Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Suali: Ni nini Maana ya Twahara ki Lugha na Kisheria ?

Jawabu: Utwahara kilugha
Kujisafisha na kujitakasa na uchafu

Utwahara kisheria
Utwahara kutokana na Kujitwahirisha na najisi

 

VIGAWANYO VYA TWAHARA

 

Suali: Twahara inagawanyika sehemu ngapi?

Jawabu: Twahara inagawanyika sehemu mbili:

1. UTWAHARA WA NDANI

Nao ni kuusafisha moyo na ushirikina na maasia na kila chenye kuutia doa. Haiwezekani kuhakikishika utwahara iwapo kutakuwa na uchafu wa ushirikina ndani ya moyo, kama ilivyo katika maana ya maneno ya Mwenyezi Mungu:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَٰذَا ۚ وَإِنْ خِفْتُمْ عَيْلَةً فَسَوْفَ يُغْنِيكُمُ اللَّهُ مِن فَضْلِهِ إِن شَاءَ ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ   التوبة:28

 

[Enyi Mlioamini! Hakika washirikina ni najisi, basi na wasiukaribie Msikiti wa Haram (Msikiti wa Makka) baada ya mwaka wao huu. Na mkiwa mnaogopa umasikini, basi Mwenyezi Mungu Atawakwasisha nyinyi kwa fadhla Zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi Mwenye hekima} [8: 28]

Na Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema:

 

المؤمن لا ينجس.]    رواه البخاري]

 

[Muumini hanajisiki.]  [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

 

2.UTWAHARA WA NJE

Nao ni utwahara wa mwili kutokana na hadathi na najisi.

Na inagawanyika vigawanyiko viwili:

1.Utwahara kutokana na hadathi (hali ya kutokuwa na udhu na kuwa na janaba)

Hadathi ni kile kinachotukia katika mwili kikamzuia Muislamu kufanya ibada ambazo zinahitaji utwahara, kama kuswali, kutufu kwenye Alkaba na zinginezo. Na inagawanyika vigawanyo viwili:

2. Kujitwahirisha na Najisi:

Nao ni kuiyondoa najisi mwilini na nguoni na sehemu ya kufanya ibada, Na kuondoa najisi ni lazima kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliye tukuka:

 

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ}     المدثر:4}

[Na nguo zako zitwahirishe]  [74: 4]

Na neno lake Mtume ﷺ:

 

قوله صلى الله عليه وسلم : إذا جاء أحدكم إلى المسجد فلينظر فإن رأى في نعليه قذرا أو أذى فليمسحه وليصل فيهما . رواه أبو داود

 

[Mmoja wenu akija msikitini na atazame, akiona uchafu au kitu cha kuudhi kwenye viatu vyake basi na avipanguse kisha aswali navyo].  [Imepokewa na Abuu Daud].


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575048
TodayToday3115
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 20

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682920522ecbf3412448801747525714
title_682920522ee042480342491747525714
title_682920522ef4012374600931747525714

NISHATI ZA OFISI

title_6829205230f7e10037581331747525714
title_68292052310a911315027741747525714
title_68292052311cf3535101861747525714 Add content here

HUDUMA MPYA

: 6 + 1 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com