JE YAFAA KWA MWANAMKE ALIE KWENYE HEDHI KUOSHA MAITI?
Hakuna aya wala Hadithi inayomkata Mwanamke alie kwenye Hedhi kuosha Maiti,au kuhudhuria anapooshwa Maiti,wala hatujui Hadithi kutoka kwa Bwana Mtume ﷺ kuhusu jambo hili,wala hatuji yoyote katika Wanachuoni walioharamisha jambo ilo isipokuwa imepokewa kwa baadhi ya wema waliotangulia kama Hasan Al Basari na Ibnu Siriin wamechukia jambo hilo,kama alivyo pokea Ibnu Abii Shayba katika Muswannaf yake
Chanzo: islamweb.net
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.