TABIA YA RUHUMA
Mwenyezi Mungu anasifika kwa sifa ya rehema kwa watu wake mwenye kurehemu na mwingi wa huruma. Ni sifa mbili za Mwenyezi Mungu, mwingi wa huruma kwa viumbe vyote hapa duniani, na kwa waumini siku ya kiyama, mwenye rehema pekee siku ya kiyama. Rehema zake Mwenyezi Mungu hazihesabiki, amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
{مَّا يَفْتَحِ اللَّهُ لِلنَّاسِ مِن رَّحْمَةٍ فَلَا مُمْسِكَ لَهَا ۖ وَمَا يُمْسِكْ فَلَا مُرْسِلَ لَهُ مِن بَعْدِهِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُت}
"Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu hapana wa kuizuia. Na anayo izuia hapana wa kuipeleka isipo kuwa Yeye." [Fatir:2]
Amesema Shinqiti: rehema zake Mwenyezi Mungu ni kwa watu wote duniani na kesho akhera kama kuteremsha mvua. Kama Alivyosema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
{فَانظُرْ إِلَىٰ آثَارِ رَحْمَتِ اللَّهِ كَيْفَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ}
"Basi ziangalie athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyo ihuisha ardhi baada ya kufa kwake." [Al-Ruum:50]
Enyi Waja wa Mwenyezi Mungu, sisi tunatakiwa tuwe na rehema kati yetu, na baina ya viumbe vyote, kwasababu tofauti kama:-
Mwenyezi Mungu ametuamrisha kama alivyosema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam:
[Kuweni na rehema mtarehemewa, sameheni mtasahemewa]
Tukisifika na tabia hii tutapata watakaoturehemu katika dunia. Amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam:
[Warehemuni walio duniani mtarehemewa na walio mbinguni].
Na amesema tena Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam:
[ Asiyerehemu watu, Mwenyezi Mungu pia nae hamrehemu].
Sampuli za Rehema za Mwenyezi Mungu
Kuwaumba wanadamu kwa sura nzuri, Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
{لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ}
"Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa." [Al-Ttiin:4]
Kumtukuza mwanadamu na kumfadhilisha kuliko viumbe vyote. Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَىٰ كَثِيرٍ مِّمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلًا
"Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba." [Al-Israai:70]
Kumpatia mwanadamu riziki, Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا ۚ كُلٌّ فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ
"NA HAKUNA mnyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Naye anajua makao yake na mapitio yake. Yote yamo katika Kitabu chenye kubainisha." [Huud:6]
Kudhalilisha vilivyomo mbinguni na ardhini kwa ajili yetu, amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala
{وَسَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ وَالنُّجُومُ مُسَخَّرَاتٌ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ}
"Na amefanya ukutumikieni usiku na mchana, na jua na mwezi,na nyota zikutumikieni kwa amri yake. Hakika katika hayo zipo ishara kwa watu wenye akili." [An-Nahl:12]
Kutumilizwa Mtume na kubainishia watu pepo na kuwakhofisha na moto, amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ ۖ وَأَنزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّهُ مَن يَنصُرُهُ وَرُسُلَهُ بِالْغَيْبِ ۚ إِنَّ اللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ
"Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu," [Al-Hadiid:25]
Kutumilizwa kwetu Mtume Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
وَمَا أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِمْ ۖ فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
"Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote." [Al-Anbiyaa:107]
Kupewa sheria ya kiislamu, na sheria yenyewe ni nyepesi. Amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam :
[Fanyeni upesi wala msifanye uzito, na wabashirieni watu wala msiwakhofishe].
Ndugu Waislamu, tufanye bidii kufanya mambo ya kheri ili tupate rehema za Allah. Rehema za Allah hazipatikani kwa kutamani bali ni lazima Muislamu kufuata sababu zote zitakazo mfiksha yeye kupata rehema za Mwenyezi Mungu.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.