Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Tukiyaangalia maji kwa kuuzingatia wingi na uchache wake tutayakuta yamegawanyika sehemu/mafungu mawili:-

1. Maji mengi, na
2. Maji machache

MAJI MENGI: Haya kwa mtazamo wa sheria ni yale yaliyofikia Qullatein na zaidi yake.

Qullatein ni miongoni mwa vipimo vilivyokuwa vikitumiwa na Waarabu zamani. Kwa vipimo tuvitumiavyo leo Qullatein ni sawa na lita 216 za ujazo.

Kwa vipimo vya ukubwa Kullatein ni sawa na dhiraa moja na robo upana, urefu na kina. Dhiraa moja ni sawa sawa na sentimeta 48 (48 cm)

 

HUKUMU YA MAJI MENGI

Maji yaliyofikia Qullatein na kuendelea hayanajisiki kwa kuingia tu najisi ndani yake bali ya kuwa yamenajisika ikiwa najisi hiyo itaharibu mojawapo ya zile sifa tatu za maji.Kwa hadithi ya bwana Mtume ﷺ:

 

   إذَا كَانَ الْمَاءُ قُلَّتَيْنِ لَمْ ، يَحْمِلْ الْخَبَثَ]    رواه أحمد إبن ماجة وغيرهما]

 

[Maji ya kifikia Qullatein haya bebi Uchafu]     [Imepokewa na Ibnu Majah na Ahmad]

Kwa Mafhumu ya hadithi hii inamanisha Maji ya kiwa ni chini ya Qullatein yanabeba Uchafu.

MAJI MACHACHE

Maji yatahukumiwa kuwa ni machache ikiwa hayakufikia kiwango cha kullatein yaani yako chini ya lita 216 za ujazo ambazo ni karibu ya madebe 12 yaliyojaa.

HUKUMU YA MAJI MACHACHE

Maji haya yatanajisika kwa kuingiwa na najisi hata kama najisi hiyo haikuharibu mojawapo ya sifa za maji, na yatahukumiwa kwa mujibu wa sheria kuwa ni maji najisi. 

KUMBUKA

Msimamo huu ni kulengana na Madh'habu ya Imamu Shafi na Imam Ahmad Mungu awerehemu,ama Imam Malik na wengineo wamesema hakuna tafauti ya Maji mengi na mai kidogo,na wakasema Maji hayanajisiki mpaka ya badilike moja katika sifa zake Rangi yake au harufu yake au ladha yake,sawa ya kiwa ni Maji mengi au maji kidogo.Na huu ndio msimamo wa Sheikhul-Islam Ibnu Taymiyah Mungu amrehemu.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575017
TodayToday3084
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 21

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682920522ecbf3412448801747525714
title_682920522ee042480342491747525714
title_682920522ef4012374600931747525714

NISHATI ZA OFISI

title_6829205230f7e10037581331747525714
title_68292052310a911315027741747525714
title_68292052311cf3535101861747525714 Add content here

HUDUMA MPYA

: 1 + 8 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com