UTAJO KATIKA MASH'ARUL HARAAM (MUZDALIFAH)

 

Amesema Jaabir radhi za Allah ziwe juu yake  kwamba ‘Mtume alimpanda Al-Qaswa (jina la ngamia wake) mpaka alipofika Mash’arul Haraam (huko Muzdalifah), kisha akaelekea Qiblah akamuomba Mwenyezi Mungu , akakabbir (akamtukuza), akaleta Tahlil (akamsifu), na akampwekesha. Hakuacha kusimama mpaka kulipopambazuka ndipo alipoondoka kabla ya kutoka jua.     [Imepokewa na Muslim.]


comments