Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


1.HUKMU YA UVINDU NA UMANJANO

Mwanamke akiona damu ya manjano au iliyochanganyika baina ya umanjano na weusi, au akaona umajimaji tu, huwa ni moja ya hali mbili:

A). Ima aione wakati wa hedhi au imeungana na hedhi kabla ya utwahara:

Katika hali hii itapewa hukumu ya hedhi, kwa hadithi ya Aishah Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba wanawake walikuwa wakimtumia kibakuli ambacho ndani yake kuna pamba yenye dowa rangi ya manjano, na yeye akiwambia:

 

[انتظرن لا تعجلن حتى ترين القصة البيضاء]

 

[Ngojeni musifanye haraka mpaka muone paku leupe] akikusudia kwa hilo ndio kutwahirika na hedhi

B). Ima aione wakati wa twahara:

Katika hali hii huwa haizingatiwi kuwa ni kitu chochote, na haimpasi udhu wala kuoga, kwa hadithi ya Ummu Atiyyah kwamba alisema:

 

كُنَّا لا نَعُدُّ الْكُدْرَةَ وَالصُّفْرَةَ بَعْدَ الطُّهْرِ شَيْئًا]     رواه أبوداود]

 

[Hatukuwa tukiizingatia damu iliyochafuka au iliyo manjano baada ya kujitwahirisha kuwa ni chochote]    [Imepokewa na Abu Daud.].


2. HUKMU YA KUKATIKA KATIKA KWA HEDHI:

Mwanamke aonapo damu siku moja na kukatika siku moja na mfano wake, basi yeye ni mojawapo wa hali mbili

1. Hali hiyo iendelee na yeye kila wakati:
Basi hiyo ni damu ya istihadhah

2. Iwe yakatikakatika:
Kwa namna ya kwamba ikawa yamjia wakati mwingine na atwahirika wakati mwingine. Basi hukumu yake ni kama ifuatayo:

a. Kukatika damu kukipungua kwa siku moja, basi kipindi hiko kitahesabiwa kuwa ni katika kipindi cha hedhi.

b. Na akioona katika kipindi cha utwahara dalili za damu, kama kuona paku leupe, basi kipindi hiki ni cha utwahara, liwe ni dogo au kubwa, au liwe chini ya siku moja au zaidi.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575081
TodayToday3148
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 6

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682927821776c562094561747527554
title_68292782178568607291911747527554
title_682927821794721454191621747527554

NISHATI ZA OFISI

title_6829278218f46561391971747527554
title_682927821903618003030801747527554
title_68292782191173186941631747527554 Add content here

HUDUMA MPYA

: 14 + 8 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com