SOMO LA FIQHI YA KUAMILIANA


somo lafiqhi


Suala la pili:  Nguzo za kuuza na kununuwa.

Nguzo za kuuza na kununuwa ni tatu

1) Muuzaji na Mnunuzi

2) Bidhaa

3) Kauli kutoka kwa Muuzaji (Ijaab) na Mnunuzi (Qabul) mfano aseme Muuzaji: Nimeuza. Naye Mnunuzi aseme nimenunua.

Mbali na hayo, kuna Kauli ya vitendo mfano wake; Mnunuzi apeane pesa kwa Muuzaji naye apeane bidhaa pasi na mazungumzo kati yao.


comments