JE YAFAA KUMUOMBEA DUA KAFIRI ANAEPENDA UISLAMU ??
Suali: Mtu akiwa si muislamu lakini anapenda uislamu na waislamu na kuwataja vizuri. Je mtu huyu akifa inafaa kumuombea dua?
Jawabu: Mtu akiwa hakupiga shahada ya kushuhudia kuwa Mwenyezi mungu ni mmoja na kuwa Mtume muhammad ni Mtume wa Mwenyezi mungu huwa bado hajakuwa Muislamu hata kama alikuwa akijua kuwa uislamu ni dini ya haki,au ni dini yenye mafunzo mazuri, hilo halimfanyi kuwa ni muislamu.
Huyu hapa Ammi yake Mtume ﷺ alikuwa akijua kuwa Uislamu ni dini bora,na aliwahi kutunga mashairi ya kuusifu Uislamu,lakini yeye hakusilimu kwa kuogopa lawama za watu,na alipo kufa Allah Subhana wataala alimkataza Mtume kumuombea msamaha kwa sababu alikufa kafiri Allah anasema:
مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ} التوبة:113}
"Haimpasii Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni." [Al-Tawba:113]
Na Allah ndie mjuzi zaidi
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.