Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


AINA ZA IBADA YA HIJA 

Aina za ibada ya Hija ni Aina Tatu:

1. Tamattu:
Nayo ni ahirimie Umra katika miezi ya Hijja mpaka amalize na ajitoe kwenye ihramu yake, kisha katika mwaka huohuo ahirimie Hija.

Na mwenye kufanya tamattu’ anapo fika makka atafanya amali ya Umra nayo: Nikutufu, na kufanya sai kati ya Swafaa na marwa, na kunyoa au kupunguza, kisha atajitoa kwenye ihramu yake na avae nguo zake, ikifika tarehe nane mwezi wa mfungotatu, atahirimia hija kisha atafanya amali za hijja na atawajibika kuchinja kwa kupumzika kwake

2. Qiraan:
Nayo ni ahirimie Hijja na Umra kwa pamoja., au ahirimie Umra kisha anuilie kufanya hija kabla ya kuanza kufanya tawafu, na mwenye kufanya Qiraan atabaki kwenye ihramu yake mpaka amalize kufanya hija, na atalazimika kuchinja kwa kule kuhirimia pamoja kwa amali ya hija na umra.

3. Ifraad:
Nayo ahirimie Hijja peke yake.na mwenye kufanya ifraadi atabaki na ihramu zake mpaka amalize kuhuji na hatolazimika kuchinja.

Na nusuk bora katika hizo tatu ni tamattu kwa sababu Mtume ﷺ Aliwaamrisha maswahaba zake wafanye tamattu  [Kwa hadithi iliyopokewa na Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake iliyoko kwenye Sahihi ya Muslim.] Kisha ni Qiraan kisha ni Ifraad


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575117
TodayToday3184
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 7

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68292eacd3e0f3800299341747529388
title_68292eacd3f6e7411854271747529388
title_68292eacd410116770196831747529388

NISHATI ZA OFISI

title_68292eacd62bc9194100731747529388
title_68292eacd641115363953591747529388
title_68292eacd65559595469331747529388 Add content here

HUDUMA MPYA

: 11 + 9 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com