Menu

 

 

JE MTU HULAZIMI KUOGA ANAPO MUINGILIA MKEWE KWA NYUMA?

 

SWALI: Mtu kumuingilia mkewe kwa tupu ya nyuma ni katika Madhambi Makubwa lakini mtu atakapo fanya hivyo hulazimika Kuoga kwa Mtazamo wa Mas'ala ya Fiqhi?

 

JAWABU: Mtu anapo muingilia mkewe kwa nyuma,pamoja na kuwa amefanya dhambi kubwa, vile vile hulazimika Kuoga. Wamelielezea hilo wanachuoni wote wa Fiqhi, kwa sababu tupu ya nyuma ya hisabiwa ni tupu. Mtu anapo muingingilia mkewe kwa nyuma hulazimika kuoga wote wawili aliyemuingilia na aliyeingiliwa.
Asema Imam Al-Nnawawiy Mungu amrehemu katika kitabu chake "Sharh-Al Muhadhab " Tumetaja ya kuwa Madh'habu yetu kuwa kumuingia mwanamke katika tupu yake ya mbele au ya nyuma au tupu ya mwanamume na myama hulazimika kuoga japo kuwa hatashusha (kutokwa na Manii) na hii ndio Kauli ya jamhuri ya wanachuoni,toka kwa mwaswahaba na Taabi'iin"

Na Amesema Ibnu Qudaamah Mungu Amrehemu katika kitabu chake Al-Mughniy " naye ni mwanchuoni wa Madhabu ya Hanbaliy "Na ni lazima Kuoga kwa kila mtu aliye Ingilia au aliyeingiliwa akiwa ni katika watu wanaolazimika Kuoga sawa iwe ni tupu ya mbele au ya nyuma aliyeingiliwa awe ni Mwanadamu au Mnyama,sawa awe yuko hai au ni Maiti, kwa Khiyari yake au ametendewa nguvu, akiwa Macho au amelela"
Kwa hivyo mtu anapo Muingilia mkewe kwa nyuma pamoja na kuwa ni Madhambi makubwa ni lazima kwake kuleta toba na vile vile hulazimika kuoga Janaba kama tulivyo nukuu kwa Wanachuoni.

Na Allah ndie Mjuzi zaidi


 

 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6574756
TodayToday2823
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 10

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682906a042d133491889771747519136
title_682906a042e7f14560102421747519136
title_682906a042fde20309396861747519136

NISHATI ZA OFISI

title_682906a0453c318032115411747519136
title_682906a04551613574023221747519136
title_682906a04565813407857951747519136 Add content here

HUDUMA MPYA

: 10 + 5 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com