Menu

SHIRKI


 مظاهر الشرك بالله عز وجل


MAANA YA SHIRKI 

Nayo ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta´ala) pamoja na kiumbe mwengine au kitu chochote kile kingine katika haki za Mwenyezi Mungu. Au sema ni kumsawazisha asiyekuwa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu katika yale mambo ambayo ni haki zake Mwenyezi Mungu.

Basi atakaeomba asiye Mwenyezi Mungu, au kuwapa majina ya Mwenyezi Mungu, au kuamini kwamba kuna Mola mwengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu, atakuwa amefanya shirki.

Na Shirki ni katika dhambi kubwa zaidi kuliko dhambi nyingine yoyote ile.

Mwenyezi Mungu mtukufu amesema:

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ}    لقمان:13}

 

[Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa]     [Luqmaan:13].

 Kwa nini Shirki ni dhulama kubwa, kwa sababu yeye Mwenyezi Mungu ndie anae umba na kuruzuku waja wake,na yeye ndie anaehuisha na ndie anafisha,na hakuna lolote linalokuwa katika ulimwengu huu ila ni kwa uwezo wake na matakwa yake Mwenyezi Mungu aliye tukuka,kasha mwanadamu akamwacha Mwenyezi Mungu aliye mneemesha neema zote hizi na akaenda kuabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu basi mja huu huwa amefanya dhulma ya hali juu.

Na kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu amemuharamishia kuingia peponi kwa yoyote yule atakae kufa hali ya kuwa ni Mushik,Mwenyezi Mungu anasema:

 

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ}    المائد:72}

 

[Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.]     [Al Maaida:72]

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu hamsamehe mja atake kufa hali ya kuwa ni mushrik,lakini allah huenda akamsamehe anaye mtaka ambae amekufa na madhambi mengine lakini hakuwa amemshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu,Mwenyezi Mungu anasema:

 

إِنَّ اللَّهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا}     النساء:48}

 

[Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa]    [Al Nisaai:48]


SIKILIZA SHEREHE YA MADA HII NA SHEIKH SALIM KHATIB



LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575725
TodayToday432
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 3

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6829e05a0f77517271352321747574874
title_6829e05a0f89913977540631747574874
title_6829e05a0f9af4184962671747574874

NISHATI ZA OFISI

title_6829e05a115a22207669201747574874
title_6829e05a116b4184836141747574874
title_6829e05a117bf328356261747574874 Add content here

HUDUMA MPYA

: 10 + 14 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com