Menu

 

NI ZIPI AIBU AMBAZO YAFAA KUZIDHIHIRISHA KWA ALIEPOSA?

 

Suali : Nina maradhi ya nafsi kwa miaka kadhaa sasa.na kwa mda sasa nahifadhi swala zangu nasoma Qur'ani na namtaja Mwenyezi Mungu na natoa sadaka na nawasaidia watu sana,na hali yangu imekua nzuri na nafuu sana lakini nahisi kuna chanzo cha maradhi katika mwili wangu, jee ni wajibu kwangu kumueleza aliekuja kuniposa kuhusu jambo hilo?

Jawabu: Alhamdulillah tunamuomba ALLAH akuponye na akupe afya inavyoonekana maradhi yako haya ni jambo la kudhania tu na hayapatikani kiuhakika katika maisha yako.Na lau tutakisia yakwamba maradhi hayo yapo: twasema: Ikiwa haya hayaathiri maisha ya ndoa,wala hayaathiri malezi ya watoto basi haina haja kumueleza aliekuja kuposa kuhusu maradhi hayo.Ama ikiwa maradhi hayo yana athari baada ya ndoa kwa kuleta madhara baada ya ndoa na kupitia maradhi hayo hakutakua na mapenzi na utulivu basi ni lazima kumueleza mposaji kuhusu hilo.Na kulificha jambo hilo inahesabika ni katika udanganyifu na limekuja katazo la udanganyifu kwa ujumla katika hadithi iliyopokelewa na Abu hureira yakwamba Mtume Muhammad anasema:

 

مَنْ غَشَّ فَلَيْسَ مِنِّي]     رواه مسلم]

 

[Atakaefanya udanganyifu sio katika mimi]     [Imepokelewa na Imam muslim]  No. (102)
Na usitilie maanani dhana na fikra potovu kuhusu maradhi yako aghlabu ya hayo ni vitimbi vya sheitani na hila zake,ili akuzuie na ndoa na kuitunza nafsi na machafu.
Na msingi wa kumueleza mposaji kuhusu maradhi ya mposwaji.
A) Yawe maradhi yale yanaathiri maisha ya ndoa na yanaathiri kutekeleza kwake haki za mume na watoto.
B) Yawe yanamchukiza mume kwa mandhari yake au harufu yake.
C) Yawe maradhi ya uhakika tena ya kudumu sio ya kudhania na ya kuja kwa mda na kisha yataondoka baada ya mda fulani au baada ya kuolewa.
Na waliulizwa wanazuoni wa kamati ya kudumu ya fatwa nchini Saudi Arabia.
"Kuna binti kijana hua anapatwa mara kwa mara na uwenda wazimu kisha inamuondokea baadae na anarudi katika hali yake ya kawaida kwa mda mrefu au mfupi.Na hua posa zinamjia lakini inakua ngumu kuolewa kwake kutokana na kwamba familia yake hawajui wamueleze nini mwenye kuposa kutokana na hali aliyo nayo binti yao. Jambo ambalo linamkosesha fursa ya kuolewa binti huyu na mwishoe familia yake wanapendelea kumuozesha binti yao kwa mtu mwenye ulemavu au mwenye udhuru huenda akamkubali binti yao kwa urahisi .na sasa kuna mposaji ana udhuru yeye ni tasa na kuna mposaji mwengine ambae ni mtoto wa shangazi yake ambae amekuja kumposa huku akijua maradhi yake yale binti. Isipokua tatizo ni kwamba mamake huyu kijana ambae ni shangazi yake binti nae ana maradhi yale yale kama ya binti.na tulipomuuliza daktari kuhusu ndoa kama hii akasema kwamba haipendelei kutokana kwamba kuna uwezekano mkubwa wawili hawa wakioana na wao wakazaa wenye maradhi hayo.
Swali sasa ni: Je ni ipi hukmu ya kisheria kuhusu ndoa hii? Na jee akizaliwa mtoto mgonjwa itakuwa tumemdhulumu yule kijana,?  Kwa sababu tutakua tumechangia kufanyika kwa ndoa kama hii,pamoja na kujua kwetu kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuzaliwa watoto wenye ugonjwa.
Wakajibu: "haifai kumzuia na kumyima binti kuolewa,na mumuozeshe huyu alekuja kumposa kisha muegemeze jambo lenu kwa ALLAH na muwache maneno ya daktari ambayo ni ya kukisia tu; na hilo ni kutoka na maslahi yanayopatikana katika ndoa baina ya pande zote mbili kijana na binti,na kumlinda binti na hatari ya kukaa peke yake bila ya ndoa,kwa sharti la binti kumridhia huyu mume ambae walii wake ameridhia amuoe"  imeisha
Sheikh Abdul aziz bin baaz,Sheikh Abdul razaq Afiify,Sheikh Abdallah bin Ghadyaan,Sheikh Swaleh Al fawzaan,sheikh Abdul aziz Aal sheikh.
"Fatwa za kamati ta kudumu" (18/194)
Na aliulizwa Sheikh Muhammad Swaleh Al Uthymeen ALLAH amrehemu:
Mtu amemposa mwanamke na mwanamke huyu anajulikana ana aibu ya kimaumbile,lakini aibu hii imefichikana haiko bayana wazi wazi,na aibu hii inatarajiwa kuondoka kwa tiba kama vile mbalanga je mwenye kuposa ataambiwa kuhusu aibu hii?
Akajibu: "Mtu akiposa mwanamke na ana aibu iliyofichika na kuna mtu anatambua kuhusu aibu ile: akiuliza mwenye kuposa kumhusu mwanamke yule ni wajibu kwake kumbainishia na kumuwekea wazi aibu ile, na hili liko wazi,na hata kama hakuuliza atamuelezea hivyo hivyo. Kwa sababu jambo hili ni katika mlango wa nasaha, haswa ikiwa ni katika jambo ambalo haitarajiwi kuondoka,ama ikiwa ni jambo ambalo linatarajiwa kuondoka: basi ni jepesi zaidi, lakini kuna vitu ambavyo vinaweza kuondoka na kupona lakini pole pole kama vile mbalanga mfano - ikiwa ni kweli yaondoka- mimi mpaka sasa sijajua kama yaondoka,hivyo basi inatofautishwa kati ya maradhi ambayo inatarajiwa kupona karibuni na ambayo inatarajiwa kupona baada ya mda mrefu"
Imeisha.
(Liqaatul baabul Maftuuh) (5/ swali namba 22)

hizi ndozo fatawa za wanachuoni kuhusu aibu zinazofaa kumjulisha aliekuja kuposa.

 

Na Allah ndie Mjuzi zaidi


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575486
TodayToday193
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 9

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6829882f889389042147841747552303
title_6829882f88a4618989914791747552303
title_6829882f88b4c2959870761747552303

NISHATI ZA OFISI

title_6829882f8a47412538912271747552303
title_6829882f9c0a78771424171747552303
title_6829882f9c1bd13972653941747552303 Add content here

HUDUMA MPYA

: 6 + 7 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com