Menu

HUKMU YA KUVAA NIQAAB KATIKA IBADA YA UMRA NA HAJJI


SWALI: Nini hukumu ya mwanamke alie hirimia umra kisha akavaa Niqaab na kufinika uso wake?

JAWABU: Mwanamke akihirimia ibada ya umra au hajji huwa haifai kufinika uso wake kwa kuvaa niqaab au kuvaa soksi za mikono,kama ilivyo kuja katika hadithi ya Mtume kuhusu Mwanamke alie hirimia

 

 

عن ابن عمر رضي الله عنهما أن رسول صلى الله عليه وسلم قال : " لاتنتقب المرأة المحرمة ولا تلبس القفازين " . رواه البخاري

 

Kutoka kwa Ibnu Umar radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kwamba Mtume amesema: [Asivae niqaabu  mwanamke alie kwenye ihramu na asivae soksi za mikono]    [imepokewa na Bukhari]
Lakini ikiwa atafunika uso wake kwa kutojua hukmu yake au kwa kusahau atakuwa hawajibiki na kitu chochote ,lakini kama alikuwa anajua basi atakuwa na khiyari kufanya moja katika mambo matatu,ima afunge siku tatu,au alishe masikini sita kila maskini nusu ya pishi,au achinje mbuzi na aigawe nyama yake kwa masikini wa mji wa makkah.

Na Mwenyezi Mungu ndie mjuzi zaidi.


 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575395
TodayToday102
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 10

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68297532af4102833445941747547442
title_68297532af4fa1145341371747547442
title_68297532af5db11216794871747547442

NISHATI ZA OFISI

title_68297532b0bd113682418491747547442
title_68297532b0cb75085649641747547442
title_68297532b0d9e20548923851747547442 Add content here

HUDUMA MPYA

: 5 + 9 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com