Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


MAANA YA KUTAYAMAMU 
Kutayamamu kilugha: Ni Kukikusudia kitu na kukielekea
Ama Maana yake kisheria: Ni Kupukusa uso na viganja vya mikono miwili kwa ardhi Twahara kwa nia ya kujitwahirisha

HUKMU YA KUTAYAMAMU
Inapasa kutayamamu yakikosekana maji au ikawa haiwezikani kuyatumia kwa jambo linalolazimu utwahara kama vile Swala. na kutayamamu kunapendekezwa katika kufanya jambo linalopendekezwa kama vile kusoma Qur'ani.

DALILI ZA KUTAYAMAMU 

Kutayamamu kumethibiti katika Qur-ani Tukufu, Sunna na Ijmaa ya Wanachuoni.

Dalili ya Kutayamamu katika Qur'ani.

1. Mwenyezi Mungu  Anasema:

 

فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ}     النساء:43}

 

[Mkitopata maji kusudieni ardhi nzuri, mpanguse nyuso zenu na mikono yenu ]    [4:43]

Ama Dalili yake katika Sunna.

2. Amesema Mtume :

 

أعطيت خمسا ، لم يعطهن أحد من الأنبياء قبلي : نصرت بالرعب مسيرة شهر ، وجعلت لي الأرض مسجدا وطهورا ، فأيما رجل من أمتي أدركته الصلاة فليصل     رواه البخاري

 

[Nimepewa mambo matano hakuna aliyepewa kabla yangu: Nimenusuriwa kwa kitisho masafa ya mwezi, nimefanyiwa ardhi kuwa ni mahali pa kuswali na pa kujitwahirishia: kwani yoyote katika umma wangu atakayeingiliwa na kipindi cha Swala na aswali]             [Imepokewa na Bukhari.].

Ama Ijmaa, wanazuoni wote wamekogomana na kukubaliana kuwa tayamamu imefanywa kuwa ni sheria, itumike badala ya ya udhu na josho katika hali na mazingira maalum yaliyobainishwa na sheria.

HEKIMA YA SHERIA KUWEKA KUTAYAMAMU

1. Kuwasahilishia umma wa Mtume Muhammad

2. Kuepusha madhara yanayosababishwa na utumiaji maji katika hali ya ugonjwa, na baridi kali na mfano wa hayo.

3. Kudumisha mafungamano ya ibada yasikatike kwa kukosekana maji, au kutoweza kuyatumia


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575002
TodayToday3069
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 97

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682920522ecbf3412448801747525714
title_682920522ee042480342491747525714
title_682920522ef4012374600931747525714

NISHATI ZA OFISI

title_6829205230f7e10037581331747525714
title_68292052310a911315027741747525714
title_68292052311cf3535101861747525714 Add content here

HUDUMA MPYA

: 8 + 9 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com