SOMO LA FIQHI YA KUAMILIANA
Biashara ili iwe sawa yanasharutishwa mambo yafuatayo:
Mwanzo: Maridhiano kati ya Muuzaji na Mnunuzi: MwenyeziMungu anasema
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً عَن تَرَاضٍ مِّنكُمْ} سورة انساء:29}
[Enyi Mulioamini Msiliane mali zenu kwa batili, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana baina yenu] [Suratul Nisaa:29].
Imepokewa na Sai’d al-khudhri MwenyeziMungu awaele radhi kwa Mtume (S.A.W) amesema [Uhakika wa biashara ni kuridhiana]. Basi kutokana na hayo hairuhusiwi kufanya biashara kwa kumlazimu mtu kwa njia isiyo ya haki. Kuna kulazimishwa kwa haki nao ni kumlazimu hakimu mwenye deni kuuza mali yake ili alipe deni.
Pili: Awe anaruhusiwa kufanya biashara: awe amebaleghe, mwenye akili, awe huru (asiwe mtumwa) na awe mwongofu.
Tatu: Awe ni mwenye kumiliki bidhaa: au awe ni msimamizi mfano: wakili, aliyepewa wasia, au ni walii, kwa ajili hiyo haruhusiwi mtu kuuza bidhaa ambayo si miliki yake, kutokana na neno lake mtume (S.A.W) akimuambia Hakim bin Hazim MwenyeziMungu amuele radhi [usiuze bidhaa isiyo yako]. Imepokewa na Ahmad (3/402) Nasai (7/289) Tirmidhi hadithi nambari (1232) Ibn Majah hadithi nambari (2187) na amesahihisha Al-Bani, tazama kitabu cha Irwau Ghalil (5/132)
Nne: Iwe bidhaa inaruhusiwa kutumiwa: kama vile vyakula, vinywaji, mavazi, vipando na mashamba, kwa ajili hiyo haipaswi kufanya biashara ambayo huruhusiwi kutumiwa mfano: pombe, nguruwe, vyombo vya mziki; kutokana na hadithi ya Jabir Mwenyezi Mungu amuele radhi mtume (S.A.W) amesema “Hakika ya Mwenyezi Mungu ameharamisha kufanya biashara ya kuuza pombe,nguruwe na masanamu .” Imepokewa na Bukhari (2236), Muslim (1581).
Imepokewa na ibn Abass Mwenyezi Mungu awaele radhi kwa mtume amesema [Mtume wa Mwenyezi Mungu ameharamisha thamani ya mbwa] [Imepokewa na Ahmad (1/247) Abu daud (3477)] imesahihishwa al-Arnut katika hashiya al-musnad (4/95).
Tano: Iwe bidhaa inayowezekana kupokewa; kwani bidhaa inayoshindikana kupokelewa ni kama haipo, kwa ajili hiyo hairuhusiwi kuuzwa; kwani hayo yanapelekea kupatikanwe na udanganyifu, kutokana na hayo hairuhusiwi kuuza samaki akiwa katika bahari, wala ndege akiwa hewani, na maziwa yakiwa kwenye titi, na kuuza mtoto wa mnyama akiwa kwenye tumbo la mama, au mnyama aliyekimbia. Abuhureira MwenyeziMungu amuele radhi amesema [Mtume wa MwenyeziMungu amekataza kufanya biashara ambayo ina udanganyifu]. [Imepokewa na Muslim (1513).]
Sita: Iwe bidhaa inajulikana kwa kila Muuzaji na Mnunuaji: Nao ni kwa kuiona wakati wa kufanya biashara, au ziwe sifa za bidhaa zinajulikana, kwani ujinga ni katika udanganyifu, na udanganyifu umekatazwa, na hairuhusiwi mtu kununua kitu ambacho hajakiona, au amekiona na hakijui, au kufanya biashara kwa bidhaa ambayo haikuwepo wakati wa kufanyiana mauzo.
Saba: Iwe thamani ya bidhaa inajulikana: Nayo ni kwa kuweka wazi bei ya bidhaa, na kujua kima chake.
![]() | Today | 3259 |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.