Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Suala: Ni nini Maana ya Udhu katika Luga na katika sheria?
Jawabu: Udhu katika lugha ni Uzuri na usafi
Na Maana ya Udhu katika Sheria:

Ni kutumia maji kwenye viungo maalumu kwa nia ya kujitwahirisha.

Ni ipi Hukumu ya kutawadha?
Jawabu: Kutawadha: ima ni lazima na ima inapendekezwa:

A. Ni lazima kutawadha kwa mambo matatu
1. KUSWALI.

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu mtukufu aliposema:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ}  المائدة:6}

 

[Enyi Mlioamini! Mnapo simama kwa ajili ya swala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni]   [Al Maaida: 6]

Na kwa hidithi iliyopokelea na Abuu Hurayra radhi za Allah ziwe juu yake asema kuwa Mtume amesema:

 

لا يقبل الله صلاة أحدكم إذا أحدث حتى يتوضأ]    متفق عليه]

 

[Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapokuwa na hadathi (atakapotengukiwa na udhu) mpaka atawadhe (tena) ]     [Imepokewa na Bukhariy na Muslim.]

 

2. KUTUFU ALKA:

Kwa kauli yake Mtume kumwambia mwanamke aliye katika hedhi siku za haji:

 

افعلي ما يفعل الحاج غير أن لا تطوفي بالبيت حتى تطهري]    رواه البخاري]

 

[Fanya yote anayo fanya mwenye kuhiji isipokuwa usitufu mpaka utwahirike]

[Imepokewa na Bukhari.]

 

3. KUSHIKA MSAHAFU:

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu mtukufu:

 

لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ}   الواقعة:79}

 

[Hawaigusi isipokuwa wale waliotwahiriwa]    [Al Waaqia: 79]


B. Kutawadha kunapendekeza katika mambo mengine yasiyokuwa hayo
Kwa neno lake Mtume aliposema:

 

ولا يحافظ على الوضوء إلا مؤمن]    رواه أحمد وإبن ماجة]

 

[Na hajilazimishi na udhu isipokuwa mwenye Imani]   [ Imepokewa na Ahmad na Ibnu Maajah].

Na kunapendekezwa zaidi kutawadha wakati wa kujadidisha udhu kwa kila Swala, kutawadha kwa kumtaja Mwenyezi Mungu na kuomba, wakati wa kusoma Qur’ani, kabla ya kulala, kabla ya kuoga, na kutokana na kumbeba maiti na baada ya kila tukio la kutangua udhu, hata kama hataki kuswali.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575051
TodayToday3118
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 15

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682923fb131cb18966383611747526651
title_682923fb1332c891753561747526651
title_682923fb1347618078294381747526651

NISHATI ZA OFISI

title_682923fb156ff11800875451747526651
title_682923fb1584d704645831747526651
title_682923fb159927282378861747526651 Add content here

HUDUMA MPYA

: 7 + 9 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com