Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Wanachuoni wa Fiqhi wamelezea, mambo yenye kubatilisha upangusaji wa khofu na wakatataja mambo ya fuatayo

1. Kumalizika muda wa upangusaji ulioruhusiwa kisheria kwa mkazi na msafiri.

Muda huo utakapomalizika, mpakazaji anatakiwa kwa mujibu wa sheria azivue khofu zake, kisha atawadhe udhu kamili, hapo ndipo anaweza kuzivaa tena kwa twahara hii mpya na kupata ruhusa ya kupakaza juu yake atakapotawadha tena, pia muda mpya utaanzia hapo.

2. Kupatikana kwa jambo linalowajibisha josho kama vile janaba, hedhi au nifasi.

Katika hali hii imempasa na kumlazimu mpangusaji kuzivua khofu, akoge josho lililomuwajibikia, kisha ndipo anaruhusiwa kuzivaa tena ikiwa anaona kuna haja ya kufanya hivyo. Imepokelewa hadithi na Swafwaan Ibn Assaali Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:

 

كَانَ رَسُولُ اللهِ ﷺ يَأْمُرُنَا إِذَا كُنَّا مُسَافِرِينَ أَنْ نَمْسَحَ عَلَى خِفَافِنَا، وَلَا نَنْزِعَهَا ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ مِنْ غَائِطٍ، وَبَوْلٍ، وَنَوْمٍ، إِلَّا مِنْ جَنَابَةٍ»   رواه الترمذي والنسائي

 

[Alikuwa  Mtume wa Mwenyezi Mungu akituamrisha tunapokuwa safarini tupakaze juu ya khofu zetu na wala tusizivue kwa muda wa siku tatu kutokana na kukidhi haja kubwa na ndogo na kulala ila kutokana na janaba (tu)].     [Imepokewa na Tirmidhiy na Nasaai.]

3. Mtu kuzivua khofu zote mbili au mojawapo, hata kama ikiwa uvuaji huo ni kwa kutoa sehemu kubwa ya mguu bila ya kuutoa mguu wote.

Au kwa kutoboka khofu kiasi cha kuuonyesha mguu. Katika hali zote hizi imempasa mpakazaji kuzivua.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575051
TodayToday3118
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 15

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682923fb131cb18966383611747526651
title_682923fb1332c891753561747526651
title_682923fb1347618078294381747526651

NISHATI ZA OFISI

title_682923fb156ff11800875451747526651
title_682923fb1584d704645831747526651
title_682923fb159927282378861747526651 Add content here

HUDUMA MPYA

: 1 + 3 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com