UTAJO KATIKA MASH'ARUL HARAAM (MUZDALIFAH)
Amesema Jaabir radhi za Allah ziwe juu yake kwamba ‘Mtume ﷺ alimpanda Al-Qaswa (jina la ngamia wake) mpaka alipofika Mash’arul Haraam (huko Muzdalifah), kisha akaelekea Qiblah akamuomba Mwenyezi Mungu , akakabbir (akamtukuza), akaleta Tahlil (akamsifu), na akampwekesha. Hakuacha kusimama mpaka kulipopambazuka ndipo alipoondoka kabla ya kutoka jua. [Imepokewa na Muslim.]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.