Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Fadhla za Lailatul Qadr na Hadhi yake
1. Katika usiku huu ndio Qur’ani iliteremshwa.
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ}    القدر:1}

 

[Hakika Tumeiteremsha (Qur’ani) katika Laylatu-Qadr (usiku wenye hishima kubwa)] [Al-qadr –Aya 1].

2. Usiku huu ni bora kuliko miezi elfu moja.
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema kuhusu usiku huu:

 

لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ}      القدر:3}

 

[Huo usiku wa hishima ni bora kuliko miezi elfu]. [Al-qadr –Aya 3].

Yaani matendo ndani ya usiku huu ni bora kuliko matendo ya miezi elfu ambayo hayako katika usiku huu wa hishima.

3. Huteremka Malaika na Jibril katika Usiku huo.
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا}      القدر:4}

 

[Huteremka Malaika na roho katika usiku huo]  [Al-qadr –Aya 4]. Na makusudio ya roho: Ni Jibril.

Kutoka kwa Abu Hureira Radhi za Allah ziwe juu yake Amesema: Amesema Mtume :

إِنَّهَا لَيْلَةُ سَابِعَةٍ أَوْ تَاسِعَةٍ وَعِشْرِينَ ، إِنَّ الْمَلائِكَةَ تِلْكَ اللَّيْلَةَ فِي الأَرْضِ أَكْثَرُ مِنْ عَدَدِ الْحَصَى]     رواه أحمد]

 

[Lailatu Al-qadr ni tarehe ishirini na saba au ishirini na tisa, hakika Malaika usiku huo ni wengi sana katika ardhi kuliko idadi ya changarawe za mawe]    [Imepokewa na Ahmad.].

4. Ni usiku wa amani.
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ}     القدر:4}

 

[Ni amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya alfajiri ]   [Al-qadr – Aya 5].

Yaani usiku wote huo ni kheri tupu, hakuna shari kutoka mwanzo wake hadi kupambazuka kwa alfajiri.

5. Ni usiku wenye baraka.
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ}    الدخان:3}

 

[Kwa yakini tumeteremsha (Qur’ani) katika usiku uliobarikiwa – bila shaka Sisi ni waonyaji]   [Ad-Dukhan – Aya 3].

Ibn Abbas radhi za Allah ziwe juu yake  Asema: ”Yaani: Usiku wa Lailatu Al-qadr”.

6. Ndani ya usiku huu ndiyo yanakadiriwa makadirio ya mwaka mzima.
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ}     الدخان:4}

 

[Katika (usiku) huu hubainishwa kila jambo la hikima]    [Ad-Dukhan – Aya 4].

7. Atakayesimama kufanya ibada katika usiku huu hali ya kuamini na kutarajia malipo atasamehewa madhambi
Amesema Mtume :

 

مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ]       رواه البخاري ومسلم]

 

[Atakayesimama (kufanya ibada) usiku wa Lailatu Al-qadr kwa imani na kutarajia malipo, basi atasamehewa yote yaliyotangulia katika madhambi yake]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575025
TodayToday3092
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 26

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682920522ecbf3412448801747525714
title_682920522ee042480342491747525714
title_682920522ef4012374600931747525714

NISHATI ZA OFISI

title_6829205230f7e10037581331747525714
title_68292052310a911315027741747525714
title_68292052311cf3535101861747525714 Add content here

HUDUMA MPYA

: 4 + 7 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com