BAADA YA KUFA
Nini kufa? Kufa ni kuepukana roho na kiwiliwili, au kufa ni kukatika matumizi ya roho kwa kiwiliwili na kukosa kiwiliwili ala yake na kumuepusha mtu na amali yake na watoto wake na mke wake. Kufa inakata utamu wa maisha ya kilimwengu na kwenda ulimwengu mwengine. Mtu ambae alikuwa akifurahia maisha ya ulimwengu amepata khasara baada ya kufa. Na yule ambae alikuwa akifurahi kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu basi atapata neema kubwa na ina kamilika kufaulu kwake.
Watu wengi hudhania ya kwamba Mtu anapo kufa na akazikwa amemaliza kila kitu na amepumzika na ulimwengu, wala halimjii yeye jambo lolote. Kudhania hivyo ni kosa kubwa bali hakika Mwanadamu baada ya kufa kwake anaingia katika maisha mapya, maisha ya barzakh na kutoka maisha ya barzakh huenda kwenye maisha ya Akhera ambayo ndiyo maisha ya mwisho na ya milele.
Njooni tuangalieni kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam zina semaje kujibu suala; Ni nini baada ya kufa ?
Hakika Qu’rani imebainisha wazi na Hadithi za Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam yatakayo tokea baada ya kufa. Wakati anapokufa Mwanadamu na akazikwa, jambo la kwanza linalompata ni fitina ya kaburi.
Imepokewa katika sahihi mbili ya Bukhari na Muslim kutoka kwa Anas Bin Malik Akipokea kutoka kwa Mtume ﷺ:
إِنَّ الْعَبْدَ إِذَا وُضِعَ فِي قَبْرِهِ وَتَوَلَّى عَنْهُ أَصْحَابُهُ وَإِنَّهُ لَيَسْمَعُ قَرْعَ نِعَالِهِمْ ، أَتَاهُ مَلَكَانِ فَيُقْعِدَانِهِ فَيَقُولَانِ : مَا كُنْتَ تَقُولُ فِي هَذَا الرَّجُلِ لِمُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ؟ فَأَمَّا الْمُؤْمِنُ فَيَقُولُ : أَشْهَدُ أَنَّهُ عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ ، فَيُقَالُ لَهُ : انْظُرْ إِلَى مَقْعَدِكَ مِنَ النَّارِ قَدْ أَبْدَلَكَ اللَّهُ بِهِ مَقْعَدًا مِنَ الْجَنَّةِ فَيَرَاهُمَا جَمِيعًا ، قَالَ قَتَادَةُ : وَذُكِرَ لَنَا أَنَّهُ يُفْسَحُ لَهُ فِي قَبْرِهِ ، ثُمَّ رَجَعَ إِلَى حَدِيثِ أَنَسٍ , قَالَ : وَأَمَّا الْمُنَافِقُ وَالْكَافِرُ فَيُقَالُ لَهُ : مَا كُنْتَ تَقُولُ فِي هَذَا الرَّجُلِ ؟ فَيَقُولُ : لَا أَدْرِي ، كُنْتُ أَقُولُ مَا يَقُولُ النَّاسُ ، فَيُقَالُ : لَا دَرَيْتَ وَلَا تَلَيْتَ وَيُضْرَبُ بِمَطَارِقَ مِنْ حَدِيدٍ ضَرْبَةً ، فَيَصِيحُ صَيْحَةً يَسْمَعُهَا مَنْ يَلِيهِ غَيْرَ الثَّقَلَيْنِ
[Hakika mja anapo wekwa katika kaburi lake na wakaondoka watu wake, Anasikia mlio wa viatu vyao. Akasema wanamjia Malaika wawili wakamkalisha wakamuambia unasemaje juu ya mtu huyu. Akasema: Ama Muislamu atasema: Nilikuwa nikishuhudia ya kwamba ni mja wa Mwenyezi Mungu na ni Mtume wake. Akasema: Ataambiwa angalia makao yako motoni umebadilishiwa pepo Atayaona makao mawili. Amesema Qatada tumeelezwa: hukunjuliwa kaburi lake. Ama mnafiki na Kafiri ataulizwa unajua nini juu ya Mtu huyu atasema sijui nilikuwa nikisema walivyokuwa wakisema watu ataambiwa hukujuwa na wala hukutaka kujua atapigwa nyundo ya chuma moja moja, atapiga ukelele watasikia watu wote wasiokuwa viumbe aina mbili (wanadamu na majini)]. [Imepokewa na Bukhari]
Na imepokewa na Abu Ayyub radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie Amesema:
[خرج رسولُ الله - صلى الله عليه وسلم - بعدما غَربت الشَّمس، فسَمع صوتًا، فقال: [يَهودُ تُعذَّب في قبورها
[Alitoka Mtume ﷺ na jua limetoka, Akasikia sauti ya Yahudi ana adhibiwa katika kaburi lake’] [Imepokewa na Bukhari na Muslim].
Kwa hivyo, Alikuwa Mtume haswali swala yeyote ila alikuwa akijilinda na adhabu ya kaburi. Na akaamrisha hivyo watu wake].
Kisha ataadhibiwa kafiri na mnafiki. Na Mu’mini atastarehe. Basi tujiulize nafsi zetu, je tumeandaa jawabu ya masuali ya kaburini. Ewe mja wa Mwenyezi Mungu, hakika hiko ni kiyama kitakuja hakina shaka. Na baada yayote atawafufuwa Mwenyezi Mungu walioko kwenye makaburi. Na dalili ni Aya tukufu:
وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ ۖ قَالَ مَن يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ} يس:78-79}
[Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika?Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba.] [Yaasin : 77 – 79].
Halafu atawakusanya watu wote kwa ajili ya hisabu. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:
مَن يَهْدِ اللَّهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُمْ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِهِ ۖ وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا ۖ مَّأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ كُلَّمَا خَبَتْ زِدْنَاهُمْ سَعِيرًا
[Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali wakikokotwa juu ya nyuso zao, nao ni vipofu na mabubu na viziwi. Na makaazi yao ni Jahannamu. Kila moto ukifanya kusinzia tutazidi kuuchochea uwake] [Al-Israa :97]
Haya ndiyo matukio ya kuogopesha utawaona wabaya na madhalimu na wanafiki wameinamisha vichwa vyao, hawarudishi macho yao, wala hasemi siku hiyo ila aliye pewa ruhusa na Mwenyezi Mungu ﷻ. Na nyoyo siku hiyo zimefika kooni wamekasirika na madhalimu hawana muombezi wala rafiki mwenye kutiiwa. Na siku hii kiasi chake ni miaka khamsini alfu.
Wakati huo watu watasimama mbele ya Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala. hakuna pa kufichika. Siku hiyo watu watatoka makaburini vikundi vikundi kwa ajili ya kuona vitendo vyao. Na itaanza hisabu. Amesema Mtume ﷺ:
يجاء بالكافر يوم القيامة فيقال له أرأيت لو كان لك ملء الأرض ذهبا أكنت تفتدي به فيقول نعم فيقال له قد كنت سئلت ما هو أيسر من ذلك
[Ataletwa kafiri siku ya kiama aambiwe waonaje lau ungekuwa na mjazo wa ardhi dhahabu ungalijikomboa? atasema ndiyo. Ataambiwa umeulizwa ambalo ni sahali kuliko hilo]. [Imepokewa na Bukhari]
Na katika mapokezi mengine:
[أردت منك ما هو أهون من هذا وأنت في صلب آدم أن لا تشرك شيئا فأبيت إلا أن تشرك بي]
[Nimekuuliza ambalo ni sahali kuliko hili na wewe uko katika mgongo wa Adam usimshirikishe Mwenyezi Mungu ﷻ ukakataa ila unishirikisha na viumbe vingine].
Ndugu Muislamu haya ni baadhi ya yale yatakayo tokea siku ya kiama, mbali na yale tuliyo ghafilika nayo. Na kila mmoja katika sisi atakuwa juu ya yale aliyo yafanya katika maasi. Ewe hakimu, Ewe rais, utatubiya lini? rudi kwa Mwenyezi Mungu ﷻ . Utamwambia nini Mola wako. Je hukumbuki neno la Mtume ﷺ:
ما من عبد يسترعيه الله رعية يموت يوم يموت وهو غاش لرعيته إلا حرم الله عليه الجنة] متفق عليه]
[Hakuna mchungaji yoyote aliye pewa uchungaji na Mwenyezi Mungu, atakufa siku atakayo kufa na yeye ni mdanganyifu ila Mwenyezi Mungu atamuharamishia pepo]. [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Enyi mawaziri na manaibu hamuogopi Mwenyezi Mungu kwa mliyo yabeba juu ya mabega yenu. Je mume jiandaa vipi na hali hii ya utisho miongoni mwa fitina ya kaburi na adhabu yake kukusanywa kwa ajili ya hisabu. Nini mume jianda na siku hiyo. Ewe Mwenye kufanya khiyana, Je utawacha lini khiyana zako, utasimamisha lini swala. Rudi kwa Mwenyezi Mungu ﷻ. Na wewe mwizi utaaacha lini wizi wako kwa hakika huna budi lazima upitie njia hii ngumu. Na wewe barobaro umejiandaa vipi na siku hii. Je umejiandaa na siku ya kufa. Na wewe msichana wadhani ya kwamba kifo hakitakuja kwako?
Na baada ya hapo zifunguliwe vitabu. Na wenye kupewa vitabu ni aina mbili; ni mwenye kupokea kitabu kwa mkono wa kulia, na mwenye kupewa kitabu kwa mkono wa kushoto. Kisha iwekwe mizani kwa uadilifu siku ya kiama. Baada ya hayo itakuja sirat na kila mmoja atapitia njiya hiyo. Tunamuomba Mwenyezi Mungu ﷻ atuafikie tuweze kufaulu katika siku hii nzito.
SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH YUSUF ABDI
ATHARI YA MASIA KATIKA MAISHA YA BINADAMU
Himidi zote na shukurani zote ni za Mwenyezi Mungu alieumba Mbingu na Ardhi akaumba na binadamu kwa malengo ya kumuabudu yeye peke yake. Aliyeweka Twaa na Maasia, mwenye kumtii ataingia peponi na mwenye kumwasi ataingia motoni. Swala na Salamu zimshukie kipendi chetu Mtume Muhammad ﷺ Yeye na Aali zake na Swahaba zake wote.
Hakika maasia yana athari mbaya kwa mtu mmoja bali kwa mujitamaa wote. Na wala hakuna shaka ya kwamba maasia wanayo fanya watu usiku na mchana athari ambayo inaangamiza mtu mmoja na jamii yote na maisha yote. Kwa hivyo, nguzo ya maisha na kutengenea kwa maisha ni katika twaa na kwa msimamo juu ya amri ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) na kufuata sharia ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) iliyo safi. Na kujiepusha na twaa na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)ni kumfuata shetani.
Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ ۙ وَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ ۚ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَائِنَةٍ مِّنْهُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاصْفَحْ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ
[Basi kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani, na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyo kumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipo kuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na waache. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.] [Al-Maidah : 13].
ATHARI YA MAASIA
1- Nyoyo kuwa ngumu
2- Kubadilisha maneno ya Allah (Subhaanahu wa Taala) bila ya kujali
3- Raana ndani ya moyo nayo moyo kuwa mweusi. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala (Si hivyo! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao kwa maovu waliyoyachuma). Inaonyesha ya kwamba maasia yana athari mbaya sana, nazo ni kuwa nyeusi nyoyo za watu wenye kuasi hapo huwa hazijui mema wala mabaya, haziamrishi mema wala hazikatazi mabaya.
4- Kusahau kitabu cha Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala. Na tunaposahau maagizo ya Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala) ni kuishi maisha mabaya. Kama Alivyosema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا ۖ وَكَذَٰلِكَ الْيَوْمَ تُنسَىٰ}
[Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona? (Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa.] [Twaha: 124-126]
- Athari kubwa ya maasia na iliyo khatari ni ugomvi baina ya mja na Mola wake.
- kuwa mzito kumtii Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)
- Kukosekana hifadhi ya Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala)
- Kusalitiwa na maadui na kuwa dhaifu mbele ya adui pamoja na kuondolewa utisho kutoka katika nyoyo za maadui
- Kudhihiri njaa na kuondoshwa baraka katika riziki.
SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH ATHMAN SHEE
KUMTEGEMEA MWENYEZI MUNGU SUB'HANAHU WA TA'ALA
Namshukuru Mwenyezi Mungu ﷻ Ambae wanamtegemea yeye wenye kumtegemea, Aliyesema mwenye kumtegemea yeye anamtosha. Sala na Salamu zimshukie Mtume Muhammad, Mtume wa mwisho na Jamaa zake na Sahaba zake wote..
Kutegemea imechukuliwa katika neno (wakala) kama kusema fulani amelitegemeza jambo lake kwa fulani na akamtegemea yeye. Kwa hivyo, kutegemea ni tafsiri ya kutegemea kwa mwenye kutegemewa, na wala hamtegemei mwanadamu mtu mwingine ila anaitakidi kwake kupata jambo.
Kutafuta riziki ni maumbile ya kila mwanadamu. Utaona kukipambazuka mwanadamu anakwenda mbio, kwa sababu ya kutafuta riziki. Mkulima anajiandaa kwenda shambani. Mfanya biashara ajiandaa kwenda kwenye biashara yake. Kila mja hujiandaa kivyake. Na wote wanapata shida kwa sababu kila mmoja anataka kuhifadhi na kupata chakula cha yule anayemlazimu kumlisha; mke, watoto ama chakula cha familia yake.
Na hakika kuwa na himaya ya kutafuta cha kutosheleza au kutaka utajiri pamoja na kuwa njia yake ina vikwazo na safari ndefu. Yote hayo hupelekea lawama. Enyi Waja Dini ya kiislamu inakataa ya kwamba riziki inapatikana kwa njia ya udanganyifu. Na inakataza na kuchukia Muislamu kuitegemea njia hiyo ili apate riziki kutokana nayo. Na katika kuziba mlangu huu na njia hii. Amesema Mtume ﷺ:
ولا يحملن أحدكم استبطاء رزقه أن يخرج إلى ما حرم الله عليه فإنه لا يدرك ما عند الله إلا بطاعته] رواه عبدالرزاق والطبراني]
[Isiwepelekeeni nyinyi uzito wa kupata riziki mukaingia katika kumuasi Mwenyezi Mungu. Hazipatikani zilizoko kwa Mwenyezi Mungu ila kwa Twaa yake]. [Imepokewa na Abdurazzaq na Al Twabraniy]
Kwa hivyo, ni yapi mapitio? Na nini suluhisho kutokana na maisha haya wanaoishi, watu wanatusiana, baadhi yao wanakula nguvu za wengine na baadhi yao kuwadhulumu baadhi. Na katika zama zetu hizi tunazoishi tunashuhudia hayo na kuna mifano mingi.
Ndugu Muislamu isome Hadithi hii inayotoka kwa Mtume wenu Muhammad, ikipokewa na ‘Umar Bin Khatwab (R.A) Akisema: “Nimemsikia Mtume ﷺ:
لو أنكم تتوكلون على الله حق توكله لرزقكم كما يرزق الطير، تغدو خماصاً وتروح بطاناً] رواه الترمذي]
[Lau hakika nyinyi mungalikuwa munamtegemea Mwenyezi Mungu haki ya kumtegemea, Angaliwaruzuku nyinyi kama anavyowaruzuku ndege, anatoka asubuhi akiwa na njaa, na anarudi jioni akiwa ameshiba.] [Imepokewa na Al-Ttirmidhi]
Kutokana na hadithi hii tunajifunza ya kwamba tukimtegemea Mwenyezi Mungu kikweli basi Mwenyezi Mungu atatupa tunalolitaka.
Ndugu Muislamu, zimekuja Aya nyingi na Hadithi nyingi zilizo sahihi kubainisha kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa kila jambo letu na katika maisha yetu yote. Na hakika kumtegemea Mwenyezi Mungu ni jambo kubwa na ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu akiwaamrisha waja wake Waislamu. Amewaamrisha hilo kwa hali zote. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:
وَلِلَّهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِلَيْهِ يُرْجَعُ الْأَمْرُ كُلُّهُ فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ} هود:123 }
[Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyo fichikana katika ardhi na mbingu, na mambo yote yatarejezwa kwake. Basi muabudu Yeye na umtegemee Yeye. Na Mola wako Mlezi haghafiliki na yale mnayo yatenda.] [Huud : 123]
Na Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:
وَتَوَكَّلْ عَلَى الْحَيِّ الَّذِي لَا يَمُوتُ وَسَبِّحْ بِحَمْدِهِ ۚ وَكَفَىٰ بِهِ بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا} القرقان:58}
[Na mtegemee Aliye Hai, ambaye hafi. Na umtukuze kwa sifa zake. Na yatosha kwake kuwa yeye ni Mwenye khabari za dhambi za waja wake.] [Al-Furqan : 58].
Na Amesema tena Subhanahu wa Ta'aala:
وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ } الشعراء217}
[Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.] [Shuaraa : 217].
Na Amesema tena Mwenyezi Mungu Subhanahu waTa'aala:
وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّهِ وَكِيلًا} الأحزاب:3}
[Na mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni wa kutegemewa.] [Ahzaab : 3].
Na katika Hadithi ya Mtume ﷺ inatuelezea kuhusu kumtegemea Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Imetokana na Abu Hurayra radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie Akipokea kwa Mtume ﷺ:
يدخل الجنة أقوام أفئدتُهم مثل أفئدة الطير] رواه مسلم]
[Wataingia peponi watu nyoyo zao ni mfano wa nyoyo za ndege.] [Imepokewa na Muslim]
Maana yake wanaomtegemea Mwenyezi Mungu na kumesemwa nyoyo zao ni laini.Ewe Ndugu, Muislamu Hakika kutegemea ni kusadikisha kutegemea moyo kwa Mwenyezi Mungu katika kuleta mambo mema na kuondosha madhara. Vilevile kumtegemea Mwenyezi Mungu ni ukweli na imani na utulivu na kua na mafungamano baina ya mja na Mola wake.
Amesema Ibnul-Qayyim Mwenyezi Mungu Amrehemu : "Kutegemea ni nusu ya imani na ni nusu ya pili ya kurudi kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu amewaahidi wenye kumtegemea malipo makubwa na malipo mengi "Katika Hadithi iliyoko katika sahihi mbili hadithi ya watu sabini elfu wataingia peponi bila hisabu, nao ni wale ambao hawataki kuzunguliwa, wala hawajichomi, wala hawatabiri ndege wanamtegemea Mola wao".
Na hakukuwa kutegemea Mwenyezi Mungu kunakanusha kuchukua sababu za sheria zilizo halali. Mfano mtu akisema mimi sitafuti riziki wala siendei mbio, ikiwa imeandikwa kwangu niwe tajiri nitakuwa tajiri bila kutaabika wala shida, ikiwa Sikuandikiwa basi siwi hakuna haja nisumbuke wala nipate taabu. Kwahivyo, linalotakiwa ni kumtegemea Mwenyezi Mungu pamoja na kufuata sababu.
Na Mtume ﷺ Amewasifu wenye kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa sifa mbili:
1. Kwenda kutafuta riziki.
2. kutegemea sababu za kisheria.
Mwenye kukosa moja wa sifa mbili hizi hakika ameangukia patupu na amefanya shirki. Na mwenye kwenda kwa sababu zilizo halali na akamtegemea mola wake na akamshukuru mola kwa kila yanayopendeza na akasubiri hukumu ya Mwenyezi Mungu wakati anapopata msiba na machukivu amefaulu na amefadhilisha ukamilifu wote.
SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH SHADDAD ALI
ALAMA ZA SIKU YA QIYAMA
Ni lazima kwa kila Muislam ajue nguzo za imani,na niliza kuamini nguzo kama hizo na kutenda amali njema kwa ajili yake. na Katika nguzo za imani kuna kuamini siku ya kiama ambayo ni siku ya mwisho siku ya malipo. na kabla siku hii haijafika kuna alama za kuonesha kwamba imeshakaribia. Na sio siri kwani zimesha dhihiri baadhi ya alama,kwa hivyo ni vyema muislamu ajiandae na siku hiyo,Mwenyezi Mungu ﷻ Anasem:
فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً ۖ فَقَدْ جَاءَ أَشْرَاطُهَا ۚ فَأَنَّىٰ لَهُمْ إِذَا جَاءَتْهُمْ ذِكْرَاهُمْ} محمد:18}
[Kwani wanangoja lingine ila kiama kiwajie? basi alama zake zimekwisha kuja, kutawafaa nini wakati kitakapowajia] [ Muhammad : 18].
Ni lazima kwa kila muislamu kuamini siku ya mwisho alipe umuhimu mkubwa suala hili, kwani haikamiliki imani ya mtu mpaka aamini alama za kiama (kwani kuamini alama hizo ni katika kuamini siku ya kiama)ukizingatia kwamba Mtume ﷺ alizitaja alama hizi na hakitasimama kiama mpaka zitokee alama hizi. Swahaba Hudhaifa ibn Asiid radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema:[ Tulikuwa tumekaa katika kivuli cha chumba cha Mtume ﷺ tukataja kiama na sauti zetu zikawa juu (mpaka Mtume ﷺ akasikia) akasema :
[إنها لن تقوم حتى ترون قبلها عشر آيات]
[Hakika hakitosimama kiama mpaka muone kabla yake alama kumi]. [Imepokewa na Muslim].
Na Mwenyezi Mungu ﷻ Amebainisha ya kwamba siku ya kiama haijulikani ni wakati gani na wala hakuna anayejua isipokuwa yeye peke yake. Na hakumhusisha yoyote kukijuwa kiama si Malaika aliyekurubishwa wala Mtume aliyetumilizwa na Mwenyezi Mungu. Pia imebainishwa kwamba kiama kimekaribia wakati wake kama zilivyoeleza Aya za Quran Tukufu na hadithi za Bwana Mtume ﷺ Mwenyezi Mungu s.w. Amesema:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي ۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَا إِلَّا هُوَ ۚ ثَقُلَتْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا تَأْتِيكُمْ إِلَّا بَغْتَةً ۗ يَسْأَلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنْهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ اللَّهِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ الأعراف:187
[Wanakuuliza kuhusu kiama kitakuja lini? sema: ilimu yake iko kwa Mola wangu tu hakuna wa kudhihirisha wakati wake ila yeye. Imekuwa nzito mbingu na ardhi, hakita kuja kiama ila ghafla] [Al-Araaf : 187].
Amesema Mwenyezi mungu Subhaanahu wa Taala :
يَسْأَلُكَ النَّاسُ عَنِ السَّاعَةِ ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ اللَّهِ ۚ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا} الأحزاب:63}
[Watu wanakuuliza kuhusu kiama kitakuja lini? sema: ilimu yake iko kwa Mola wangu tu. Na kipi kitakacho kujulisha lini kiama, pengine kiama kiko karibu] [Al-Ahzab : 63].
Na pale Jibril alipomuuliza Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam kuhusu kiama Mtume ﷺ akajibu:
[hakuwa mwenye kuulizwa ni mjuzi kuliko anayeuliza]
Aya na hadithi za Mtume ﷺ zinazoshiria kwamba hakuna anayejuwa wakati wa kutokea kiama isipokuwa Mwenyezi Mungu ﷻ.
Vile vile mitume waliobakia hawajui wakati gani kiama kitasimama.
Kwa kweli Mwenyezi Mungu amebainisha wazi kwamba kiama kimekaribia na vile vile Mtume wetu Muhammad rehma na amani zimfikie ameweka wazi katika hadithi zake kwamba kiama kimekaribia sana.
Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amesema kwenye Qurani Tukufu:
وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا} الأحزاب:63}
[Na kipi kitakujulisha lini kiama pengine kiko karibu] [Al-Ahzab : 63].
Mwenyezi mungu Subhaanahu wa Taala Amesema:
اقْتَرَبَ لِلنَّاسِ حِسَابُهُمْ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ مُّعْرِضُونَ} الأنبياء:1}
[imekaribia watu hisabu yao(ya kiama)nao wamo katika kughafilika na wanalipuuza] [Al-Anbiya : 1].
Mtume ﷺ Nasema:
بُعِثْتُ أَنَا وَالسَّاعة هكذا - ويشير بأصبعيه فيمدُّ بهما] رواه البخاري ومسلم]
[Nimetumilizwa na kiama kama vidole viwili]. Akashiria vidole viwili cha kati na cha shahada. [Imepokewa na Bukhari wa Muslim]
VIGAWANYO VYA ALAMA ZA QIYAMA
Kwa hakika alama za kiama zimegawanyika vigawanyo viwili.
Alama ndogo.
Alama kubwa.
Alama ndogo ni zinatangulia au zinazokuja kabla ya siku kiama kwa mda mrefu na zinazoeleka na zinaweza kudhihiri baadhi yake pamoja na alama kubwa au zikaja baada ya alama kubwa.
Ama alama kubwa ni mambo makubwa ambayo yatadhihiri karibu na kiama na huwa si ya kawaida kwa mfano kuja Dajjal na nyenginezo.
Na ukizingatia kudhihiri kwake zimegawanyika vigawanyo vitatu
Alama zilizodhihiri na kuweko
Alama zilizodhihiri na bado zinatokea
Alama ambazo hazijatokea mpaka sasa.
ALAMA NDOGO ZA SIKU YA QIYAMA
Alama ndogo za kiama nazo ni kama zifuatazo;
1.Kutumilizwa Mtume ﷺ.
Mtume ﷺ amesema:
بُعِثْتُ أَنَا وَالسَّاعة هكذا - ويشير بأصبعيه فيمدُّ بهما] رواه البخاري ومسلم]
[Nimetumilizwa na kiama kama vidole viwili]. Akashiria vidole viwili cha kati na cha shahada.
2. Kufa Mtume ﷺ ni miongoni mwa alama ndogo za kiama, kwani ni ishara wazi ya kukatika wahyi kutoka mbinguni.
3. kudhihiri fitna kubwa; itachanganyika haki na batili zitatikisika imani mpaka mtu ataamka asubuhi hali ya kuwa ni muislamu na atalala hali ya kuwa ni kafiri au atalala hali ya kuwa ni kafiri na ataamka hali ya kuwa ni muislamu.
Hii ni kuonesha kwamba mtu kuingia katika ukafiri ni wepesi kwa kule kuchanganyika haki na batili na ndio hali za zama zetu hizi, watu wamechanganyikiwa kiasi kwamba hawajui haki ni ipi na batili ni ipi. Na kila ikidhihiri fitna atasema haya ndio maangamivu yangu kisha itaondoka itakuja nyingine atasema muumini haya ndio maangamivu na na hazitawacha fitna kudhihiri kwa watu mpaka kiama kisimame. Mtume ﷺ amesema:
إن بين يدي الساعة فتنا كقطع الليل المظلم, يصبح الرجل فيها مؤمناً ويمسي كافراً, ويمسي مؤمناً ويصبح كافراً, القاعد فيها خير من القائم, والقائم فيها خير من الماشي, والماشي فيها خير من الساعي رواه أحمد وأبوداود وإبن ماجة
[Hakika kabla ya kiama kutakuwa na fitna kama kipande cha usiku wa giza mtu ataamka muislamu na atalala kafiri na atalala kafiri na ataamka muislamu na aliyekaa ni bora kuliko aliyesimama na aliyesimama ni bora kuliko aliyetembea na anayetembea ni bora ni kuliko anayekwenda mbio]. [Imepokewa na Ahmad na Abuu Dawud na Ibnu Maajah]
4.Kudhihiri moto katika ardhi ya Hijazi na kupotea amana. Mtume ﷺ:
لا تقوم الساعة حتى تخرج نار من أرض الحجاز، يضيء لها أعناق الإبل ببُصرى] رواه البخاري ومسلم]
[Hakitasimama kiama mpaka utoke moto katika ardhi ya Hijazi unatoa mwangaza moto huo kiasi utaona shingo za ngamia Basra]. [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Hakika moto huu umeshadhihiri katikati ya karne ya saba mwaka 654 hijria na ulikuwa mkubwa waliweza kuuona wanavyuoni wengi ambao waliokuwa zama hizo na waliokuja baada yao katika kuuelezea moto huo.
5. Vilevile kupotea amana ni katika alama za kiama watu kutotekeleza majukumu waliopewa na kutowajibika inavyotakiwa, Mtume ﷺ asema:
إِذَا ضُيِّعَتِ الأَمَانَةُ فَانْتَظِرِ السَّاعَةَ] رواه البخاري]
[Ikipotea amana ngojea kiama]. [Imepokewa na Bukhari]
6.Kuenea zinaa kiasi kwamba litakuwa jambo la kawaida na asiyejihusisha na jambo hilo watu. Mtume ﷺ:
والذي نفسي بيده؛ لا تفنى هذه الأمة حتى يقوم الرجل إلى المرأة، فيفترشها في الطريق، فيكون خيارهم يومئذ من يقول لو واريتها وراء هذا الحائط أخرجه أبو يعلى في مسنده حديث وصححه الألباني في الصحيحة
[Naapa kwa ambae nafsi yangu iko mkononi mwake hautamalizika umma huu mpaka asimame mwanamume na mwanamke na amlaze njiani afanye nae zinaa aseme mbora wao siku hiyo lau mtazunguka nyuma ya ukuta (mufanyie huko) ]. [Imepokewa na Abuu Ya'alaa katika Musnadi yake na kusahihishwa na Al Baniy]
7.Kuenea ribaa tukijua kuwa riba ni katika madhambi makubwa sana lakini namna itakavyoenea litakuwa jambo la kawaida, lakini watu hawajali na watajaza matumbo yao haramu.
Mwenyezi mungu Subhaanahu wa Taala Amesema:
{وَأَحَلَّ اللَّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا ۚ} البقرة:275}
[Na Mwenyezi Mungu amehalalisha biashara na ameharamisha riba ] [Al-Baqara : 275].
Mtume ﷺ amesema:
بين يدي الساعة يظهر الربا، والزنا، والخمر] رواه الطبراني]
[Kabla ya kuja kiama kutadhiri riba na zinaa na pombe]. [Imepokewa na Al Twabraniy]
8.Kudhihiri na kuenea muziki kwa wingi na watu watahalalisha miziki hiyo, Mtume ameeleza haya katika hadithi zake nyingi suala hili kwa hivyo inatakiwa Waislamu wachunge mipaka ya Mwenyezi Mungu kwa kuomba msamaha kwake na kutubia, kwani hali za wanaadamu ni mbaya na za kusikitisha sana. Huku tusisahau kupeana nasaha kwa kuamrishana mema na kukatazana yalio mabaya.
9.Watu kujenga majumba makubwa na marefu tena kutoka kwa watu walio kuwa duni katika jamii kufikia kiwango cha utajiri na haya ni kwa mujibu wa maneno ya Mtume ﷺ:
أن تلد الأمة ربتها، وأن ترى الحفاة العراة العالة رعاء الشاء يتطاولون في البنيان] رواه البخاري]
[Ni kuzaa mtumwa wa kike bwana wake na utaona watu wasiokuwa na viatu waliouchi, masikini, wachunga mbuzi wanashidana kurefusha majumba]. [Imepokewa na Bukhari]
Na Mtume ﷺ Amesema:
لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يَتَبَاهَى النَّاسُ فِي الْمَسَاجِدِ] رواه أبوداود وصححه الألباني]
[Hakitasimama kiama mpaka watu wajifakhiri kwa kujenga Misikiti]. [Imepokewa na Abuu Dawud na kusahihishwa na Al Baaniy]
10.Kukithiri uongo baina ya watu, watadanganyana kwa wingi huku tunajua kwamba uongo ni katika makosa makubwa Aliyoyakataza Mwenyezi Mungu katika Qurani na vile vile Mtume rehma na amani zimfikie ameukataza uongo katia hadithi zake tukufu. Mtume ﷺ amesema katika hadithi yake:
لا تقوم الساعة حتى تظهر الفتن ، ويكثر الكذب ، وتتقارب الأسواق] رواه مسلم]
[Hakitasimama kiama mpaka zidhihiri fitna, kukithiri uongo na kukaribiana masoko]. [Imepokewa na Muslim]
11. Vilevile hakitasimama kiama mpaka atamani aliye hai mauti kwa namna hali za watu zitakavyokuwa mbaya. Mtume ﷺ:
لا تقوم الساعة حتى يمر الرجل بقبر الرجل ، فيقول : يا ليتني مكانه] رواه البخاري ومسلم]
[Hakitasimama kiama mpaka mtu aende kwa kaburi la mtu aseme natamani mahali pako]. yaani atatamani alie hai afe yeye. [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Kukaribiana masoko ni miongoni mwa dalili za kiama kama ilivyo tanguli katika Hadithi.
[Hakitasimama kiama mpaka kukithiri uongo na kukaribiana masoko].
Hizi ndio miongoni mwa alama chache za kiama na ni vyema kwa muislamu yoyote azijue vizuri kwani akiziona huenda akajiandaa na siku ya mwisho kabla hajafikiwa na mauti kwa kufanya vitendo vizuri na kujiepusha na vitendo vibaya.
SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH HASSAN SUGO
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.