Menu

KUPEWA UTUME NA KUSHUKA KWA WAHYI


hqdefault 66


Mtume alipotimiza umri wa miaka arobaini, ambayo ni kilele cha ukamilifu na ndio miaka ya kupelekwa Mitume, alama za Utume zilianza kudhihiri na kumeremeta kwake kutoka upeo wa maisha.

Alama hizo ni pamoja na kuota kwake ndoto za ukweli, ikawa haoti ndoto yoyote isipokuwa hutokea, mfano wa mpasuko wa Al-fajiri kwa uwazi wake. Hali hiyo iliendelea kwa muda wa miezi sita. Muda wa Utume wake ulikuwa ni miaka ishirini na mitatu, kwa hiyo ndoto hizi zilikuwa ni sehemu moja katika sehemu arubaini na sita za Utume. Ilikuwa mwezi wa Ramadhani katika mwaka wa tatu tokea kujitenga kwake Mtume  alipokuwa katika pango la Jabal Hiraa, wakati Mwenyezi Mungu Mtukufu Alipoamua Kuimimina Rehema Yake kwa walimwengu, kwa hivyo akamkirimu mja wake Utume na kumteremsha kwake Jibril (a.s) na aya za Qur'ani.
Baadhi ya wataalamu walichunguza na kupitia vielelezo na dalili mbalimbali, waliweza kutambua kuwa siku hiyo ilikuwa ni siku ya Jumatatu, kwa siku ishirini na moja zilizopita katika mwezi wa Ramadhani, zinazoafikiana na tarehe 10/8/610 C.E. Wakati huo Mtume alikuwa na umri wa miaka arubaini na miezi sita na siku 12 kwa mwenendo wa mwezi, na muda huo inasemwa ni kiasi cha miaka 39 miezi mitatu na siku ishirini na mbili kwa mwenendo wa jua. 


*Arraheeq Al Makhtum 100-101


 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575396
TodayToday103
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 7

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68297532af4102833445941747547442
title_68297532af4fa1145341371747547442
title_68297532af5db11216794871747547442

NISHATI ZA OFISI

title_68297532b0bd113682418491747547442
title_68297532b0cb75085649641747547442
title_68297532b0d9e20548923851747547442 Add content here

HUDUMA MPYA

: 7 + 1 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com