MASHARTI YA LA ILAHA ILLA ALLAH


section 400


Nayo ni mambo ambayo haitimii kauli hii ya ikhlasi illa baada ya kupatikana haya masharti saba, yote pamoja. Na kama tunavyojua kwamba la ilaha illa Allah ndio ufunguo wa pepo lakini kila ufunguo lazima una meno. Nayo haya masharti ndiyo meno ya la ilaha illa Allah. Haifungui pepo bila haya meno:

[علم، يقين، وإخلاص، وصدقك مع ... محبة، وانقياد، والقبول لها]

 

[Elimu, yakini, ikhlasi, kusadikisha, upendo, kutii na kukubali]


1. Elimu ambayo haikubali kutomjua Mwenyezi Mungu
Lazima mwisilamu ajue maana ya la ilaha illa Allah ya sahihi ambayo ni kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki illah Mwenyezi Mungu, na asiwe kama wale hawaelewi maana yake kabisa kabisa ua wanaelewa maana yake vibaya kama wale wanaoelewa maana yake kuwa ni tauhidurububiyya. Nayo hii maana si kweli, kwani la ilaha illa Allah si tauhidurububiyya bali ni tauhidul-uluhiyya kama ilivyotangulia.

Dalili ya sharti ya elimu ni:

 

[ فَاعْلَمْ أَنَّهُ لا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنْبِكَ}     [محمد: من الآية 19}

 

[Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu]      [Muhammad aya 19]


2. Yakini ambayo haikulbali shaka
Baada ya kujua maana ya la ilaha illa Allah, ni lazima mwisilamu awe na yakini na imani ya kuwa hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki illa Mwenyezi Mungu , basi hafai kuweka shaka yoyote katika imani hiyo. Amesema Mwenyezi Mungu:

 

[ إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنْفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أُولَئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ}   [الحجرات: 15}

 

[Hakika Waumini ni wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake tena
wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Hao ndio wakweli]     [Hujuraat aya 15]

Naye mtume (Swala Allahu alaihi wasallam) huku akimwambia Abu Haraira (Radhia Allahu anhu):

 

اذهب بنعلي هاتين، فمن رأيت وراء هذا الحائط يشهد أن لا إله إلا الله مستيقنا بها قلبه، فبشره بالجنة]      رواه مسلم]

 

[Nenda na viatu viwili hivi vyangu, basi yeyote utakaeona nyuma ya huu ukuta akishuhudia kuwa hapa mola apasae kuabudiwa kwa haki illa Mwenyezi Mungu huku moyo wake ukiwa na yakini nayo, basi mbashirie pepo.]     [Imepokewa na Muslim]

3. Kukubali na kutokataa
Nayo ni kukubali mambo ambayo la ilaha illa Allah inaamrisha kwamba tufanye maamrisho na tuwache makatazo:

[ فَإِنَّهُمْ لا يُكَذِّبُونَكَ وَلَكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّهِ يَجْحَدُونَ}    [الأنعام: من الآية33]
 

[Tunajua ya kwamba yanakuhuzunisha wanayo yasema. Basi hakika wao
hawakukanushi wewe, lakini hao madhaalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.]  [Al-An`aam aya 33]

4. Kufuata
Nako ni kutenda na si kama kukubali ambako huwa tu kwa ulimi

 

[ وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا}    [ النساء: من الآية 125}

 

[Na nani aliye bora kwa dini kuliko yule aliye usilimisha uso wake kwa
Mwenyezi Mungu, naye akawa mwema, na anafuata mila ya Ibrahim mwongofu? ]    [Annisaa 125]

Na amesema Mtume ﷺ:

 

[ لا يؤمن أحدكم حتى يكون هواه تبعا لما جئت به ]     [ حديث حسن صحيح في كتاب الحجة بإسناد صحيح، وفي الجامع الصغير]

 

[Haamini mmoja wenu hata yawe matamanio yake ni yenye kufuata niliyokuja nayo]


5. Kusadikisha
Bila kukadhibisha ambako huwa ni jambo la wazi wazi au unafiki ambako ni kukadhibisha kwa ndani ndani.

 

[ الم، أَحَسِبَ النَّاسُ أَنْ يُتْرَكُوا أَنْ يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لا يُفْتَنُونَ، وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ}  [العنكبوت: 1-3}
 

[1. Alif Lam Mim (A.L.M.)2. Je! Wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe? 3. Hakika tuliwajaribu walio kuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha walio waongo.]     [Ankabuut aya 1-3]

Na neno lake Mtume ﷺ:

 

 ما من أحد يشهد أن لا إله إلا الله وأن محمدا رسول الله صدقا من قلبه، إلا حرمه الله على النار ]    رواه البخاري]
 

[Hakuna yeyote anaeshuhudia kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu ikisadikisha haya moyoni mwake ila Mwenyezi Mungu atamharamishia moto]     [Imepokewa na Bukhari]

 

Na Mtume alipomfundisha yule mwarabu mambo ya din ina mwarabu akamwambia: Naapa kwa Mwenyezi Mungu sitazidisha kwa haya wla sitapunguza chochote kwayo. Akasema mtume ﷺ:

 

أفلح إن صدق]    رواه البخاري]


[Amefaulu ikiwa ni mkweli]    [Imepokelewa na Bukhari]

6. Ikhlasi ipingayo shirki
Awe na ikhlasi kwa kuelekezwa moyo wake kwa Alla na asimshirikishe Allah na yeyote si kwa riyaa wala aina zengine za shirki.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

أَلَا لِلَّهِ الدِّينُ الْخَالِصُ}    الزمر:3}

 

[Hakika Dini Safi ni ya Mwenyezi Mungu tu.]    [Azzumar:3]

Na amesema tena Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

قُلِ اللَّهَ أَعْبُدُ مُخْلِصًا لَّهُ دِينِي}     الزمر:14}

 

[Sema: Mwenyezi Mungu tu namuabudu kwa kumsafishia Yeye tu Dini yangu.]     [Azzumar:14]

 

7. Kuwa na Mahaba.
Sharti ya saba ni kuwa na Mapenzi juu ya hii kalima na kila kinachofungamana nacho na kuchukia kila kinacho kwenda kinyume na kalima hii na kuwachukia wanaopinga kalima hii

Asema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

[وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَتَّخِذُ مِنْ دُونِ اللَّهِ أَنْدَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّهِ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِلَّهِ}   [البقرة: من الآية 165}

 

[Na katika watu wapo wanao chukua waungu wasio kuwa Mwenyezi Mungu.
Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walio amini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana. ]     [Al Baqara:165]

Na kwa neno lake Mtume ﷺ:

 

 ثلاث من كن فيه وجد بهن حلاوة الإيمان: أن يكون الله ورسوله أحب إليه مما سواهما، وأن يحب المرء لا يحبه إلا الله، وأن يكره أن يعود في الكفر بعد إذ أنقذه الله منه كما يكره أن يقذف في النار      رواه البخاري

[Matatu yatakaekuwa kwake, atapata utamu wa imani: Awe Mwenyzi Mungu na Mtume wake ni wapenzi bora zaidi kwake kuliko yeyote asiyekuwa wao,na ampende mtu,hampendi illa kwa (ajili ya)Mwenyezi,na achukie kurudi kuwa kafiri baada ya Mwenyezi Mungu kumuongoa kutoka huko, kama vile anachukia kwamba atupwe motoni]    [Imepokelewa na Bukhari].

 


SIKILIZA SHEREHE YA MADA HII NA SHEIKH SALIM KHATIB




comments