Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Kuna aina mbili za josho kwa mtazamo wa kisheria Josho wajibu na Josho la sunna.

Josho la wajibu :Hili ni lile josho ambalo haitosihi ibada yenye kuhitajia twahara kama vile swala bila ya kupatikana kwanza josho hili wakati wa kuwepo sababu zake.

NA mambo ambayo yakimtokea Muislamu yatamsababishia awajibikiwe kukoga josho hili la faradhi. Mambo hayo ni :

1. KUTOKWA NA MANII
Na manii ni maji meupe, mazito yanatoka kwa kasi wakati wa matamanio, na yana harufu inayofanana na yai lililoharibika, kwa neno lake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا}      المائدة:5}

 

[Na mkiwa na janaba jitwahirisheni]    [Al Maaida: 6]

Na neno lake Mtume kumwambia Ali radhi za Allah ziwe juu yake.

 

إذا فضحت الماء فقد وجب الغسل ]    رواه أبو داود]

 

[Ukimwaga maji Oga]    [ Imepokewa na Abu Daud.]

MAELEZO

1. Lau mtu aota na asitokwe na Manii, basi haimpasi kuoga. Na yanapotoka baada ya kuamka itamlazimu kuoga.

2. Akikuta Manii na asikumbuke kuwa ameota itamlazimu aoge kwa ajili ya kutokwa na Manii. Mtume amesema:

 

إنما الماء من الماء]    رواه مسلم]

 

[Hakika ulazimu wa kutumia Maji unasababishwa na kutokwa na Maji]    [Imepokewa na na Muslim.] Yaani: Kuoga kunalazimu kwa kutokwa na manii.

3.Lau ahisi kuwa manii yanataka kutoka kisha yasitoke, basi haimlazimu kuoga.

4.Lau atokwa na manii kwa hitilafu fulani mwilini mwake au ugonjwa bila ya matamanio, basi hana ulazima wa kuoga.

5.Akiwa na janaba akaoga, kisha akatokwa na manii baada ya kuoga, haimlazimu kuoga tena, kwa kuwa hayo kwa kawaida hutoka bila matamanio. Na kutoka shakani ni kutawadha.

6.Aamkapo usingizini mwenye kulala akapata urutuba (maji maji ya manii) ambao hajui sababu yake, huwa ni moja kati ya hali tatu:

A). Akate kuwa ni manii, na hapo itampasa kuoga, awe akumbuka kuwa ameota au hakumbuki.

B). Akate kuwa si manii, hapo haimpasi kuoga, na hukumu yake ni hukumu ya mkojo.

C). Awe na shaka baina ya kuwa ni manii au si manii. Hapo ni juu yake ajitahidi, akikumbuka chenye kutilia nguvu kuwa ni manii, basi ni manii. Na akikumba chenye kutilia nguvu kuwa ni madhii, basi ni madhii. Na akitokumbuka chochote itamlazimu kuoga kwa kuondoa shaka.

7.Aonapo manii na asikumbuke aliota lini, basi itamlazimu kuoga na kuzirudia Swala usingizi wa mwisho aliyoulala.

2.KUUNDAMA (KUJAMIANA)

Nako ni kukutana tupu ya mwanamume na tupu ya mwanamke, kwa kuingia sehemu ya mbele yote ya dhakari kwenye tupu, hata bila ya kushusha manii, kwa kauli ya Mtume ﷺ:

 

وَمَسَّ الْخِتَانُ الْخِتَانَ فَقَدْ وَجَبَ الْغُسْل]        رواه مسلم]

 

[Tupu ikishapita kwenye tupu, basi Hulazimu kuoga ]     [Imepokewa na Muslim].

3. KAFIRI KUSILIMU
Kwa kuwa Mtume alimuamuru Qais bin ‘Aswim aliposilimu kuoga [Imepokewa na Abu Daud.].

4. Kukatika damu ya Hedhi na Nifasi
Kwa hadithi ya Aishah kwamba Mtume alimwambia Fatimah binti Abi Hubaish 

 

فإذا أقبلت الحيضة فاتركي الصلاة ، فإذا ذهب قدرها فاغسلي عنك الدم وصلي]   رواه البخاري ومسلم]

 

[Hedhi ikija acha kuswali, na ikiondoka mda wake osha damu na uswali]     [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Na nifasi ni kama hedhi kulingana na maoni ya wanavyuoni kwa umoja wao.

5. KIFO
Kwa kauli yake Mtume katika hadithi ya kumuosha binti yake Zainab alipokufa: [Muosheni mara tatu, au tano, au zaidi ya hapo mkiona hivyo]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575178
TodayToday3245
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 15

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682939484375715719876871747532104
title_68293948438c914547477721747532104
title_6829394843a2f8419295901747532104

NISHATI ZA OFISI

title_68293948456558188777361747532104
title_682939484575b8092622691747532104
title_682939484585110958426321747532104 Add content here

HUDUMA MPYA

: 9 + 5 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com