JE? KUNA SWAHABA YOYOTE AMBAE HAKUOWA KWA SABABU YA KUTAFUTA ELIMU
Suali : Jee kuna swahaba yoyote ambae hakuoa kwa sababu ya kutafuta Elimu?
Jawabu : Mtume ﷺ amependekeza jambo la kuoa (nikah) na ameliamrisha na kulitilia mkazo kwani amepokea Imamu Al Bukhary (5063) na Imamu Muslim (1401) kutoka kwa Anas radhi za Allah ziwe juu yake asema:
أَنَّ نَفَرًا مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَأَلُوا أَزْوَاجَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ عَمَلِهِ فِي السِّرِّ؟ ، فَقَالَ بَعْضُهُمْ: لَا أَتَزَوَّجُ النِّسَاءَ ، وَقَالَ بَعْضُهُمْ : لَا آكُلُ اللَّحْمَ ، وَقَالَ بَعْضُهُمْ: لَا أَنَامُ عَلَى فِرَاش ٍ، فَحَمِدَ اللهَ وَأَثْنَى عَلَيْهِ ، فَقَالَ: (مَا بَالُ أَقْوَامٍ قَالُوا كَذَا وَكَذَا ؟ لَكِنِّي أُصَلِّي وَأَنَام ُ، وَأَصُومُ وَأُفْطِرُ ، وَأَتَزَوَّجُ النِّسَاءَ ، فَمَنْ رَغِبَ عَنْ سُنَّتِي فَلَيْسَ مِنِّي
[ya kwamba kikundi katika maswahaba walikuja kuwauliza wake za Mtume kuhusu matendo yake ya siri? Wakasema baadhi yao: sitoowa wanawake, na wakasema baadhi yao: sitokula nyama. Na wakasema baadhi yao: sitolala katika tandiko (godoro). Mtume (aliposikia na kuwaita) akamhimidi Mwenyezi Mungu kisha akamsifu kisha akasema [wana nini baadhi ya watu wamasema kadha wa kadha ? Lakini mimi naswali na ninaalala, na ninafunga na ninakula (siku nyingine) , na naoa wanawake, yule ambae atakua mbali na sunna yangu basi sio katika mimi].
Na amepokea Ibnu majah (1846) kutoka kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume ﷺ
[النِّكَاحُ مِنْ سُنَّتِي ، فَمَنْ لَمْ يَعْمَلْ بِسُنَّتِي فَلَيْسَ مِنِّي]
[Nikah " kuoa" ni katika sunna yangu basi yule asieifanya sunna yangu sio katika mimi] hadithi hii ameisahihisha na Sheikh Albany katika "Sahih ibnu Majah"
Wala hatujui yeyote katika maswahaba ambae hakuoa kwa sababu ya kutafuta elimu au kwa ajili ya kuieneza.
Na wanazuoni wa maswahaba waliopokea hadithi, na ikachukuliwa kwao elimu na fiqhi,na wanafunzi wao,wote walioa, wala hatujui hata mmoja kati yao alieacha kuowa, au aliwaamrisha wanafunzi wake kutooa ili ajishughulishe na elimu na darsa na mambo mengine.
Na miongoni mwa hao ni makhalifa wanne Abubakar, na Omar, na Uthman, Ali radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote.
Na miongoni mwao ni:Viongozi wa jeshi , kama vile Amru binl' Aas , na Abu ubaydah bin Al jarraah, na khalid bin Al Walid, na Shurahbiil bin Hasanah na wengine radhi za ALLAH ziwe juu yao wote.
Na vile vile :Maswahaba waliopokea hadithi nyingi zaidi za Mtume ﷺ, kama vile Abu hureirah ,na Abu saeed , na Anas bin Maalik ,na Abdallah bin Omar , na Abdallah bin Abbas , na Abdallah bin Amru na wengine radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao.
Na amepokea Al Tirmidhy (3790) kutoka kwa Anas bin Malik amesema : Amesema Mtume ﷺ:
أَرْحَمُ أُمَّتِي بِأُمَّتِي أَبُو بَكْرٍ، وَأَشَدُّهُمْ فِي أَمْرِ اللَّهِ عُمَرُ، وَأَصْدَقُهُمْ حَيَاءً عُثْمَانُ بْنُ عَفَّانَ، وَأَعْلَمُهُمْ بِالحَلَالِ وَالحَرَامِ مُعَاذُ بْنُ جَبَلٍ، وَأَفْرَضُهُمْ زَيْدُ بْنُ ثَابِتٍ، وَأَقْرَؤُهُمْ أُبَيُّ بْنُ كَعْبٍ، وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَمِينٌ ، وَأَمِينُ هَذِهِ الأُمَّةِ أَبُو عُبَيْدَةَ بْنُ الجَرَّاحِ
[Mwenye huruma zaidi na umma wangu katika umma wangu ni Abubakar, na mwenye mkazo zaidi katika amri za Mwenyezi Mungu kushinda wote ni Omar, na mwenye haya ya ukweli kushinda wote ni Uthman bin Affan,na mjuzi zaidi wa halali na haramu kushinda wote ni Muadh bin Jabal,na mwenye ujuzi zaidi wa elimu ya mirathi kushinda wote ni Zaid bin Thabit , na msomaji zaidi wa Qur'ani kushinda wote ni Ubay bin Ka'ab, na kila umma una muaminifu na muaminifu wa umma huu ni Abu Ubayda bin Al Jarrah]
Hadithi hii ameisahihisha Sheikh Albany katika " sahih Al Ttirmidhy"
Na hawa wote walioa na miongoni mwao ni Muadh bin Jabal radhi za ALLAH ziwe juu yake mjuzi zaidi wa halali na haramu katika umma huu.
Na mwenye kutafuta elimu atakuta yakwamba katika hiyo elimu anayoitafuta kuna yanayohimiza mtu kufunga nikah "ndoa" na kulisisitiza jambo hili, na mwenye kukusanya baina ya kutafuta elimu na kuoa basi amekusanya vizuri viwili , na amewaiga Maimamu wa dini katika Maswahaba na wafuasi wao na wenye kuwafwata hao kwa wema.
Na Allah ndie mjuzi zaidi.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.