Menu

Sehemu ya Ibaada


FADHLA YA KUMSWALIA MTUME ﷺ


KUMSWALIA MTUME


Anasema Mwenyezi Mungu alietukuka katika kitabu chake kitukufu:

 

{إِنَّ اللَّهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا}

 


[Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu]     [Suratul Ahzab aya ya 56.]

Makusudio ya aya hii tukufu kwamba Mwenyezi Mungu alietukuka amewaeleza waja wake utukufu wa mja wake na Mtume Muhammad wake ﷺ kwake yeye huko mbinguni, yakwamba yeye Mwenyezi Mungu anamsifia Mtume kwa Malaika wake walio karibu nae, na yakwamba Malaika wanamswalia yeye Mtume, kisha Mwenyezi Mungu akawaamrisha waja wake walio Ardhini kumswalia na kumatakia salamu Mtume ili akusanye sifa kwao kwa watu wote walio mbinguni na walio Ardhini. kama alivyosema Ibn kathir (Allah amrehemu.)

Na makusudio ya kumswalia Mtume ni kumuombea dua kwa njia maalum na kulitukuza jambo lake Mtume  .

Wanasema wanazuoni: Swala ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume ni rehema yake na radhi zake, na kumsifia kwake kwa Malaika, na swala ya Malaika ni dua kwa Mtume na kumuombea msamaha, na swala ya Waislamu kwa Mtume ni dua kwake na kumuombea msamaha na kutukuza jambo lake.

Na fadhla ya kumswalia Mtume ni kubwa asema Mtume ﷺ:

 

أتاني جبريل فقال: يا محمد أما يرضيك أن ربك عز وجل يقول: إنه لا يصلي عليك من أمتك أحد صلاةً إلا صليت عليه بها عشراً، ولا يسلم عليك أحد من أمتك تسليمة إلا سلمت عليه عشراً؟ فقلت: بلى، أي ربي

 

[Alinijia Jibril akasema: Ewe Muhammad haikuridhishi wewe yakwamba mola wako alietukuka anasema: Hakika hakuswalii wewe yeyote katika umma wako swala moja isipokua namswalia yeye mara kumi , na hakutakii salamu yeyote katika umma wako salamu moja isipokua nitamtakia salamu mara kumi ? Nikasema : ndio mola wangu].

Hadithi hii ni sahihi ameipokea imam Ahmad na wengineo.

Anasema Swahaba: aliamka Mtume Muhammad siku moja nafsi yake ikiwa safi inaonekana katika uso wake furaha, wakasema ewe Mtume wa Mungu umeamka leo nafsi yako ikiwa safi na uso wako una furaha ? Akasema:

 

أجل، أتاني آت من ربي فقال: من صلى عليك من أمتك صلاة كتب الله له بها عشر حسنات، ومحا عنه عشر سيئات، ورفع له عشر درجات، ورد عليه مثلها      وراه أحمد

 

[Ndio amenijia mwenye kuja kutoka kwa mola wangu akasema : atakaekuswalia katika umma wako swala moja Mwenyezi Mugnu atamuandikia kwa swala ile thawabu kumi , na atamfutia madhambi kumi , na atamnyanyua daraja kumi na atmrudishia mfano wake]   

[Impokewa na Ahmad] 

Na hadithi hii ina njia nyingi ambazo zinaifanya hadithi hii iwe na nguvu.

Na imekuja katika baadhi ya mapokezi ya kwamba Mtume  alisujudu kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu alipoletewa wahyi kuhusu hilo:

 

وما من عبد يصلي عليَّ إلا صلت عليه الملائكة ما دام يصلي عليَّ فليقلَّ العبد من ذلك أو يكثر]     رواه الطبراني]

 

[Na hakuna mja atakaeniswalia mimi isipokua nae Malaika watamswalia maadamu ananiswalia basi mja afanye hilo kwa uchache au afanye kwa uwingi]    [Imepokewa na At Twabraniy] .

Na imepokelewa kutoka kwa  Ibnu Mas'uud radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume amesema :

 

إن لله تعالى ملائكة سياحين في الأرض يبلغوني من أمتي السلام]     رواه النسائي]

 

[Hakika Mwenyezi Mungu ana Malaika wanaotembea katika Ardhi wananifikishia mimi kutoka kwa umma wangu salamu]     [Imepokewa na Annasai]

Na imepokelewa kutoka kwa Ammar bin yasir radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume amesema:

 

إن لله تعالى ملك أعطاه سمع العباد فليس من أحد يصلي عليَّ إلا أبلغنيها، وإني سألت ربي أن لا يصلي عليَّ عبد صلاة إلا صلى عليه عشر أمثالها      رواه الطبراني

 

[Hakika Mwenyezi Mungu ana Malaika amempa maskizi ya waja basi hakuna yeyote atakaeniswalia mimi isipokua aninifikishia, na hakika yangu mimi nimemuomba mola wangu yakwamba haniswalii mimi mja Swala moja isipokua yeye atamswalia mara kumi mfano wake].    [Imepokewa na At Twabraniy]

Hivyo basi dua ya Mtume kwa ajili yetu imejibiwa, kwa hivyo kila anaemswalia Mtume Muhammad  Swala yake inamfikia Mtume wetu kupitia Malaika maalum,
Na nyongeza ya hilo Mwenyezi Mungu anamswalia mfano wake mara kumi asema Mtume ﷺ:

 

أكثروا الصلاة علي فإن الله وكل بي ملكاً عند قبري فإذا صلى علي رجل من أمتي قال لي ذلك الملك: يا محمد إن فلان ابن فلان صلى عليك الساعة     رواه الديلمي

 

[Fanyeni wingi kuniswalia mimi kwani Mwenyezi Mungu ameniwakilishia malaika kwenye kaburi langu basi akiniswalia mtu katika Umma wangu yule malaika huniambia: Ewe Muhammada hakika fulani mtoto wa fulani amekuswalia katika mda huu]    [Imepokewa na Ad Daylamiy na Hadithi Hasan] .

Na katika Hadithy nyingine Mtume ﷺ anasema:

 

ما من أحد يسلم عليَّ إلا رد الله عليَّ روحي حتى أرد عليه السلام]    رواه أبودود وهو حديث حسن]

 

[Hakuna yeyote atanisalimia mimi isipokua Mwenyezi Mungu ananirudishia roho yangu mpaka nimjibu salamu yake]     [Imepokelewa na Abu Daawud nayo ni hadithi mzuri.]

Na Amesema tena Mtume ﷺ:

 

حيثما كنتم فصلوا عليَّ فإن صلاتكم تبلغني]     رواه أبوداود]

 

[Popote mtakapokua niswalieni mimi kwa hakika swala zenu zinanifikia]     [Imepokewa na Abuu Dawud].

Mtume na ameondoka katika ulimwengu huu, na muumini anataka kiunganishi na Mtume wake  basi Mwenyezi Mungu akatufanyia njia hii ya moja kwa moja, basi tunapomswalia Mtume wetu anafikishiwa kwa jina yakwamba fulani amemswalia , kisha na yeye pia anatujibu salamu.


Makala haya yameandikwa na

Sheikh Muhammad Swaleh Al Munajid

Imefasiriwa na Mahamd Fadhil El Shiraziy



KUJILAZIMISHA NA SUNNAH


BN5I3BYCIAAaxET


Shukrani za dhati ni za Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Bwana wa viumbe vyote. Na rehma na amani zimfikie Mtume Muhammad. Swalla Llahu Alayhi wasallam.

Ni nani kati yetu ambaye hapendi apendwe na Mtume ?
Ni nani kati yetu ambaye hampendi Mtume?
Ni nani kati yetu ambaye hatarajii kuwa pamoja na Mtume ?
Ni nani kati yetu ambaye hatarajii maombezi ya Mtume ?
Jawabu ni kuwa hakuna mtu asiyetaka yote tuliyoyataja. Na njia ya pekee ya kutufikisha kumpenda yeye ni kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala). Na miongoni mwa alama za mapenzi ya kweli ya kumpenda Mtume ni kumtii na kufuata Sunna zake. Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala amesema:


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا     النساء:59

 

[Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.]  [Al-Nnisaa: 59]

Pia amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:


قُلْ أَطِيعُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ}   آل عمران:32}

 

[Sema: Mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na wakigeuka basi Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri.]      [Al-Imraan:32]
Katika aya nyingine Amesema tena Mola: Subhaanahu wa Taala:


مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا}   النساء:80}

 

[Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao]   [Al-Nnisaa:80]

Na ziko Aya nyingi zenye maana kama haya lakini tulizozitaja zinatosha.

Na Mtume , alituhimiza sana kumtii yeye katika hadithi nyingi sana. Miongoni mwa hadithi hizo; Mtume amesema:


أوصيكم بتقوى الله عز وجل، والسمع والطاعة، وإن تأمر عليكم عبدٌ؛ فإنه من يعش منكم فسيرى اختلافًا كثيرًا، فعليكم بسنتي وسنة الخلفاء الراشدين المهديين، عَضُّوا عليها بالنواجذ، وإياكم ومحدثات الأمور؛ فإن كل بدعةٍ ضلالةٌ رواه أبوداود والترمذي

 

[Nawausia uchaji Mwenyezi Mungu na kusikiliza na kutii na hata akiwa kiongozi wenu ni mtumwa. Na atakayeishi katika nyinyi ataona tofauti nyingi, basi shikamaneni na Sunna yangu na Sunna ya makhalifa wema waongofu, ishikeni kwa magego]     [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Tirmidhiy]

Pia Mtume tena:


كل أمتي يدخلون الجنة إلا من أبى، قيل يا رسول الله، ومن يأبى؟ قال: من أطاعني دخل الجنة، ومن عصاني فقد أبى]   رواه البخاري]

 

[Umma wote utaingia peponi isipokuwa atakayekataa kuingia peponi. Maswahaba wakamuuliza: Ni nani atakayekataa ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema Mtume Atakaye nitii mimi ataingia peponi na atakayeniasi basi atakuwa amekataa]   [Imepokewa na Bukhari]

Katika maneno ya maswahaba juu ya kushikamana na Sunna. Amesema Umar Ibn Khatwab Radhi za Allah ziwe juu yake alipokuwa akilibusu Hajar Aswad (jiwe jeusi):


[إنِّي لأَعْلَمُ أَنَّك حَجَرٌ , لا تَضُرُّ وَلا تَنْفَعُ , وَلَوْلا أَنِّي رَأَيْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يُقَبِّلُكَ مَا قَبَّلْتُكَ]

 

[Hakika mimi najua wewe ni jiwe hunufaishi wala hudhuru, na lau nisingelimuona Mtume akikubusu basi nisingelikubusu.]

Ndugu katika imani! Ningependa kuwatajia faida anazopata Muislamu endapo atashikamana na Sunna za Bwana Mtume Na miongoni mwa faida hizo ni kama zifuatavyo:

FAIDA YA KUSHIKAMANA NA SUNNAH

1. Kushikamana na Sunna ni kinga na hifadhi ya Waislamu wasifarikiane kwani ndiyo ambayo huleta mshikamano baina ya waumini na kuwa watu hawafarakani madamu watashikamana kwao na Sunna ya Bwana Mtume rehma na amani zimfikie.
2. Faida ya pili ya kushikamana na sunna ni kuokoka na kipote kipotofu kitakacho kwenda motoni. Amesema Mtume :
[Jua ya kwamba waliokuwa kabla yenu waliopewa kitabu waligawanyika mapote sabini na mbili, na umma huu utagawanyika vipote sabini na tatu, vipote sabini na mbili vitaenda motoni na kimoja pekee ndicho kitakachoenda peponi nacho ni kinachoshikamana na Sunna]
3. Faida nyengine ya kushikamana na Sunna ni kupata uongofu na kusalimika na upotofu. Amesema :
[Enyi watu, hakika mimi nimewaachia kitu mutakaposhikamana nacho hamtapotea milele: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna yangu.] Kwani kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Bwana Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam vinamuongoza aliyeshikamana navyo.
4. Miongoni mwa faida za kushikamana na sunna ni kwamba mtu atakaposhikamana na Sunna ataingia katika kundi la Mtume . Anahadithia Anas Ibn Malik Mwenyezi Mungu awe radhi naye, ya kwamba walikuja watu watatu katika nyumba za Mtume . Wakaulizia ibada ya Mtume . Wakaelezewa ibada yake basi waliiona kidogo sana. Wa kwanza akasema: Mimi nitaswali usiku kucha milele wala sitolala. Wa pili akasema : Mimi nitafunga siku zote na wala sitokula hata siku moja. Wa tatu akasema: Mimi nitajiepusha na wanawake milele sitaoa. Alipokuja Mtumeakaelezewa kuhusu maswahaba wale akawaambia:

 

أنتم الذين قلتم كذا وكذا؟ أما والله إني لأخشاكم لله وأتقاكم له، لكني أصوم وأفطر، وأصلي وأرقد، وأتزوج النساء، فمن رغب عن سنتي فليس مني

 

[Nyinyi ndio mliosema hivi na hivi na hivi? Ama mimi naapa kwa Mwenyezi Mungu ya kwamba mimi ni mchaji Mwenyezi Mungu zaidi pamoja na hivyo, mimi naswali usiku nalala nafunga na siku nyingine nala na vile vile naoa wanawake. Basi anayejiepusha na mwenendo wangu si katika mimi].  [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

HUKMU YA KUIWACHA SUNNAH

Na kujiepusha na Sunna ya Mtume inaweza kuwa maasi au ni ukafiri, tunamuomba Mwenyezi Mungu atulinde na ukafiri. Mtu atakapoacha Sunna kwa kuipuuza na kuipinga na kuikosoa atakuwa ameikosoa Dini na kuikosoa Dini ni katika sampuli za ukafiri.Tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala na ukafiri.
Na endapo mtu ataacha Sunna kwa uvivu, sio kwa njia ya kuikosoa basi ni kulingamana na Sunna yenyewe, ikiwa ni jambo la wajibu, atapata dhambi kwa kuacha wajibu na akiacha lililopendekezwa atakuwa amepitwa na fadhila kubwa kabisa.

Kwa hivyo ni juu yetu kushikamana na Sunna za Bwana Mtume ili tupate radhizake Mwenyezi mugnu Mtukufu.


 SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH ALI BAHERO




KUTAHADHARI NA UZUSHI KATIKA DINI


 UZUSHI


Shukrani za dhati ni za Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Aliyesema:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا}     المائدة :3}

[Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. ]   [Al-Maaida:3]

Na rehma na amani zimfikie Mtume wetu aliyesema:


من أحدث في أمرنا هذا ما ليس منه فهو رد ]       رواه البخاري ومسلم]

 

[Atakayezusha katika jambo letu hili (Dini) ambalo si katika dini atarudishiwa mwenyewe].   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Tumcheni Mwenyezi Mungu Ambaye amemtumiliza Mtume Muhammad pale walipokuwa watu wako katika upotofu wa ushirikina na kufuata dini ya baba zao potofu. Akawatoa katika ushirikina na kuwaleta katika Uislamu (Dini ya haki). Kwa Kweli, Mtume alisubiri mengi maovu aliyotendewa na waovu mpaka Dini ikakamilika.Pia aliweza kuwatahadharisha watu na kufuata hawaa zao na kuzusha katika Dini ya Mwenyezi Mungu baada ya kuondoka yeye.
Kwa kweli uzushi katika dini ulianza punde tu baada ya kuondoka Mtume , kwani vipote vingi vilizuka kwa sababu ya watu kuacha Sunna ya Bwana Mtume na kufanya mambo bila ya elimu na kufuata matamanio ya nafsi. Na mfano wa vikundi hivyo ni Muutazila, Masufi, Khawaarij, Murjia na vikundi vyengine. Kuna ushahidi mwingi wa kushikamana na sunna na kujiepusha na bidaa. Mola Subhaanahu wa Taala Amesema:

 

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ}   آل عمران: 31}

 

[Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu.]   [Al-Imraan:31]
Pia Mwenyezi Mungu amesema:

 

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۖ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ}      الحشر:7}

 

[Atakachowapeni Mtume kichukueni na atakachowakataza jiepusheni nacho]   [Al-Hashri:7]

Mtumeamesema:


من أحدث في أمرنا هذا ما ليس منه فهو رد ]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Atakayezusha katika Dini yetu hii jambo ambalo halimo katika Dini basi atarudishiwa mwenyewe].    [Imepokewa na Bukhari na Muslim ]

Vile vile Mtume Asema katika hadithi yake:

 

فمن رغب عن سنتي فليس مني]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Anayejiepusha na sunna yangu si katika mimi].   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na katika hadithi nyingine Mtume anasema:

أخرج ابن ماجه عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَبَى اللَّهُ أَنْ يَقْبَلَ عَمَلَ صَاحِبِ بِدْعَةٍ حَتَّى يَدَعَ بِدْعَته. ضعفه الألباني

Amepokea Ibnu Maajah kutoka kwa Ibnu Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema : Amesema Mtume rehma na Amani zimfikie yeye [Anakataa Mwenyezi Mungu kukubali amali ya mtu mzushi mpaka ache uzushi]. Lakini sheikh Al-Albaniy ameidhofisha Hadithi hii

Na amesema Mtume rehma na amani zimfikie yeye:

 

وإياكم ومحدثات الأمور، فإن كل محدثة بدعة وإن كل بدعة ضلالة]    رواه أبوداود]

 

[Jiepusheni na kuzusha mambo (katika dini) kwani kila uzushi ni upotofu]. [Imepokewa na Abuu Daud]

Inatakiwa waumini washikamane na Sunna na wajiepusha na uzushi katika Dini. Kwani ndiko kumkubali kikamilifu Bwana Mtume , na pia kumtii yeye. Wala haifai kwa Muislamu kwenda kinyume na Sunna ya Mtume . Ametahadharisha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) hilo aliposema:

 

فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ}    النور:63}

 

[Na wajitadhari wanaokhalifu amri ya Mtume wasije wakapata fitna au adhabu kali ]   [Al-Nnuur:63]

Vilevile, Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Anasema:

 

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا الأحزاب:36

 

[Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.]  [Al-Ahzaab: 36]

Aya hizi zanaonesha kwamba yoyote atakayemuasi Mola na Mtume atakuwa katika upotevu na kupata adhabu kali ya Mwenyezi Mungu
Ndugu Muislamu kwenda kinyume na Sunna ya Mtume ni sababu ya kufarakana Waislamu katika Dini na kupotoka upotevu ulio wazi, Amesema Mola Subhaanahu wa Taala:

 

وَهَٰذَا صِرَاطُ رَبِّكَ مُسْتَقِيمًا ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ}   الأنعام:126}

 

[Na hii ndiyo Njia ya Mola wako Mlezi Iliyo nyooka. Tumezipambanua Aya kwa watu wanao kumbuka.]   [Al-An'aam:126]

Vilevile, kukhalifu Sunna ni sababu ya mtu kufuata matamanio ya nafsi. Na Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Ametutahadharisha kufuata matamanio kwa kusema:

أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَٰهَهُ هَوَاهُ }    الجاثية:23}

 

[Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake,]    [Al-Jaathiyah:23]

Na wanaofuata matamanio ni wale ambao Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala) Aliwataja kwa kusema:

 

أُولَٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ}     محمد:16}

[Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao, na wakafuata pumbao lao.]   [Muhammad:16]
Uzushi katika Dini, Mtume ameuita kuwa ni upotofu kwa sababu mzushi amepotea kwa kufuata matamanio. Tusisahau Mtume alikuwa akijilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na tabia mbaya, na kufuata matamanio ya moyo. Enyi waja wa Mwenyezi Mungu ! Haifai kwa mtu yeyote kuleta maoni yaliyo kinyume na Sunna ya Bwana Mtume . Amesema ‘Abdillahi Ibn ‘Abbas: (R.A.) “ Atakayeleta maoni ambayo hayapo katika kitabu cha Mwenyezi Mungu wala hadithi za Mtume kwani hajui yatakayompata yeye atakapo kutana na Mwenyezi Mungu
Jueni kuwa mzushi ni dhalili na pia ana hasira za Mwenyezi Mungu aliyetukuka. Amesema Imam Shatwiby, Mwenyezi Mungu amrehemu: “Hakika mzushi atavishwa udhalili duniani na hasira za Mwenyezi Mungu”. Na hii ni kwa neno la Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Aliposema:

 

إِنَّ الَّذِينَ اتَّخَذُوا الْعِجْلَ سَيَنَالُهُمْ غَضَبٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَذِلَّةٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُفْتَرِينَ}   الأعراف:152 }

 

[Hakika wale walio muabudu ndama, itawapata ghadhabu ya Mola wao Mlezi na madhila katika maisha ya dunia. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wazushi.]   [Al-A'raaf:152]

Adhabu hii itakuwa pia kwa wale wanaofanana nao kitabia kwani uzushi ni kumsingizia Mwenyezi Mungu. Asema Imam Malik Mwenyezi Mungu amrehemu: 

 

من ابتدع في الاسلام بدعه يراها حسنه فقد زعم ان محمدا ( صلى الله عليه وسلم ) خان الرسالة لان الله يقول ( اليوم أكملت لكم دينكم ) فما لم يكن يومئذ دينا فلا يكون اليوم دينا

 

"Atakayezusha katika Uislamu uzushi, akauona uzushi huo ni mzuri basi amedai ya kwamba Mtume Muhammad amefanya khiana katika ujumbe, kwani Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Amesema: “ Leo nimewakamilishia Dini yenu”. Kwa hivyo, lile ambalo halikuwa siku hiyo Dini basi leo haliwi dini’.
Na ameweka bayana Mtume kama ilivyo katika sahihi Muslim kwamba wazushi watasogea katika birika la Mtume na watafukuzwa kwa sababu ya uzushi wao unamaliza Dini sahihi ya Mwenyezi Mungu.


SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH ALI BAHERO




KUJIANDAA NA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI


vipi tupoke ramadhan


Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Ametuwekea misimu mbali mbali na kwa minaajili ya kuipatiliza misimu hiyo kwa kurudi kwa Mwenyezi Mungu kwa kukufanya ibada, miongoni mwa misimu hiyo ni mwezi wa Ramadhani.

Mwenyezi Mungu mtakatifu ametuambia:

 

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

 

[Mwezi wa Ramadhani ambao umeteremshwa Qur’an ndani yake ambayo ni ubainifu na uongofu kwa watu na upambanuzi. Mwenye kuushuhudia Mwezi wa Ramadhani miongoni mwenu na afunge na atakayekuwa mgonjwa ama akawa safarini (na akala katika mwezi wa Ramadhani) basi ni juu yake kufunga katika siku nyengine, Mwenyezi Mungu awatakia wepesi na wala hawatakii uzito na ili mukamilishe hesabu ya masiku na mumtukuze Mweyezi Mungu, hakika mukifanya hivyo mutakuwa ni wenye shukrani]  [Al-Baqara:185]
Ndugu Muislamu mwezi mtukufu wa Ramadhani umetukabili inatupasa tuupokee kwa kumcha Mwenyezi Mungu na kufanya twaa na ibada kwa wingi na kukaa mbali na maovu kama tunavyo jua ya kuwa malipo ya amali njema huongezeka na vile vile malipo ya amali mbaya. Na mwezi huu mtukufu mwanzo ni kumi la rehma na kumi la maghfira na mwisho ni kuachwa huru na moto. Kufunga mchana ni wajibu na kusimama kwa ibada usiku ni sunna yenye kukamilisha faradhi. Ukifunga kwa imani na kutarajia malipo utasamehewa madhambi yaliyotanguliia. Ukifanya ‘umra ni kama uliye hijji. Milango ya pepo hufunguliwa na ya moto hufungwa. Na saumu ni ibada ya pekee ambayo Mola amejihusishia mwenyewe kama alivyosema Mtume katika hadithi ya Bukhari aliyoipokea kutoka kwa Abu Huraira kuwa Mwenyezi Mungu amesema
[Amali zote za binaadamu ni zake ila saumu. Hakika ya saumu ni yangu na ni Mimi ndiye nitakaye ilipa na saumu ni kinga, ikiwa ni siku ya mmoja wenu kufunga basi asifanye machafu, wala asiseme maovu, basi atakapo tukanwa na yoyote au akataka kupigana naye basi amwambie mimi nimefunga. Naapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mikononi mwake harufu ya kinywa cha mmoja wenu ni nzuri zaidi kuliko harufu ya miski, na mwenye kufunga ana furaha mbili, moja huipata akifungua saumu, na ya pili ni wakati akikutana na Mola wake].

 

WAKATI WA KUFUNGA MWEZI WA RAMADHANI

Fungeni kwa kuuona mwezi na fungueni kwa kuuona mwezi, kwani Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam amekataza kutangulia kufunga Ramadhani kwa siku moja ama mbili ila ikiwa mtu ana ada ya funga yake kama vile jumatatu na Alkhamisi, na haifai kufunga siku ya shaka, Amesema Ammar bin Yaasir “Mwenye kufunga siku ya shaka basi amemuasi Abal Qaasim, yaani Mtume .
Na amepokea Bukhari kutoka kwa Ibnu ‘Umar ya kuwa Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam amesema katika maana ya Aya: [Msifunge mpaka muuone mwezi wala msifunguwe mpaka muuone mwezi, na iwapo mtafinikwa na mawingu kamilisheni hesabu ya thalathini].
Na atakaye uona mwezi kwa yaqini na amjulishe kiongozi aliyewakilishwa wala asifiche.
Na utakapotangazwa mwezi katika vyombo vya habari, kuingia kwa Ramadhani fungeni na kutoka kwa Ramadhani fungueni, kwani kutangaza kwa kiongozi aliyewakilishwa ndio hukumu.
Kufunga Mwezi wa Ramadhani ni nguzo moja katika uislamu na mwenye kupinga huwa kafiri.
Kufunga ni nguzo iliothibiti katika Qur-ani na mwenye kupinga huwa amemkanusha Mungu na Mtume na maelewano ya Waislamu wote Allah atwambia:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}     البقرة:183}

[Enyi mlio amini mmefaradhiwa swaumu kama walivyofaradhiwa waliotangulia ili mupate kumcha Mungu]    [Al-Baqara:183]
Na saumu ni wajibu kwa kila muislamu alio baleghe na akawa na akili na uwezo wa kufunga, na mwanamke asiyekuwa na hedhi. Kafiri si wajibu kufunga, lakini ataulizwa siku ya kiyama na akisilimu halazimishwi kulipa zilizopita ila akisilimu katikati ya huo mchana wa Ramadhani atalazimika akamilishe siku na mtoto mdogo si wajibu kufunga mpaka abaleghe lakini yafaa tuwafundishe kufunga kama walivyokuwa masahaba. Na kubaleghe kwa mtoto hujulikana kwa moja katika mambo matatu: Jambo la kwanza; ni kufikia miaka kumi na mitano. Jambo la pili; ni kutokwa na manii kwa kuota, ama jambo jingine. Jambo la tatu; ni kutokwa na nywele za kinena. Na mtoto wa kike huzidisha Jambo la nne nalo nikupatwa na hedhi. Mtoto akipatwa na mambo haya tuliyoyataja, humlazimu faradhi zote za Mwenyezi Mungu ikiwa ana akili.
Na mwendawazimu si wajibu kufunga wala faradhi yoyote nyingine. Na wala mwenye kushindwa kufunga kwa sababu ya utu zima ama ugonjwa ambao hautarajiwi kupona, itakuwa si lazima kufunga lakini atalisha maskini kila siku alioacha atalisha maskini mmoja, kila maskini robo ya pishi kwa pishi za Mtume na ni bora kumuongezea kitoweo.

 

HUKMU YA WENYE UDHURU

Mgonjwa anayetarajiwa kupona, ikiwa saumu haimsumbui wala kumdhuru, haifai kula kama mtu huyo hana udhuru wowote. Na ikwa saumu inamsumbua lakini haimdhuru na inafaa afungue na ni karaha kufunga na ikiwa saumu itamdhuru ni haramu kufunga na popote atakapopoa itamlazimu ailipe saumu na akifa kabla ya kupona hana madhambi.
Na mwanamke mwenye mimba akiwa ni dhaifu ama mimba itamletea uzito akashindwa kufunga mwanamke huyo anaruhusiwa asifunge lakini akihisi ya kuwa na uwezo wa kufunga, atafunga hata ikiwa ni kabla ya kujifungua na itakapokuwa haiwezekani atasubiri baada ya kujifungua na kutwahirika na nifasi. Na mwanamke mwenye kunyonyesha akiogopea kupunguka maziwa atakula kisha atalipa.
Na msafiri akikusudia kukimbia saumu haifai ni lazima afunge. Na ikiwa hakukusudia kukimbia kufunga basi ana hiari ya kufunga na kutofunga. Na ikiwa kufunga na kutofunga ni sawa basi ni bora afunge.
Na ikiwa safari itamsumbua ni karaha kufunga iwapo mashaka yatazidi na ni haramu kufunga. Kwani Mtumealitoka kwenda Makka mwaka wa fat-hi na huku amefunga akaambiwa kuna watu wameshindwa kufunga na wanakusubiri wewe utakavyofanya. Mtume akaitisha maji akanywa na watu wanamwangalia kisha na watu wakanywa, kisha akaambiwa kuna watu hawakufungua akasema Mtume : [Hayo ni maasi].

HUKUMU YA ANAE FANYA KAZI YA DREVA

Na safari ni ya aina yoyote ile, kama madereva wa malori wakati wowote wanapoacha miji yao wanaruhusiwa kufungua kama vile wanavyoruhusiwa kupunguza swala za rakaa nne na kuzikusanya swala mbili mbili ikiwa mtu amesafiri katikati ya mchana ni vizuri akamilishe saumu ya siku ile ya kwanza ya safari.
Na haifai kufunga kwa mwenye hedhi na nifasi na wala haiswihi. Wakati wakitwahirika na hedhi ni lazima wafunge hata kama hawajaoga kisha watalipa siku walizokula.

KUHIMIZA KUSIMAMA USIKU WA RAMADHANI

Ndugu Muislamu Mtume amehimiza kusimama kufanya ibada katika masiku ya Ramadhanii. Na mtu akiendelea na imamu kuswali mpaka akamaliza huandikiwa thawabu za mtu aliyesimama usiku kucha.
Na ni juu ya maimamu kumcha Mwenyezi Mungu katika kuswalisha tarawehe. Inafaa awachunge wanaomfuata asiwaendeshe mbio bila ya utulivu katika kusimama, kurukuu na kusujudu. Kwani Mwenyezi Mungu Amesema Subhaanahu wa Taala:



[لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا } [هود:7}

 

[Ili akufanyieni mtihani ajuulikane ni nani miongoni mwenu mzuri zaidi wa vitendo.] [Huud:7]
Na Mtume alikuwa ni mwenye kupenda kheri zaidi na ni kielelezo chema lakini hakuzidisha zaidi ya rakaa kumi na moja sio katika Ramadhanii wala masiku mengine. Na Mtume ﷺ aliswali na jamaa katika Ramadhani kisha akaacha kwa kuogopea isifaradhishwe.
Na iliyo swahihi kutoka kwa Amirul muuminiina ‘Umar ibnul Khatwb ni kuwa alimuamrisha ‘Ubai ibn Ka’ab na Tamimi Daar waswalishe watu kwa rakaa kumi na moja na hii ndio idadi aliodumu nayo Mtume na akafuata khalifa muongofu ‘Umar Ibnul khatwab ndio bora zaidi, na ikiwa mtu atazidisha kwa mapenzi yake sio kufuata sunna hapingwi lakini asifanye haraka kama wanavyofanya maimamu wengi waleo

Mungu atuafikie kupaliza nyakati za twaa na atuhifadhi na maovu na atuongoze njia iliyonyooka na atuepushe na njia ya motoni na atufanye wenye kufunga Ramadhani na wenye kusimama usiku kwa ibada kwa imani na kutarajia malipo na thawabu za Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyyezi Mungu ni Mpaji na ni Mkarimu.
Namaliza maneno yangu kwa kumuomba Mwenyezi Mungu msamaha na kuwaombea Waislamu wote msamaha kutokana na madhambi yote.

FAIDA ZA KUFUNGA

Miongoni mwa faida ni kuivunja nafsi, kwani shibe ya maji na chakula na kuvaana na wanawake inapelekea kughafilika.
Faida nyingine ni moyo kukaa faragha kwa kumfikiria Mwenyezi Mungu na kuleta dhikri, kwani tumbo likiwa tupu husababisha moyo kunawirika.
Na faida nyingine ni kwa mtu tajiri hujua neema ya Mola juu yake. Kwa sababu ya kujinyima kwa muda fulani na hupelekea kumkumbuka ndugu yake aliyenyimwa neema ile moja kwa moja humsikitikia mwenzake maskini.
Na saumu hufanya mapitio ya damu kuwa membamba ambayo ndio mapitio ya shetani, kwani shetani anatembea katika mwili kama inavyotembea damu basi Mtume amesema “Fungeni mapito ya shetani kwa njaa.”
Saumu ya Mja haiwezi kutimia ila akiepuka yaliyo haramishwa katika hali zote.
Kwani Mtume Amesema: 

 

[من لم يدع قول الزور والعمل به فليس لله حاجة في إن يدع طعامه وشرابه]

 

[Ambaye haachi maneno ya uongo na kutumia uongo, Mwenyezi Mungu hana haja aache chakula chake na kinywaji chake]. Na watu wema ilikuwa wakifunga hukaa Msikitini ili kuepukana na kusengenya.


Sikiliza Mada hii na Sheikh Yusuf Abdi




SIKU YA IJUMAA NA HUKMU ZAKE


jomo3a


Hakika Mwenyezi Mungu huumba atakavyo na huchagua atakavyo. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:

 

وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ ۗ مَا كَانَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ ۚ سُبْحَانَ اللَّهِ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ} القصص: ٦٨}

 

[Na Mola wako Mlezi huumba na huteuwa atakavyo. Viumbe hawana khiari.] [Al-Qaswas: 68]
Na Mwenyezi Mungu ndie anaye jua hekima kwa kila kitu anacho kichagua miongoni mwa viumbe vyake. Mwenyezi Mungu huchagua Mitume miongoni mwa Malaika na watu. Na Mwenyezi Mungu  ameufadhilsha Mji wa Makka kushinda sehemu nyingine. Na akauchagua Mji wa Madina kuwa ni mji aliohamia Mtume na Masahaba. Kisha akauchagua Baytul Maqdis akajalia ni sehemu ya Mitume wengi ambayo Mwenyezi Mungu ﷻ ametuelezea habari zao katika Qur’an Tukufu.

Na Mwenyezi Mungu amefadhilisha baadhi ya Miezi kuliko mingine na Usiku na Mchana. Akachagua Miezi mine Mitukufu (Dhul-qa’ada, Dhul-hijja, Muharam na Rajab). Na bora wa masiku ni siku ya Ijumaa.

HUKMU YA SWALA YA IJUMAA

Swala ya Ijumaa ni miongoni mwa swala muhimu za faradhi. Na ni wajib kwa kila Muislamu mwanamume ,mwenye akili timamu, alie baleghe ambae hana nyudhuru za kisheria za kumzuia kuetekeleza ibada hiyo.
Na sharia imetia mkazo zaidi na kusisitiza kutekelezwa swala ya ijumaa kwa jamaa. Na malipo yake ni makubwa zaidi.

FADHLA ZA SIKU YA IJUMAA

1. Kupata Thawabu na Malipo kwa kila hatua ya kwenda Msikitini sawa na Mtu aliyesimama kuswali na kufunga Mwaka mzima. Amesema Mtume ﷺ:

 

مَنْ اغْتَسَلَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ وَغَسَّلَ وَبَكَّرَ وَابْتَكَرَ وَدَنَا وَاسْتَمَعَ وَأَنْصَتَ كَانَ لَهُ بِكُلِّ خُطْوَةٍ يَخْطُوهَا أَجْرُ سَنَةٍ صِيَامُهَا وَقِيَامُهَا] رواه الترمذي وأحمد]

[Mwenye kuoga na kujisafisha, kisha akaenda Msikitini na mapema na akamkurubia Khatibu na akasikiliza kwa utulivu. Mwenyezi Mungu atamlipa kwa kila hatua malipo sawa na Mtu aliyesimama kuswali na kufunga Mwaka mzima] [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Ahmed].
2. Kusamehewa Madhambi yake ya wiki mzima pamoja na siku tatu za ziada. Amesema Mtume ﷺ:

 

مَنْ تَوَضَّأَ فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ ثُمَّ أَتَى الْجُمُعَةَ فَاسْتَمَعَ وَأَنْصَتَ غُفِرَ لَهُ مَا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْجُمُعَةِ وَزِيَادَةُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ]   رواه مسلم]

 

[Mwenye kutawadha vizuri, kisha akaja Msikitini na akamsikiliza Khatibu na kunyamaza. Anasemehewa Madhambi yake ya wiki mzima pamoja na siku tatu]. [Imepokewa na Muslim.]
3. Kukubaliwa dua katika siku hii tukufu. Amesema:


فِي الْجُمُعَةِ سَاعَةٌ لَا يُوَافِقُهَا عَبْدٌ مُسْلِمٌ قَائِمٌ يُصَلِّي فَسَأَلَ اللَّهَ خَيْرًا إِلَّا أَعْطَاهُ]   رواه مسلم] 

 

[Hakika katika Siku ya Ijumaa kuna wakati, haafikiwi Muislamu na wakati huo hali akiwa anamuomba Allah Kheri, ila Mwenyezi Mungi humpatia]. [Imepokewa na Muslim]

ADABU NA SUNNA ZA SIKU YA IJUMAA 

1.Kuoga na kujisafisha na kupaka manukato mazuri pamoja na kuondosha harufu mbaya mwilini.. Amesema Mtume  ﷺ:

 

مَنْ اغْتَسَلَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ غُسْلَ الْجَنَابَةِ ثُمَّ رَاحَ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَدَنَةً]  رواه البخاري ومسلم]

 

[Mwenye kuoga siku ya Ijumaa, Josho la Janaba kisha akaenda Msikitini (na mapema.) Mfano wake ni kama mtu aliyetowa sadaka ya Ngamia]  [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

2. Kwenda Msikitini mapema na kumkurubia khatibu. Amesema Mtume ﷺ:

 

احْضُرُوا الذِّكْرَ ، وَادْنُوا مِنَ الْإِمَامِ ] رواه أبوداود]

 

[Nedeni mkasali sala ya Ijumaa, na mkae karibu na khatibu]. [Imepokewa na Abuu Daud]

3. Kujishughulisha kwa Kumtaja Allah, kusoma Qur’an, kuomba msamaha, kuomba dua kwa wingi na kumsalia Mtume Muhammad .

4. Kumsilikiza Khatibu kwa utulivu, bila ya kujishughulisha na mambo mengine. Asema Mtume ﷺ:

 

مَنْ تَوَضَّأَ فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ ثُمَّ أَتَى الْجُمُعَةَ فَاسْتَمَعَ وَأَنْصَتَ غُفِرَ لَهُ مَا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْجُمُعَةِ وَزِيَادَةُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ] رواه مسلم]

 

[Mwenye kutawadha vizuri, kisha akaja Msikitini na akamsikiliza Khatibu na kunyamaza. Anasemehewa Madhambi yake ya wiki mzima pamoja na siku tatu]. [Imepokewa na Muslim.]

 

MAMBO YALIO KATAZWA KATIKA SWALA YA IJUMAA

1. Kuja Msikitini kuchelewa na kukata safu kwa kuruka watu, kwa lengo la kutaka kukaa safu ya mbele. Siku moja Mtume alimuona mtu akikata safu na kuruka watu; Akamuambia:

 

اجلس فقد آذيت وآنيت]  رواه إبن ماجة]

 

[Kaa chini kwa hakika umewaudhi watu na umechelewa.] [Imepokewa na Ibnu Maajah]

2. Kuwashawishi waja wa Mwenyezi Mungu, kwa kusoma Qur’an kwa sauti kubwa, au kufanya Dhikri kwa sauti ya juu. Mtume aliwakataza Masahaba kusoma kwa sauti ya juu, na akawambia; Asisome mmoja wenu Qura’n kwa sauti ya juu kuliko mwingine.

3. Kuzungumza wakati wa Khatibu anatoa khutbah ya Ijumaa. Amesema Mtume ﷺ:

 

من قال لصاحبه يوم الجمعة والإمام يخطب أنصت فقد لغا]  رواه النسائي]

 

[Ukimuambia mwenzako nyamaza na Khatibu akiwa anazungumza, amefanya upuzi]. [Imepokewa na Al-Nnasaai]

KHATARI YA KUACHA SWALA YA UJUMAA

Mtume MuhammadAmesisitiza na kutilia mkazo juu la suala la kutekeleza swala ya Ijumaa. Na akawatahadharisha Waislamu wanaoacha kutekeleza swala hii. Adhabu kubwa watakayo pata watu hao hapa duniani ni nyoyo zao kuwa ngumu na kupigwa muhuri wa kughafilika. Amesema Mtume :

 

لينتهين أقوام عن ودعهم الجمعات، أو ليختمن الله على قلوبهم، ثم ليكونن من الغافلين]   رواه مسلم وأحمد والنسائي]

 

[Hawataendelea watu kuacha swala ya Ijumaa, mpaka Mwenyezi Mungu apige muhuri nyoyo zao, kisha watakuwa niwenye kuishi katika mughafala]. [Imepokewa na Muslim na Ahmad na Al-Nnasaai]
Ndugu Muislamu, tujihadhari sana na kuacha swala ya Ijumaa, kwasababu adhabu yake ni nzito sana. Moyo ukiwa mgumu, basi mwanadamu anakuwa sawa na myama, hajali lolote wala chochote. Utamuona hamuogopi Mwenyezi Mungu, kwa kufanya maasi usiku na mchana.
Tunamuomba Allah Subhaanahu wa Taala athibitishe nyoyo zetu juu ya twaa yake, na atulinde na machafu yote.


     KWA FAIDA SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH HASSAN SUGO



LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6574500
TodayToday2567
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 39

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6828ed58bb73210419530221747512664
title_6828ed58bb8e710230409911747512664
title_6828ed58bba5515547899941747512664

NISHATI ZA OFISI

title_6828ed58bd406379813301747512664
title_6828ed58bd4db17892064961747512664
title_6828ed58bd5bd7581151031747512664 Add content here

HUDUMA MPYA

: 15 + 3 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com