HAKI YA MUISLAMU JUU YA MUISLAMU MWENZAKE
Uislamu ni dini kubwa imeweka muongozo ambao kwamba inakusanya haki na uwajibikaji, miongoni mwa haki hizo ni haki ya Muislamu juu ya Muislamu mwenzake. Lengo kubwa ya haki hizi ni kuleta mapenzi na udugu wa kiislamu. Kila Muislamu akijua haki yake na ya mwenzake, basi itakuwa ni wepesi Waislamu kushikamana na kuwa kitu kimoja.
UHAKIKA WA UDUGU KATIKA DINI
Umma wa kiislamu leo umekuwa kama povu la bahari, umevunjika nguvu zake na kuwa wanyonge. Na ulimwengu hauna heshima isipokuwa watu wenye nguvu. Na sababu ya kudhoofika umma wa kiislamu ni kufarikiana kati yao. Na nguvu ni matunda ya umoja na mapenzi na haukudhoofika umma huu ila baada ya kukosa umoja nao ni udugu.
Uhakika wa udugu ni pale Mtume ﷺ alipounganisha maswahaba walipokuwa Makkah pamoja na kuhitalifiana rangi zao na maumbile yao na ndimi zao na malengo yao ya maisha. Amemuunga Hamza ambaye ni mkureishi na Salman ambaye ni mfursi na Bilal ambaye ni mhabasha na Suheib ambaye ni mrumi na wote wakawa wanaimba qaswida hii: Uislamu ndio baba yangu Wakijifakhiri kwa kabila la Qais au Tamim. Na wote walikuwa karibu na Neno lake Mwenyezi Mungu ﷻ:
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ} الحجرات:10}
[Kwa hakika Waislamu wote ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na Mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe]. [Al-Hujuraat:10]
Hii ndio daraja ya kwanza katika udugu wa kiislamu, kisha Mtume ﷺ akaunganisha watu wa Madina amabao ni kabila la Aus na Khazraj baada ya kupigana vita muda mrefu kati yao.
Kisha Mtume ﷺ akaunganisha watu wa Makka (waliogura) na watu wa Madina. Kulipatikana tukio ambalo halina mfano kwa mwanadamu. Amepokea Anas hadithi akisema:
[Alikuja AbdurRahman bin ‘Auf kwa Mtume ﷺ akamuunga na Sa’ad bin Rabiya na alikuwa na mali nyingi, akasema Sa’ad: nitakugawiya nusu ya mali yangu na nitakupatia mmoja kati ya wake zangu. Tazama anayekupendeza zaidi nimuache. Akasema AbdurRahman Mwenyezi Mungu akubariki, (nionyeshe soko)].
Kwa sasa hatuwezi kupata mfano wa Sa’ad!?. Mmoja wa watu wema alisema: Wako wapi wanaotoa mali yao usiku na mchana, siri na dhahiri akajibiwa: Wameenda pamoja na wasioomba watu wakafanya ung’ang’anizi.
Haki ya Muislamu juu Muislamu mwenzake ni kumpenda kwa ajili ya Mungu. Amepokea Anas Bin malik akisema ﷺ :
[Mambo matatu mtu akiwa nayo anapata imani; moja wapo ni kumpenda mtu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu].
MIONGONI MWA HAKI YA MUISLAMU JUU YA MUISLAMU MWENZAKE
Kutembeleana kwa lengo ya kujuana hali. Amepokea Abu Huraira hadithi kutoka kwa Mtume ﷺ akisema: [Mtu alimtembelea ndugu yake katika kijiji kingine Mwenyezi Mungu akamtuma Malaika kwa sura ya binadamu, akamuuliza waenda wapi? Akasema: naenda kumtembelea ndugu yangu. Akasema: Je ana neema unayotarajia (kutoka kwake)? Akasema: Hamna neema yoyote, isipokuwa nimempenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Akasema Malaika: Mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu nimetumwa kwako. Jua Mwenyezi Mungu anakupenda kama unavyompenda ndugu yako].
Kuitikia Salamu. Amepokea Abu Dawud akisema Mtume ﷺ :
لا تدخلون الجنة حتى تؤمنوا ولا تؤمنوا حتى تحابوا أولا أدلكم على شيء إذا فعلتموه تحاببتم أفشوا السلام بينكم] رواه مسلم]
[Mguu hautoingia peponi mpaka muamini, na hamtomuamini mpaka mpendane. Je Nikujulisheni jambo mkilifanya mtapendana? Toleaneni salamu kati yenu]. [Imepokewa na Muslim]
Kufuata janeza na kwenda mazikoni. Amepokea Abu Huraira hadithi kutoka kwa Mtume ﷺ akisema:
حَقُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ سِتٌّ قِيلَ مَا هُنَّ يَا رَسُولَ اللَّهِ : قَالَ إِذَا لَقِيتَهُ فَسَلِّمْ عَلَيْهِ وَإِذَا دَعَاكَ فَأَجِبْهُ وَإِذَا اسْتَنْصَحَكَ فَانْصَحْ لَهُ وَإِذَا عَطَسَ فَحَمِدَ اللَّهَ فَسَمِّتْهُ وَإِذَا مَرِضَ فَعُدْهُ وَإِذَا مَاتَ فَاتَّبِعْهُ رواه مسلم
[Haki ya Muislamu juu ya Muislamu mwenzake ni sita akalizwa ni zipi ewe Mtume wa Mungu ? akasema kumsalimu pindi ukikutana nae, kuitikia wito anapo kuita, kuchukua nasaha yake anapo kunasihi, akichemua na akamuhimidi Mwenyezi Mungu kumuambia Mwenyezi Mungu akurehemu, kumtembelea anapokuwa mgonjwa, kumzika anapokufa]. [Imepokewa na Muslim]
Kutokuwa na chuki. Anas amepokea hadithi kutoka kwa Mtume ﷺ:
لا تباغضوا ولا تحاسدوا ولا تدابروا ولا تقاطعوا وكونوا عباد الله إخواناً] رواه مسلم]
[Msichukiane, wala musihusudiane,musipeane migogo, wala Musikatane kueni ndugu katika waja wa Mwenyezi Mungu]. [Imepokewa na Muslim]
Hasadi ni maradhi hatari jee huridhiki kwa aliyegawanya riziki ambaye ni Mwenyezi Mungu. Inapaswa kumuomba Mwenyezi Mungu yeye ndiye mtoaji. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:
وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ } الحشر:10}
[Na waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu Tusamehe sisi na ndugu zetu waliotangulia katika Uisalmu]. [Al-Hashri:10]
Amepokea Anas akisema: Ilikuwa tumekaa pamoja na Mtume ﷺ makasema Mtume:
[Atakuja mtu wa peponi, akatokea mtu wa Answaar ndevu zake zilikuwa safi, na ameshika vitu vyake kwa mkono wa kushoto. Na siku ya pili Mtume akasema hivyo hivyo, na akatokea mtu yule yule hata siku ya tatu. Abdullah bin Amru akamfuata nyumbani kwake na akawa naye muda wa siku tatu, wala hakumuona akisimama usiku isipokuwa akishtuka usiku humtaja Mwenyezi Mungu katika kitanda chake mpaka ikifika swala ya alfajiri. Na alikuwa hamsikii isipokuwa akizungumza maneno ya kheri. Akamsimulia ‘Abdallah Bin ‘Amru sababu ya kumfuata kwa kuwa wewe ni mmoja kati ya watu wa peponi. Akasema: sina chuki na Muislamu yoyote].
Kumsaida Muislamu mwenzake akiwa na shida. Amesema Mtume ﷺ:
مَن نفَّس عن مؤمنٍ كربةً من كُرَب الدنيا، نفَّس الله عنه كربةً من كُرَب يوم القيامة، ومن يسَّر على معسرٍ، يسَّر الله عليه في الدنيا والآخرة، ومن ستر مسلمًا ستره الله في الدنيا والآخرة رواه مسلم
[Mwenye kumsaidia Muislamu kwa kumuondoshea shida. Menyezi Mungu atamsaidia kumuondoshea shida ya siku kiyama. Na mwenye kumfanyia wepesi mtu mwenye uzito. Mwenyezi Mungu Atamfanyia upesi duniani na kesho akhera. Na mwenye kumsitiri ndugu yake Muislamu duniani na kesho akhera, Mwenyezi Mungu Atamsitiri dunuani na kesho akhera]. [Imepokewa na Muslim]
Kumnusuru Muislamu sawa akiwa amedhulumu au amedhulumiwa. Amesema Mtume ﷺ:
انصر أخاك ظالماً أو مظلوماً، فقال: رجل يا رسول الله صلى الله عليه وسلم أنصره إذ كان مظلوماً، أفرأيت إذا كان ظالماً كيف أنصره؟! قال: تحجزه أو تمنعه من الظلم، فإن ذلك نصره رواه البخاري
[Mnusuru ndugu yako anayedhulumu au anayedhulumiwa. Akasema mtu: ewe Mtume wa Mungu tunamnusuru anayedhulumiwa, lakini vipi tunamnusuru anayedhulumu? Akasema Mtume: ni kumzuia anapodhulumu huko ndiko kumnusuru kwake]. [Imepokewa na Bukhari]
Kusitiri aibu ya Muislamu na kumuombea Mungu msamaha kwa kosa lake. Kwani Muisalmu si Malaika wala si nabii kwani yeye ni mwanadamu.
Wamesema wanavyuoni: Watu ni aina mbili:-
Watu wanaojulikana kwa wema na kuepukana na maasi, basi wakikukosea unapaswa kusitiri na kutofunua aibu yake.
Watu wanaofanya maasi kwa uwazi wala hawamuonei haya Mwenyezi Mungu, hao ni waovu.
Kwa hivyo linalo takikana kwa kila Muisalmu achunge haki ya Muislamu mwenzake ili jamii zetu ziishi katika mazingara bora na kuishi kama Mwenyezi Mungu alivyo taka tuishi kwa Upendo na Mahaba ili tupate radhi zake ALLAH ﷻ
SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH SWADI ALI
HISHIMA YA MWANAMKE KATIKA UISLAMU
Ndugu katika imani, suala la mwanamke ni suala ambalo liliwashughulisha watu wengi walio pita, na linaendelea kuwashughulisha wengi katika zama zetu hizi. Dini na mila mbalimbali zimezungumzia hali ya mwanamke katika jamii. Wasomi wa elimu na falsafa tafauti wamejaribu kuzungumzia cheo cha mwanamke katika jamii. Lakini kila kundi linajaribu kumzungumzia mwanamke kwa misingi ya kufikia malengo yao. Katika Makala haya tutajaribu kuangazia cheo cha mwanamke katika jamii mbalimbali. Tutaangalia hali ya mwanamke kabla ya kuja Uislamu, na hali yake katika Uislamu, na hali yake katika mataifa ya magharibi.
HALI YA MWANAMKE KABLA YA UISLAMU
Alikuwa mwanamke katika zama za ujinga akionekana kama bidhaa ambayo haina thamani. Kila mtu anaweza kumiliki bidhaa hiyo wakati wowote.
Wanaume wakioa wanawake bila ya idadi maulumu na kuacha bila ya idadi ya talaka. Mwanamke haruhusiwi kumiliki chochote, hana haki ya kurithi, anaweza kuolewa na zaidi ya mume mmoja. Mwanamke hakuwa na cheo katika jamii ya ujahiliyah, bali alikuwa akionekana ni mtu anayeleta aibu katika jamii. Ikafikia hali hiyo, baadhi ya wanaume kuwazika mabanati wao wakiwa wadogo kuogopea kuleta aibu katika jamii. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Anatueleza hali ya mwanamke Akisema:
وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِالْأُنثَىٰ ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ يَتَوَارَىٰ مِنَ الْقَوْمِ مِن سُوءِ مَا بُشِّرَ بِهِ ۚ أَيُمْسِكُهُ عَلَىٰ هُونٍ أَمْ يَدُسُّهُ فِي التُّرَابِ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ النحل:58
[Na mmoja katika wao anapopewa khabari ya kuzaliwa mtoto wa kike, unabadilika uso wake huwa mweusi na akajaa sikitiko. Anajificha na watu kwa sababu ya khabari mbaya ile alioambiwa. (anafanya shauri) Je, akae naye juu ya fedheha hiyo, au amfukie udongoni. Ni mbaya mno hukumu yao hiyo]. [Al-Nnahl:58]
Hii ndio hali halisi ya mwanamke kabla ya kuja Dini ya kislamu. Na hali hii ilikuwa sawa katika mataifa yote, sawa taifa la kiarabu na wasiokuwa waarabu.
HALI YA MWANAMKE KATIKA UISLAMU
Baada ya mwanamke kuishi katika dhulma kwa muda mrefu, bila ya kupata haki zake. Allah Subhaanahu wa Taala Alimtumiliza Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam kuja kumkomboa mwanamke na dhulma na udhalilifu alikuwa akipata kutoka katika jamii anayo ishi. Dini ya Kiislamu inamtukuza mwanamke na inampa haki zake zote katika jamii. Miongoni mwa haki hizo:-
Mwanamke sawa na mwanamume katika kutekeleza majukumu ya Dini. Amesema Allah Subhaanahu wa Taala:
مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ} النحل:97}
[Wafanyaji mema, wanaume au wanawake, hali ya kuwa ni Waislamu, tutawahuisha maisha mema, na tutawapa ujira wao mkubwa kabisa]. [Al-Nnahl:97]
Na Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala alimfadhilisha mwanamume kuliko mwanamke katika baadhi ya mambo, kwasababu ya majukumu mazito ya mwanamume katika kusimamia familia.
Mwanamke anastahiki kurithi. Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Amesema:
لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنْهُ أَوْ كَثُرَ ۚ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا} النساء:7}
[Wanaume wana sehemu katika mali wanayoacha wazazi wao na jamaa walio karibu. Na wanawake pia wanayo sehemu katika yale waliyaacha wazazi wao na jamaa walio karibu. Sawa yakiwa kidogo au mengi. Ni sehemu zilizofaridhishiwa (na Mwenyezi Mungu]. [Al-Nnisaa:7]
Mwanamke ana haki ya kuchagua mume wa kumwoa. Hawezi kuolewa bila ya ridhaa yake. Kinyume na zama za jahiliyah, mwanamke alikuwa ni bidhaa na chombo cha starehe kila mtu anakichukuwa kwa thamani ndogo, na kwa lengo la kutekeleza matamanio yake.
Mwanamke ana haki ya kujikomboa kutokana na mume dhalimu. Sheria ya kiislamu imempatia mwanamke haki ya kutoa talaka kwa mwanamume mwenye tabia mbaya, mwenye kumnyima mkewe haki zake.
Haya ni baadhi ya mambo muhimu mabao mwanamke amepewa katika Dini ya kiislamu. Na hii ndio hali halisi ya mwanamke katika Uislamu. Uislamu ulimrejeshea mwanamke hadhi na utukufu wake katika jamii, na ikatambua mchango wake mkubwa katika kuandaa kizazi cha kesho na kulea viongozi wa kusimamia Dini ya kislamu. Amesema Mtume ﷺ katika Hija:
اتقوا الله في النساء فإنهن عوان عندكم] رواه مسلم]
[Mcheni Mwenyezi Mungu katika kuwasimamia wanawake, kwa sababu wao ni wasaidizi wenu]. [Imepokewa na Muslim]
Mtume ﷺ anaweka wazi cheo cha mwanamke nacho ni wasaidizi wa wanaume, sio mtumwa au mtumishi kama wanavyomdai watu wengine kwamba uislamu umemfanya mwanamke kuwa ni mtumwa hana haki yoyote katika jamii.
SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH ABUU HAMZA
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.