KINGA YA MUISLAMU
[{سجد وجهي للذي خلقه ، وشق سمعه وبصره بحوله وقوته {فتبارك الله أحسن الخالقين]
الترمذي 2/474 وأحمد 6/30 والحاكم وصححه ووافقه الذهبي 1/ 220 والزيادة له
[Umesujudu uso wangu kumsujudia yule ambae ameuumba na akapasuwa masikio yake, na macho yake, kwa uwezo wake na nguvu zake, (Ametukuka Mwenyezi Mungu mbora wa waumbaji)] [Imepokewa na Al-Tirmidhiy na Ahmad na Hakim na kuisahihisha]
[اللهم أكتب لي بها عندك أجراً ، وضع عني بها وزراً ، واجعلها لي عندك ذخراً ، وتقبلها مني كما تقبلتها من عبدك داود]
الترمذي 2/473 والحاكم وصححه ووافقه الذهبي 1/ 219
[Ewe Mwenyezi Mungu niandikie kwako kwa sijda hii malipo, na nifutie kwayo madhambi, na ijaalie kwangu mbele yako ni akiba, na nikubalie kama ulivyomkubalia mja wako Dawud] [Imepokewa na Al-Tirmidhi na Hakim na akasahihisha na kuafikiwa na Al-Dhahabiy]
SIKILIZA DUA ZA SIJDA YA KISOMO
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.