ATHARI YA RAFIKI MWEMA
Mwanadamu hawezi kuishi peke yake ana haja ya usaidizi na kutangamana na watu wengine. Kwa ajili hiyo uislamu umekuja kuitikia mwito wa maumbile, uislamu ukaweka ibada ambazo zinafanywa na watu wengi kwa pamoja mfano wa Swala. Uislamu ni dini ya maumbile, ushahidi wa hayo ni Hadithi iliyopokewa na Abu Hureira:
“ Yoyote anayezaliwa huzaliwa katika uislamu isipokuwa wazazi wake humfanya mtoto wao kuwa myahudi au mnaswara au majusi”. Kama Mwenyezi Mungu alipomuumba Adam na Hawaa ili waishi pamoja wala hakumuacha peke yake amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
{هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا} {الأعراف:189}
"Yeye ndiye aliye kuumbeni katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili akae naye kwa utulivu." [Al-A'raaf:189]
Uislamu umetiliwa nguvu kutokana na sababu nyingi kama kuwekwa ibada za pamoja mfano wake swala ya ijumaa, swala ya jamaa na nyenginezo. Dhihirisho la haya alipoazimia Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)kuchoma nyumba za wasio kuja kuswali swala za jamaa.
Na dharura kwa uhai ni kuchagua mtu anayesuhubiana nae ili amkumbushe anaposahau na kumjuza anapokuwa mjinga, amesema mshairi wa kiarabu: “ Mja usimuulize bali muangalie rafiki yake kila rafiki kutokana na marafiki huongozana. Akiwa rafiki huyo ni muovu jiepusheni nae kwa haraka, na ikiwa ni mwema husuhubiana nae utaongoka”.
Uchaguzi wa rafiki mwema umejengwa kutokana na msingi wa kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na dini yake. Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
{إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ} المائدة:55
"Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea." [Al-Maaida:55]
Na katika matunda ya imani ni kuchagua rafiki mwema. Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
{لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ} { الحشر:22}
"Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao." [Al-Mujaadalah:22]
Na kemeo kubwa ni kuwapenda maadui wa Mwenyezi Mungu.na Mwenyezi Mungu amewasifu Maswahaba wa Bwana Mtume Sallallahu Alayhi Wassalam kuwa niwenye Kuhurumiana wao kwa wao na niwakali Kwa Makafiri wanao mpinga Mwenyezi Mungu.
Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
{مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ } {الفتح:29}
"Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao." [Al-Fathi:29]
Na akasema Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala)
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ
"Enyi mlio amini! Atakaye iacha miongoni mwenu Dini yake, basi Mwenyezi Mungu atakuja leta watu anao wapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri, wanapigania Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya anaye laumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu na Mwenye kujua." [Al-Maaidah:54]
Mwenye akili siku zote huwakimbia marafiki waovu kama mtu anavyo mkimbia Simba, kwa sababu siku ya Qiyama mtu atakuja juta kwa sababu ya kusuhubiana na Marafiki wabaya Wakati ambao Majuto hayafaa.
tazama Neno lake Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي ۗ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنسَانِ خَذُولًا
"Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema: Laiti ningeli shika njia pamoja na Mtume! Ee Ole wangu! Laiti nisingeli mfanya fulani kuwa rafiki! Amenipoteza, nikaacha Ukumbusho, baada ya kwisha nijia, na kweli Shet'ani ni khaini kwa mwanaadamu." [Al-Furqaan:27-29]
Dhalimu aliyekusudiwa katika Aya iliyotangulia ni ‘Uqbatu ibn Abi Mu’ayit na aliyempoteza katika uongofu Ummayah ibn Khalaf.
Amefananisha Mtume(Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)
[Rafiki mwema na rafiki muovu kama mfano wa anayebeba miski na mwenye kufua vyuma kwa anae beba miski ima atakuuzia ima utapata kutoka kwake harufu mzuri na mfua vyuma ima atachoma nguo zako au utapata harufu mbaya].
Je hauoni neno la Luqman juu ya mtoto wake: Ewe mwanangu tangamana na wanavyuoni hakika Mwenyezi Mungu hukuhuisha nyoyo kwa nuru ya hikima, kama anavyohuisha ardhi iliyokufa.”
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.