Menu

HUKMU YA KUKAUKA KWA NGUO ILIO NAJISIKA


 

Swali: Ni nini hukumu yanajisi iliokauka na kupotea athari yake. Kama vile rangi au harufu na kadhalika.

Jibu: Nguo ilioingia najisi kisha ikikauka na kupotea athari ya najisi kama vile rangi au harufu au tamu kwa kupigwa na jua au kwa jambo lolote lile kwa msimamo wa jamhuri ya wanchuoni ni kuwa nguo haitwahiriki kwa kukauka ni lazima itwahrishwe kwa Maji.
Pia wameenda baadhi ya wanachuoni wakasema kuwa najisi ikiondoka na kupotea athari yake kama vile rangi au harufu au tamu yake basi chombo kile huwa ni twahara.

Kwa sababu lengo la kuondoa najisi ni kuondosha ile najisi ilioko kwenye nguo ikiwa itaondoka kwa kitu chochote kile kama banzin au mafuta ya taa basi kitu kile hutwahirika.
Ameulizwa Sheikh Ibnu Uthaymin Mungu amrehemu katika Majmuuil Fatawa. "Je najisi hutwahirika kwa kitu kingine kisichokuwa maji? Na bukhari inaosafishiwa nguo kwenye sehemu za kufulia nguo ni yenye kutwahirisha?

"Akajibu kuondosha najisi si ibada iliokusudiwa, bali ni kuondosha ule uchafu wa najisi kwa hivyo kitu chochote chenye kuondosha najisi na ikaondosha na kuondosha athari yake, basi huwa kitu kile ni chenye kutwahrisha najisi ile, sawa iwe ni kwa maji au petroli au kitu chochote chenye kuondosha,  uchafu wa njisi basi huhisabiwa ni chenye kutwahirisha. Hata kauli ambao ndio sawa alioichaguwa Sheikhul Islam Ibnu Taymiyah, lau najisi itaondoka kwa jua na upepo basi hutwahirika ile sehemu. Kwa sababu ni Kama nilivyosema uchafu wa wanajisi ukipatikana sehemu huwa sehemu ile ni najisi,na itakapoondoka sehemu ile hurudi kwenye asili yake, nao ni utwahara.

Kwa hivyo na kitu chochote chenye kuondosha najisi na athari yake, isipokuwa husamehewa rangi ilioshinda kuondoka. Kwa hivyo tunasema Bukhari inaosafishiwa nguo ikiwa itaondosha najisi basi huwa ni yenye kutwahirisha".
Kwa hivyo kupitia kwa misimamo hiyo miwili ya wanchuoni,najisi ikikauka na kupotea athari yake huwa kitu kile ni twahara, lakini msimamo wa jamhuri ni kujitoa kwenye shaka na khilafu

Na Allah ndie mjuzi zaidi.

 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6574702
TodayToday2769
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 13

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6828ff708ccaf18566864131747517296
title_6828ff708cd9d2685109901747517296
title_6828ff708ce7e10217083621747517296

NISHATI ZA OFISI

title_6828ff708e44411776653511747517296
title_6828ff708e5209465894791747517296
title_6828ff708e5f720084573761747517296 Add content here

HUDUMA MPYA

: 15 + 15 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com