MKE AKILAZWA HOSPITALI AU AKAENDA KUWAZURU FAMILIA YAKE JE HAKI YAKE KATIKA ZAMU ITAANGUKA?
Suali: Sheikh nina suali kuhusu uadilifu baina ya wake nayo ni katika hali mbili
1- alikua mgonjwa mmoja wao na akalazwa hospitalini kwa mda wa siku tano na katika kipindi hicho nilikua nalala kwa mke mwengine sasa jee ni wajibu kwangu kumlipizia kwa idadi ya siku hizo alizokua hospitalini?
2- katika hali ya mmoja wao kwenda kuwazuru familia yake kwa siku kadhaa jee ni haki kutaka kukaa na mume kwa idadi ya siku zile alizokua kwa familia yake?
Jawabu:
Kwanza mke akilazwa hospitalini kwa siku kadhaa ,basi hastahiki kugawanyiwa siku hizi ambazo yuko hospitalini; kwa sababu yeye ndie alieipoteza haki yake,na kumlazimisha mumewe kwake abaki na yeye hospitalini ili amtimizie siku zake ni kumdhuru mume.
Pili: Ikiwa mke atakwenda kuwazuru familia yake kwa siku kadhaa,au akasafiri kwenda sehemu fulani,ikiwa ni kwa ajili ya mahitaji yake basi mume hatomtimizia siku hizo,ama ikiwa ni kwa ajili ya mahitaji ya mume basi atamtimizia siku hizo.
Imekuja katika [Al mausuuatul fiqhiyyah.] [ 33/202] "Mke huenda akaipoteza zamu yake kwa ajili ya safari yake.hapa kuna ufafanuzi kwa wanazuoni wa Madhehebu ya Imamu Shafi'i na Imamu Ahmad bin Hanbali) wakasema mke akisafiri bila ya idhini ya mume wake kwa ajili ya haja zake au hata haja za mume wake au sababu zengine basi hana zamu.kwa sababu zamu ni kwa ajili ya kuliwaza, na yeye ndio sababu ya kutopatikana kwa kuondoka kwake hivyo basi zamu hii imepotea haipo.
Na ikiwa amesafiri kwa idhini ya mumewe na kwa ajili ya mahitaji yake basi atamtimizia siku zilizompita alizokaa huko kwa sababu amesafiri kwa idhini yake na kwa ajili ya mahitaji yake,kwani yeye ni kama yuko kwake na chini ya milki ya mumewe,na yeye mume ndie amejizuilia nafsi yake kwani yeye ndio amemtuma.
Na ikiwa mke amesafiri kwa idhini ya mume wake lakini kwa ajili ya mahitaji yake hatotimiziwa na mumewe hizo siku kwa mujibu wa wanazuoni wa madhehebu ya Imamu Ahmad bin Hanbal) na wanazuoni wa madhehebu ya Imamu Shafi'i katika kauli ya pili) kwa sababu yeye mke ndie aliepoteza haki yake ya kustarehe nae, na hakua katika milki ya mumewe,na na kule kumruhusu kwake kusafiri ni kutopata madhambi.
Na lau mke atasafiri kwa idhini ya mume wake kwa ajili ya mahitaji yao wote wawili haki yake haijaanguka kama alivyosema mwanachuoni (Zarkashy) na wengineo kuhusu nafaqah ya mke na hivyo hivyo kuhusu zamu,tofauti na alivyosema (ibnul Immaad) yakwamba zamu yake inaanguka na inakua haipo tena."
Na pia Angalia [Al sharhul mumti'i] [12/433] **
Na Allah ndie Mjuzi zaidi.
** Chanzo: Hii ni Fatwa ya Sheikh Mahammad Swaleh Al Munajid
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.