Menu

UCHAJI MWENYEZI MUNGU NA ATHARI ZAKE


  613


Ni nini uchaji mungu?. Ni kujiepusha na kila ambalo Mwenyezi Mungu halitaki na kutekeleza kila jambo ambalo Mwenyezi Mungu analipenda. Vile vile, uchaji Mungu ni kujilinda na adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kufanya vitendo vizuri, na kuogopa kwa siri na kwa dhahiri. Na kuogopa. Ni kama alivyosema Ali Bin Abi Twalib: ‘ Ni kumuogopa Mola, na kutumia Qur’an, na kuridhika na kidogo, na kujianda kwa siku ya safari’. Imekuja ya kwamba ‘Umar Bin Khatwab radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie alimuuliza Ubayyah Bin Ka’ab: Taqwa ni nini? Akamwambia: Je umefuata njia ya miba? Akamwambia kwa nini? Hukujua? Akasema nilitembea kwa hadhari kuogopea miba kunidunga. Akasema hiyo ndiyo taqwa’.

Kumuogopa Mwenyezi Mungu ni mkusanyiko wa kheri na mambo mengi yametajwa katika Qur’an tukufu. Hakuna kheri yoyote ya dunia na akhera wala ya ndani na nje ila Taqwa imeshikanishwa nazo. Na hakuna shari yoyote ya dunia na akhera wala ya ndani na nje ila Taqwa imekuwa mbali nayo. Na katika kheri za Taqwa ni kufunguliwa milango ya kheri, na kwa Taqwa hufunzwa usioyajua.
Taqwa ni wasia wa watu wa mwanzo na wa mwisho. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

 

إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا}   النساء:131}

 

[Na kwa hakika tuliwausia waliopewa kitabu kabla yenu, na nyinyi pia, kwamba mumche Mwenyezi Mungu ]    [Nisaa : 131]
Na Taqwa ni Mwito wa Mitume na alama ya waja wema. Kila Mtume alikuwa akiwaambia watu wake:


 أَلَا تَتَّقُونَ}    الشعراء:124}

[Je hamumuogopi Mungu]   [Ashuaraa :124]
Taqwa asli yake ni kinga baina ya mja na lile analoliogopa na kujitahadhari nalo. Na Mola wetu mtukufu ndiye Anaye stahiki kuogopewa nayeye pekee ndiye Anayetukuzwa. Kama Alivyosema Ali Radhi za Mwenyezi Mungu juu yake ‹Taqwa ni kumuogopa Mwenyezi Mungu na kutumia kitabuchake (Qur’an) na kutosheka na kichache na kujiandalia siku ya safari›.

SIFA ZA WACHAJI MUNGU.

Sifa za wanaomuogopa Mwenyezi Mungu. Katika sifa za wanaomuogopa Mungu (Subhaanahu wa Taala):
1. Kuamini mambo ya siri (ghaib)
2. Kusimamisha Swala kwa wakati wake.
3. Kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
4. Kuamini Aliyoteremsha Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala).
5. Kuwa na yakini na Siku ya Akhera. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

 

الم ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ أُولَٰئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ ۖ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

 

[Alif laam miim Hiki ni kitabu hakina shaka ndani yake ni ongofu kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu. Ambao huyaamini yasioonekana na husimamisha swala na hutoa zile tulizowapa. Na ambao wanaamini yaliyo teremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako na wanaamini Akhera. Hao wako juu ya ongofu utokao kwa Mola wao na hao ndio waongufu"]    [Al-Baqara : 1 - 5]

6. Kutekeleza ahadi na kusubiri wakati wa raha au shida. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)


لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ وَآتَى الْمَالَ عَلَىٰ حُبِّهِ ذَوِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَالسَّائِلِينَ وَفِي الرِّقَابِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُوا ۖ وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ ۗ أُولَٰئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا ۖ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ

 

[Bali wema ni wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Mitume na wanawapa mali – juu ya kuwa wanayapenda- jamaa na mayatima na maskini na wasafiri na waombao na kuwakomboa watumwa na wanasimamisha swala na kutoa zaka, na watekelezao ahadi zao wanapoahidi, na wavumiliao katika shida na raha na wakati wa vita ]   [AL-Baqarah : 177]
7. Kuomba msamaha kwa madhambi yao. Kama Alivyosema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):


وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ       آل عمران:135

 

[Na wale ambao wanapofanya uchafu au kudhulumu nafsi zao hukumbuka Mwenyezi Mungu na kuomba msamaha kwa dhambi zao ]     [Al-Imraan : 135].

 

FADHILA ZA TAQWA

Taqwa hufungua moyo. Kama Alivyosema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):


{وَاتَّقُوا اللَّهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّهُ}    {البقرة:282}

 

[Muogopeni Mwenyezi Mungu atawafundisha nyinyi"]  [Al-Baqarah : 282]

Amesema Mola(Subhaanahu wa Taala):


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَتَّقُوا اللَّهَ يَجْعَل لَّكُمْ فُرْقَانًا وَيُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۗ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ}    الأنفال:29}

 

[Enyi mlioamini mkimuogopa Mwenyezi Mungu atawapa ufafanuzi kufafanua baina ya haki na batili na atakufutieni makosa yenu,na kukusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa kabisa]     [Anfal : 29]

Kupata kabuli. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

 

وَيُنَجِّي اللَّهُ الَّذِينَ اتَّقَوْا بِمَفَازَتِهِمْ لَا يَمَسُّهُمُ السُّوءُ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ}    الزمر:61}

 

[Na Mwenyezi Mungu Atawaokowa wale wamchao kwa ajili ya kufaulu kwao hawataguswa na ubaya na wala hatahuzunika ]   [Azumar : 61]
Kuokoka na moto na kufaulu kwa nyumba ya furaha. Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):

 

تِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي نُورِثُ مِنْ عِبَادِنَا مَن كَانَ تَقِيًّا}    مريم:63}

[Hiyo nidiyo pepo tutakayowarithisha katika waja Wetu wale ambao ni wachaji Mungu] [Maryam : 63]

Mwenyezi Mungu Atujaalie katika wale wanao muogopa Mwenyezi Mungu nakupata msamaha wake Allah. Muombeni msamaha Yeye peke yake. Hakika Yeye ndie Mwenye kusamehe waja wake wote.


SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH HASSAN SUGO



LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6574759
TodayToday2826
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 13

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682906a042d133491889771747519136
title_682906a042e7f14560102421747519136
title_682906a042fde20309396861747519136

NISHATI ZA OFISI

title_682906a0453c318032115411747519136
title_682906a04551613574023221747519136
title_682906a04565813407857951747519136 Add content here

HUDUMA MPYA

: 11 + 12 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com