw'aad:62-63]

Anasema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala

فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ  عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ  هَلْ ثُوِّبَ الْكُفَّارُ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ}     المطففين:34-36

 

"Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri, Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia. Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda?"     [Al-Mutaffifin:34-36]

Anasema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

 

    {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ}        { الحجرات:12}

"Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi."     [Al-Hujuraat:12]

Inajulisha Aya katika kuhifadhi heshima ya Muislamu kwa kutangulia na katazo la dhana. Ni uzuri ulioje kwa mujtama ulio salimika na dhana mbaya. Mtume  Swalla Llahu ‘alayhi wasallam amesema

[Jiepusheni na dhana hakika ya dhana ni maongezi ya uongo wala msichunguzane wala msichukiane kuweni ndugu katika waja wa Mwenyezi Mungu].

Wamesema baadhi ya wanavyuoni dhana ambayo inafaa kuepukwa ni ile ambayo kwamba haijulikani njia yake kuwa ni ya sawa na sababu iliyokuwa ya wazi, mfano anayedhaniwa akiwa ni mtu mwema na akapewa amana kuwadhania kuwa amekhini ni haramu. Kinyume na ambae anajulikana anayefanya maovu wazi wazi kwa ajili hiyo wamesema wanavyuoni dhana mbaya kwa mtu mwema haifai na hapana tatizo kudhania uovu mtu muovu.

Imepokewa hadithi Said ibn Musaib akisema: “Amewaandikia baadhi ya maswahaba kutowacha kufanya wema kwa jambo la ndugu yake maadamu hujashindwa wala asidhani neno baya limetoka kwa ndugu yako ikiwa inawezekana kuchukulia kwa uzuri na huo ndio mfano wa watu wema pindi wanaposhindwa kuelewa baadhi ya maneno, kwa kuwahukumu makosa watu wengine bila ya kuzingatia nia na hali ya yule mtu”.

Na Ibn Qayyim amesema: “Neno moja husemwa na watu wawili mmoja wao anakusudia haki na mwingine wao anakusudia batili kwa ajili hiyo hahukumiwi mtu kuwa kafiri kwa aliyesema “ Ewe mola wangu wewe ni mja wangu na mimi ni mola wako” hakukusudia kujifanya Mwenyezi Mungu.

Na Amesema Sheikhul Islam Ibn Taymiyya "pindi anaponukuu maneno ya wenye kumkhalifu akisema “Maneno haya yana upana, na haki huchukuliwa kwa uzuri na batili huwa na mambo mengi”

Mwanadamu hana haki kwa ndugu yake isipokuwa kwa mambo yaliyo wazi. Amepokea Abdulrazaq kutoka kwa ‘Umar Ibn Khattab (R.A.)

akisema: “ Watu walikuwa wakipokea wahyi wakati wa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na wahyi ukakatika, lakini tunachukua sasa kwa yale yaliyodhihiri kutokana na vitendo vyenu kwa atakae dhihiri kheri tutamuamini na tutamkaribisha haitujalishi sisi usiri wake na Mwenyezi Mungu ndiye atakaye muhesabu kutokana na usiri wake na atakae dhihiri shari lake kwetu hatutomuamini wala hatutomsadiki hata akisema kuwa usiri wake ni mwema”. Kwa Muislamu ahesabu kuwa kila neno analozungumza au hukumu anayotamka na akumbuke Neno lake Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

         وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا}        الإسراء:36 

Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa." [ Al-Israai:36]


KUHIFADHI ULIMI

زلة لسان

 

Ulimi ni kiungo muhimu katika mwili wa mwanadamu. Ulimi ni neema kubwa miongoni mwa neema alizo neemeshwa mwanadamu na Allah Subhaanahu wa Taala. Kiungo hiki ni silaha yenye makali mawili, silaha ya kusababisha mwanadamu kufaulu hapa duniani na kesho Akhera, au ni silaha ya kumuangamiza mwanadamu hapa duniani na kesho akhera.

Ulimi ni neema aliompa Mwenyezi Mungu mja wake.Asema Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Ta'aala.

 

[أَلَمْ نَجْعَل لَّهُ عَيْنَيْنِ وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ  وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ}       [البلد:8-10}

 

"Kwani hatukumpa macho mawili? Na ulimi, na midomo miwili? Na tukambainishia zote njia mbili? " [Al-Balad:8-10]

 

Maiti wangapi wamesababisha vifo vyao kwa ajili ya ndimi zao. Je hawatatupwa watu motoni isipokuwa kwa mavuno ya ndimi zao. Inapasa kwa muumini kuhifadhi ulimi wake kwa hali yoyote ile na kujiepusha na kila ambalo linapingana na sheria, mfano wa kusengenya. Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

 {وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۚ إِنَّ اللَّهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ}     {الحجرات:12}

"Wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo!"     [Al-Hujuraat:12]

 

Imepokewa na Barzah al-Aslamy Amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam :[Enyi mlioamini, kwa ndimi zenu, wala imani haijaingia katika vifua vyenu msiwasengenye Waislamu, wala msichunguze aibu zao na mwenye kuchunguza aibu ya muislamu Mwenyezi Mungu atafunua aibu yake na kumfedhehesha mbele ya watu].

Kuhadharishwa juu ya Fitna:

Hadithi imepokewa na Ibn ‘Abass kuwa Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam alipita katika makaburi mawili akasema: [ Maiti hawa wawili wanaadhibiwa wala hawaadhibiwi kwa jambo kubwa, mmoja wao alikuwa hajisafishi anapokojoa na mwengine alikuwa akieneza fitna].

Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam Kutilia umuhimu kuhifadhi Ulimi

Kuhifadhi ulimi ndiko kumiliki kheri zote. Amepokea hadithi Mu’adh Ibn Jabal kuwa Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)Amesema: [Je nisikujuze kwa mambo yote hayo zuia ulimi wako(chunga ulimi wako).] Akasema. Mu’adh: Je tutahisabiwa kwa tunachokizungumza. Mtume akashangaa na kumuambia: [Je hawatupwi watu motoni ila kwa mavuno ya ndimi zao”.]

Na alikuwa Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)akiwahimiza wake zake kujihifadhi na maneno yasiomridhisha Mwenyezi Mungu. Imepokewa na ‘Aisha nimemuambia Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)tosheka na bibi Safia kwa jambo kadha na kadha akimaanisha ya kuwa ni mfupi Mtume akamuambia:[Umetamka neno ambalo kwamba likichanganywa na maji ya baharini litachanganyika].

Hali ya Waislamu Leo kupuuza kuhifadhi Ndimi Zao

Inapatikana katika hali zifuatazo:

  1. Maneno yasiokuwa na faida
  2. Kuingilia jambo lisilo kuhusu.
  3. Kuingilia heshima za Waislamu.
  4. Ulimi mchafu( Kutusi)
  5. Kuomboleza katika msiba.

Ushahidi wa mambo yaliyopita amehutubu na akarefusha maneno yake mbele ya ‘Umar akasema ‘Umar kurefusha maneno ni ya shetani. Na imepokewa hadith’ kutoka kwa Abu Hureira, Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam Amesema: [Muislamu bora ni yule asiyeingilia mambo ya watu, na kuingilia heshima za Waislamu ni katika sifa za wanafiki].

Amesema Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam):[Ni haramu kwa ndugu yako Muislamu damu yake, heshima yake na mali yake, Muislamu ndugu yake ni Muislamu hamdhulumu wala hamkhini na akashiria katika kifua chake taqwa ni kwenye moyo].

Maneno machafu yaliyoenea katika jamii ya kiislamu leo huenda kuwa sababu kubwa ni vyombo vya habari. Amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam : [ Hapana kitu kizito katika mizani siku ya kiyama kama tabia nzuri na Mwenyezi Mungu anachukia maneno mabaya].

Ama kuomboleza katika msiba ni jambo la kijahilia ambalo limekatazwa, na tumeamrishwa tusubiri pindi tu tunapopatikana na msiba. Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)alipita kwenye kaburi na akamuona mwanamke analia akamuambia muogope Mwenyezi Mungu na usubiri, mwanamke akajibu hujali kilichonisibu wala hakujua kwamba anayejibizana nae kuwa ni Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam  akamwambia hakika ya subira ni katika tukio la Mwanzo.

 

Tahadhari Kueneza Uongo kwa Watu

mepokewa hadithi kutoka kwa Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam akisema:[Tahadharini na muongo, kwani uongo unapeleka kwa uovu, na uovu unapeleka mtu kuingia motoni, na mtu anasema uongo mpaka anaandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni muongo].

Na Akasema tena Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam:[ Uongo haufai hata kwa dhihaka]. Wala kuahidi mtu mtoto wake wala asimtimizie.

Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala kuamrisha waumini kuwa imara katika kupokea habari:

 

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَن تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ}    الحجرات:6

 "Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na 

mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.



ATHARI YA RAFIKI MWEMA

 

 bp7

Mwanadamu hawezi kuishi peke yake ana haja ya usaidizi na kutangamana na watu wengine. Kwa ajili hiyo uislamu umekuja kuitikia mwito wa maumbile, uislamu ukaweka ibada ambazo zinafanywa na watu wengi kwa pamoja mfano wa Swala. Uislamu ni dini ya maumbile, ushahidi wa hayo ni Hadithi iliyopokewa na Abu Hureira:

“ Yoyote anayezaliwa huzaliwa katika uislamu isipokuwa wazazi wake humfanya mtoto wao kuwa myahudi au mnaswara au majusi”. Kama Mwenyezi Mungu alipomuumba Adam na Hawaa ili waishi pamoja wala hakumuacha peke yake amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

{هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا}          {الأعراف:189}

 

"Yeye ndiye aliye kuumbeni katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili akae naye kwa utulivu."      [Al-A'raaf:189]

Uislamu umetiliwa nguvu kutokana na sababu nyingi kama kuwekwa ibada za pamoja mfano wake swala ya ijumaa, swala ya jamaa na nyenginezo. Dhihirisho la haya alipoazimia Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)kuchoma nyumba za wasio kuja kuswali swala za jamaa.

Na dharura kwa uhai ni kuchagua mtu anayesuhubiana nae ili amkumbushe anaposahau na kumjuza anapokuwa mjinga, amesema mshairi wa kiarabu: “ Mja usimuulize bali muangalie rafiki yake kila rafiki kutokana na marafiki huongozana. Akiwa rafiki huyo ni muovu jiepusheni nae kwa haraka, na ikiwa ni mwema husuhubiana nae utaongoka”.

Uchaguzi wa rafiki mwema umejengwa kutokana na msingi wa kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na dini yake. Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

{إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ}       المائدة:55

"Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea."     [Al-Maaida:55]

Na katika matunda ya imani ni kuchagua rafiki mwema. Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

{لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ}        { الحشر:22} 

 

"Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao."  [Al-Mujaadalah:22]

Na kemeo kubwa ni kuwapenda maadui wa Mwenyezi Mungu.na Mwenyezi Mungu amewasifu Maswahaba wa Bwana Mtume Sallallahu Alayhi Wassalam kuwa niwenye Kuhurumiana wao kwa wao na niwakali Kwa Makafiri wanao mpinga Mwenyezi Mungu.

Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

 {مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ }        {الفتح:29}

 

"Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao."      [Al-Fathi:29]

Na akasema Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala)

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ

 

"Enyi mlio amini! Atakaye iacha miongoni mwenu Dini yake, basi Mwenyezi Mungu atakuja leta watu anao wapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri, wanapigania Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya anaye laumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu na Mwenye kujua."      [Al-Maaidah:54]

Mwenye akili siku zote huwakimbia marafiki waovu kama mtu anavyo mkimbia Simba, kwa sababu siku ya Qiyama mtu atakuja juta kwa sababu ya kusuhubiana na Marafiki wabaya Wakati ambao Majuto hayafaa.

tazama Neno lake Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا  لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي ۗ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنسَانِ خَذُولًا

 

"Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema: Laiti ningeli shika njia pamoja na Mtume! Ee Ole wangu! Laiti nisingeli mfanya fulani kuwa rafiki! Amenipoteza, nikaacha Ukumbusho, baada ya kwisha nijia, na kweli Shet'ani ni khaini kwa mwanaadamu."    [Al-Furqaan:27-29]

Dhalimu aliyekusudiwa katika Aya iliyotangulia ni ‘Uqbatu ibn Abi Mu’ayit na aliyempoteza katika uongofu Ummayah ibn Khalaf.

Amefananisha Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)

[Rafiki mwema na rafiki muovu kama mfano wa anayebeba miski na mwenye kufua vyuma kwa anae beba miski ima atakuuzia ima utapata kutoka kwake harufu mzuri na mfua vyuma ima atachoma nguo zako au utapata harufu mbaya].

Je hauoni neno la Luqman juu ya mtoto wake: Ewe mwanangu tangamana na wanavyuoni hakika Mwenyezi Mungu hukuhuisha nyoyo kwa nuru ya hikima, kama anavyohuisha ardhi iliyokufa.”




LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6574358
TodayToday2425
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 10

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6828ded22b7f33973260171747508946
title_6828ded22b8d612717139941747508946
title_6828ded22b9c23453794211747508946

NISHATI ZA OFISI

title_6828ded22d3685726823151747508946
title_6828ded22d42d19015546331747508946
title_6828ded22d5147139819121747508946 Add content here

HUDUMA MPYA

: 12 + 9 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com