Menu

MISINGI YA FIQHI

 

 

Misingi ya fiq-hi ni chimbuko la elimu hii yaani mahala ambamo elimu hii imechukuliwa.

Elimu ya fiq-hi imejiegemeza katika misingi mikuu minne kama ifuatavyo:

Qur-ani
Hadithi(sunnah)
Ijmaa,na
Qiyaasi

Hii ndio misingi na tegemeo la elimu hii ya fiq-hi.

Maana ya kila msingi

QUR-ANI

Qur-ani Tukufu ni kitabu kilichokusanya maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu alichoshushiwa Mtume wa mwisho, Nabii Muhammad kupitia kwa Malaika Jibril ili kiwe ni sheria na muongozo kwa wanadamu wote.

HADITH(SUNNAH)

Hadithi (sunnah) ni tafsiri sahihi na ufafanuzi kamili wa Qur-ani Tukufu uliotolewa na Bwana Mtume kwa njia ya vitendo, maneno na "Iqraari".

"Iqraari" ni kitendo cha Bwana Mtume kumuona mtu akitenda jambo fulani, kisha Mtume asitoe maelekezo yoyote ya kukemea au kukataza.

Ukimya huu wa Mtume hutafsirika kuwa jambo lile linafaa kwani Mtume hawezi kulinyamazia jambo baya.

IJMAA

Ijmaa ni kongamano na makubaliano ya wanazuoni wa kiislamu baada ya kuja Mtume juu ya jambo au suala ambalo halikuelezwa kwa uwazi ndani ya Qur-ani au hadithi

QIYAASI

Qiyaasi ni mizani ya kulipima jambo au suala ambalo halina ufafanuzi ndani ya Qur-ani au hadithi na jambo au suala lililotajwa ndani ya Qur-ani au Hadith, kwa kulingana sababu.

Kwa ufupi hizi ndizo maana nyepesi na za awali za misingi hii minne ambayo ndio chimbuko la elimu hii ya sheria ya Kiislamu, elimu ya fiq-hi.

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575340
TodayToday47
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 5

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682961da478f210949360401747542490
title_682961da47a137220465121747542490
title_682961da47b4a4662342461747542490

NISHATI ZA OFISI

title_682961da49c4114402560971747542490
title_682961da49d753659560281747542490
title_682961da49e9619273272581747542490 Add content here

HUDUMA MPYA

: 3 + 4 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com