Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Maelezo kuhusu Vyombo Wanachuoni wanaeleze hukmu ya kutumia vyombo katika mlango wa Twahara kwa sababu maji ya kutumia katika twahara huwa ya hifadhiwa kwenye chombo. kwa hivyo ni vema kujua hukmu ya vyombo ndio wakaweka maudhui haya katika mlango wa Twahara.

KUTUMIA VYOMBO VYA DHAHABU NA FEDHA. 

1.Kutumia vyombo vya dhahabu na fedha katika kula na kunywa
Ni haramu kuvitumia kwa kauli yake Mtume ﷺ:

 

 لا تشربوا في آنية الذهب والفضة ولا تأكلوا في صحافها فإنها لهم في الدنيا ولكم في الآخرة ]    متفق عليه]

 

[Msinywe kwenye vyombo vya dhahabu na fedha, na msile kwenye sahani zake. Kwani hivyo ni vyao wao ulimwenguni na ni vyetu kesho Akhera]   [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Na kwa kauli yake Mtume ﷺ:

 

 الذي يأكل ويشرب في آنية الذهب والفضة إنما يجرجر في بطنه نار جهنم ]    متفق عليه]

 

[Yule anayekunywa kwenye chombo cha fedha, kwa hakika anaingiza tumboni mwake moto wa Jahanamu]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2. Kutumia vyombo vya dhahabu na fedha kwa matumizi yasiyokuwa ya kula na kunywa.
Inafaa kuvitumia kwa matumizi mengine yasiyokuwa kula na kunywa, kama kutawadhia na mengineo kwa hadithi ilio tangulia kuwa imekaza kuvitumia kwa ajili ya kula na kunywa, na imethubu kwa hadithi ya Ummu Salamah radhi za Allah ziwe juu yake  alikuwa na chombo (juljul) la fedha ambayo ndani yake kulikuwa na baadhi ya nywele za Mtume .


KUTUMIA VYOMBO VILIVYOLIHIMIWA KWA FEDHA 

Inafaa kutumia vyombo vilivyolihimiwa kwa fedha kidogo kuwapo na haja,Imethubutu

 

 أنَّ قدَحَ النبيِّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم انكسَرَ، فاتَّخذ مكان الشَّعْبِ سِلسلةً من فِضَّةٍ ]    رواه البخاري]

 

[Kwamba kopo la Mtume lilivunjika akapafunga pale palipopasuka kwa silsila ya fedha. [Imepokewa na Bukhari].

MAS'ALA

Uvaaji dhahabu kwa wanaume
Haifai kwa mwanamume kuvaa dhahabu, kwa hadithi iliyothubutu kutoka kwa Abu Musa al-Ash'ari Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema:

 

 حرم لباس الحرير والذهب على ذكور أمتي وأحل لإناثهم ]      رواه الترمذي]

 

[Limeharimishwa vazi la hariri na dhahabu kwa wanaume wa umma wangu na limehalalishwa kwa wanawake wao]     [Imepokewa na Tirmidhi].


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575051
TodayToday3118
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 10

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682923fb131cb18966383611747526651
title_682923fb1332c891753561747526651
title_682923fb1347618078294381747526651

NISHATI ZA OFISI

title_682923fb156ff11800875451747526651
title_682923fb1584d704645831747526651
title_682923fb159927282378861747526651 Add content here

HUDUMA MPYA

: 5 + 2 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com