SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi 


Yanayoharamishwa kwa mwenye janaba

1. KUSWALI:
Kwa neno lake Mwenyazi Mungu Aliyetukuka:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا}    النساء:43}

 

[Enyi mlioamini! Msikaribie Swala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo sema, wala hali mna janaba isipo kuwa mmo safarini mpaka muoge]   [Al-Nisaa 43]

2. KUTUFU NYUMBA TUKUFU (Alkaba):

Kwa neno lake Mtume :

 

 

 الطواف صلاة إلا أن الله تعالى أحل فيه الكلام؛ فمن تكلم فلا يتكلم إلا بخير]     رواه النسائي]

 

[Kutufu Alkaba ni kama kuswali isipokuwa Mwenyezi Mungu amehalalisha kuzungumza,basi atakae zungumza asizungumze ila kwa kheri]   [Imepokewa na Nasai.].

3. KUGUSA MSAHAFU:
Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

 

لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ}    الواقعة:79}

 

[Hawaigusi isipokuwa waliotwahirishwa]    [56: 9].

Na neno la Mtume :

 

لا يمس القرآن إلا طاهر]    رواه مالك في الموطأ]

 

[Haugusi Msahafu isipokuwa aliye Twahara]    [Imeipokewa na Malik katika Muwatta’.]

4. KUSOMA QUR'ANI TUKUFU:
Imepokelewa kutoka kwa Sayyidna Ali Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:

 

كان النبي صلى الله عليه وسلم يقرئنا القرآن ما لم يكن جبنا]    رواه أحمد في المسند]

 

[Alikuwa Mtume ﷺ Akitusomea Qur'ani isipokuwa akiwa na janaba]   [ Imepokewa na Ahmad katika Musnad].

5. KUKAA MSIKITINI ISIPOKUWA KWA MPITA NJIA:

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

 

43:يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا}    سورة النساء}

 

[Enyi mlioamini! Msikaribie Swala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo sema, wala hali mna janaba isipo kuwa mmo safarini mpaka muoge].  [ Al-Nisaa 43]


comments