Menu

KATIKA PANGO LA HIRAA


download 3


Wakati Mtume alipofikisha umri wa miaka arobaini, alikuwa ni mmoja miongonimwa watu waliokomaa kiakili na kifikra kati ya jamaa zake, yeye alipendelea sana kujitenga, alikuwa akichukua chakula chake na maji na kwenda kwenye pango la Hiraa katika Jabal Nuru, kiasi cha maili mbili kutoka Makka.

Jabal Nuru ni pango lililo katika mazingira mazuri, urefu wake ni kiasi cha yadi nne, na upana wake ni kiasi cha yadi 1.75. Watu wa nyumbani kwake walikuwa karibu naye, mwezi wa Ramadhani alikuwa akifanya kazi hapo na alikuwa akiwalisha maskini waliokuwa wakimwendea na akiutumia wakati wake katika ibada na kufikiria juu ya mambo yanayomzunguka katika vitu vyenye kuonekana katika ulimwengu huu, na uwezo uliojaalia vitu vyote hivyo katika maumbile ya ajabu kabisa. Hakuwa na raha kuwaona watu wake katika hali walizokuwa nazo, walikuwa wakifuata itikadi za kishirikina, itikadi iliyo mbovu na dhaifu kwa hoja. Wakati wote huo mbele yake hakukua na njia iliyo wazi au utaratibu wa maisha ulio na mipaka au mfumo maalum, wala njia yenye kunyooka ambayo ingetuliza moyo wake na kumridhisha. 

Kujitenga kwa Mtume : kulikuwa ni sehemu ya mipango ya Mwenyezi Mungu kwake, ili amuandae kwa lile jambo ambalo Alimkusudia, katika mambo makubwa. Kwa vile Mwenyezi Mungu Alikuwa Amekusudia Mtume aathiri maisha ya watu  na kuwabadilisha watu katika mwelekeo mwingine, ilikuwa hakuna budi isipokuwa kwa roho hiyo kujitenga na watu kwa muda, na kujitenga na shughuli za kidunia na mazonge ya kimaisha na tamaa nyingine ndogo za watu zilizokuwa zinawashughulisha kimaisha. 

Hivi ndivyo alivyopanga Mwenyezi Mungu , Kumpangia Muhammad wakati Akimuandaa kubeba Amana kubwa ya kufikisha ujumbe ambao umegeuza hali ya dunia na kuandika historia mpya. Mtume alijitenga kwa muda wa miaka mitatu, kabla ya kupewa dhamana ya ujumbe kwa watu wote. Wakati mwingine alikuwa akijitenga kwa muda wa mwezi, akiwa peke yake na nafsi yake huru, akiyazingatia mambo yaliyo ndani ya huu ulimwengu wenye kuonekana katika siri iliyofichwa, mpaka ulipofika muda wa kushiriki katika siri hiyo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.


* Rahmaiul-Lil-t Alamivn, Juzuu 1, Uk. 4 na lbn Hisham, [uzuu I, Uk 230-235
na Fidhilal-l- Qur'an, [uzuu 2, Uk. 166

Raheeq Al Makhtum 99-100


 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575389
TodayToday96
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 14

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68297532af4102833445941747547442
title_68297532af4fa1145341371747547442
title_68297532af5db11216794871747547442

NISHATI ZA OFISI

title_68297532b0bd113682418491747547442
title_68297532b0cb75085649641747547442
title_68297532b0d9e20548923851747547442 Add content here

HUDUMA MPYA

: 13 + 6 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com