Menu

HUKMU YA KUFANYA KAZI KATIKA JUMBA LA KAMARI


Msichana anauliza kuhusu kufanya kazi katika nyumba la kamari (Casino).
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 23 na nimepata kazi katika casino sasa ni nini hukmu ya kufanya kazi katika casino na maana ya casino ni jumba la kamari ,na majumba haya ya kamari yameenea sana nchini kwetu , kwani katika kila hoteli kubwa kuna jumba ambalo wanafanya kazi ndani yake wafanyi kazi wengi kwa mishahara mikubwa sana
Na kazi katika katika jumba hili la kamari ziko aina nyingi:
1- mapokezi : na huyu kazi yake ni kuchukua nakala ya kitambulisho cha mwenye kucheza kamari na kubuki nafasi na kufunga hisabu za mwezi bas.
2- na kuna wengine wanajifunza kucheza kamari na wanacheza na wateja kwa maslahi ya kampuni, na kuna wanaowasimamia hawa, na pia kuna wanaofanya kazi katika baa hawa kazi yao ni kupeleka vyakula,vinywaji na pombe kwa wateja, na pia kuna walinda usalama, na wafanya usafi, na kuna wafanyi kazi katika mahusiano ya jamii kazi yao hawa ni kuwaleta wateja.
Nataka kujua hukmu ya kazi za hawa wote? Pamoja na kuchunga hali ya kiuchumi ambayo tunaipitia na pia kuchunga idadi kubwa ya vijana wa kiume na wa kike wanaofanya kazi humo na mishahara ya juu.
Imeenezwa tarehe 25/12/2005.
Alhamdulillah.
Kwanza:
Sio jambo la shaka kwa muislamu yeyote yakwamba Mwenyezi Mungu ameharamisha pombe na kamari akaifanya ni katika madhambi makubwa Mwenyezi Mungu anasema

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالأَنْصَابُ وَالأَزْلامُ رِجْسٌ مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ * إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ وَعَنِ الصَّلاةِ فَهَلْ أَنْتُمْ مُنْتَهُونَ

 

[Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?" ]   [Al maidah 90-91]

Pili: Mwenyezi Mungu anapoharamisha kitu basi anaharamisha pia kusaidiana katika jambo hilo na kupeana msaada katika jambo hilo kwa njia yeyote ile ALLAH anasema

 

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى وَلا تَعَاوَنُوا عَلَى الإثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ }    المائدة/2}

 

[Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.]  [Al Maidah 2.]
Na msingi kwa wanazuoni wa sheria ni kwamba "vitu vinavyokupeleka kwenye lengo fulani basi vina hukmu sawa na lengo lenyewe" hivyo basi kila jambo linalosababisha kupatikana jambo la haramu au likapelekea katika haramu nalo ni haramu.
Tatu:Haifai kwa Muislamu kupatikana sehemu ambayo Mwenyezi Mungu anaasiwa isipokua kwa dharura au kwa kulazimishwa , na ni wajibu kwake kukemea uovu huo na aubadilishe na auondoe, na kama hatoweza basi atalazimika kuondoka mahali pale , kwani linalo wajibika kwa Muislamu ni kuondoka na kuepuka sehemi ambazo zina maasi na sio kuwasaidia watu wale katika kumuasi Mwenyezi Mungu, na kukaa katika sehemu hizi kunapingana na amri ya Muislamu kukataza uovu pale anapouona, na pia inapingana na amri ya kuhama sehemu zenye uovu na maasia.
Mwenyezi Mungu anasema:

 

وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّى يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ إِنَّكُمْ إِذاً مِثْلُهُمْ  النساء:140

[Naye amekwisha kuteremshieni katika Kitabu hiki ya kwamba mnapo sikia Aya za Mwenyezi Mungu zinakanushwa na zinafanyiwa kejeli, basi msikae pamoja nao, mpaka waingie katika mazungumzo mengine.]    [Annisaa:140.]

Anasema Imama Qurtuby ALLAH amrehemu katika neno lake Mwenyezi Mungu "Musikae nao mpaka wazungumze maneno mengine" Yaani maneno ambayo sio ya kufru "nyinyi basi ni kama wao" hili linaonyesha ulazima wa kujiepusha na watu wa maasi ikiwa utadhihiri kutoka kwao uovu , kwa sababu yule asiejiepusha nao basi ameridhia matendo yao, na kuridhia ukafiri ni ukafiri Mwenyezi Mungu anasema "nyinyi basi ni mfano wao" hivyo basi yule atakaekaa kikao cha maasi , na hajawakanya ni kuwakataza katika uovu wao basi atapata madhambi sawa na wao.

Na inafaa awakataze na awakemee wanapozungumza jambo la maasi au wakalitenda kwani yule asieweza kuwakataza na kuwakemea basi inampasa anyanyuke na aondoke katika kikao hicho ili asiwe katika watu wa aya hii."

Na imepokewa kutoka kwa Umar bin Abdulaziz radhi za ALLAH ziwe juu yake yakwamba aliwakamata watu wakiwa wanakunywa pombe, akaambiwa kwamba mmoja wao amefunga akampiga kwa kumtia adabu kisha akasoma aya hii "Nyinyi basi ni mfano wao" kwa maana yakwamba kuridhia maasi pia ni maasi. Imeisha kutoka katika Tafsiri ya Qurtuby [5 Uk. 418.]

Na anasema Sheikh Ibnu Baaz ALLAH amrehemu:
"Kukemea maovu kwa moyo ni lazima kwa kila mmoja, nayo ni kuchukia huo uovu, na kujitenga na wenye kuufanya inaposhindikana kuukemea na kuukataza huo uovu kwa mkono na ulimi "
"Al Duraru Ssaniyyah fil ajwibah Annajdiyyah" [16 Uk. 142]

Pia inahofiwa kwa yule mwenye kufanya kazi sehemu kama hizi imani yake kupungua ,na uwivu kuondoka kutoka katika moyo wake , na huenda sheitani akamshawishi kutenda maasi , na Mwenyezi Mungu anasema:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ وَمَنْ يَتَّبِعْ خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ فَإِنَّهُ يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ وَالْمُنْكَرِ}    النور/21}

 

[Enyi mlio amini! Msizifuate nyayo za Shet'ani. Na atakaye fuata nyayo za Shet'ani basi yeye huamrisha machafu na maovu.]    [Annuur: 21].

Nne: Kwa utangulizi tulioeleza, itakuwa haifai kwa Muislamu kufanya kazi katika jumba hili la kamari , kwani yeye kufanya hivyo ni kusaidia katika kuasiwa Mwenyezi Mungu na anakua ni mwenye kuridhia jambo hili au anakua katika hukmu ya mwenye kuridhia jambo hili la kamari, na hili linakusanya kila anaefanya kazi katika hili jumba la kamari, inakusanya anaecheza na wateja au anawafundisha au anawalinda au anawahudumia au anawapokea na nyadhifa nyengine zisizokua hizi, na asighurike Muislamu kwa yale anayopata katika mali kwani atakwenda kuulizwa siku ya kiyama kuhusu mali wapi ameyachuma na vipi ameyatumia.

Na kitu ghali sana na chenye thamani kwa Muislamu ni dini yake hivyo basi ni wajibu kwake kuihifadhi dini yake na asiwe ni mwenye kuiuza dini yake kwa starehe duni za dunia zenye kupita na kuondoka.

Na hii ndio hukmu nayo ni kuharamisha kufanya kazi katika majumba kama haya ya kamari, na haswa kwako wewe muulizaji ni haramu zaidi unajua kwanini??

Kwa sababu wewe ni Mwanamke na uwezo wako wa kustahmili na kupambana ni mdogo kushinda wa Mwanamume , na tamaa ya wafisadi kwako ni nyingi , na atajiamini vipi binti mwenye umri kama wako juu ya nafsi yake akipata miongoni mwa hawa wapotevu katika haya majumba yatakayomchanganya katika pombe ulevi na matamanio.

Hivyo basi tunakusihi ewe muulizaji uitikie muito wa sheria na akili , usikaribie sehemu hizo , ili ujihifadhi na uhifadhi kitu cha thamani unachokimiliki.
Na kumbuka maneno ya Mwenyezi Mungu:

 

 وَمَنْ يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَلْ لَهُ مَخْرَجاً * وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لا يَحْتَسِبُ وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً الطلاق/2- 3

 

[Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea.Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.]   [Al Twalaq:2-3]

Na kwa neno lake Mutme ﷺ:

 من ترك شيئا لله عوضه الله خيرا منه }   صححه الألباني}

 

[Yule atakae acha kitu jwa ajili ya Mwenyezi Mungu  basi Mwenyezi Mungu atampa mbadala yake bora kushinda alichokiacha] ameisahihisha Albany.

Na usisahau yakwamba nafsi haitokufa mpaka ikamilishe rizki yake hivi karibuni au baadae.

Tunamuomba ALLAH akusaidie kuiacha kazi hii tena kwa kupenda mwenyewe na a kushinda hiyo.*


Chanzo ni Fatwa ya Sheikh Swaleh Al Munajjid* 

Na kufanya Tarjam na Ustadh Fadhil Muhammad

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575485
TodayToday192
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 9

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6829882f889389042147841747552303
title_6829882f88a4618989914791747552303
title_6829882f88b4c2959870761747552303

NISHATI ZA OFISI

title_6829882f8a47412538912271747552303
title_6829882f9c0a78771424171747552303
title_6829882f9c1bd13972653941747552303 Add content here

HUDUMA MPYA

: 3 + 4 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com