Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


1. Jua linapo chomoza siku hii ya tisa mahujaji wataelekea Arafa na huku wakileta talbiya

لبيك اللهم لبيك

[labbayka allamuhmma labbayka]

Na ni sunna kukaa (Namirah) mpaka jua lipinduke na kuingia wakati wa Adhuhuri, na wakati unapo ingia ni sunna kwa kiongozi wa kiislamu au naibu wake awahutubie mahujaji hutuba yenye kunasibiana na hali yao, awakumbushe kumpwekesha Mwenyezi Mungu na awafunze hukumu za hijja na mambo muhimu kuhusu dini yao.

2. Kisha atawaswalisha Adhuhuri na Alasiri kwa kuzikusanya, kutanguliza na kuzipunguza.

3. na sunna kwa Haji siku hii aelekee kibla, na azidishe kumuomba Mungu na ajitahidi sana katika kuomba, na adhihirishe unyonge wake na udhaifu wake na kumuhitajia kwake Mwnezi Mungu na akariri maombi.

Amesema Mtume :

 

خير الدعاء دعاء يوم عرفة ، وخير ما قلت أنا والنبيّون من قبلي : لا إله إلا الله وحده لا شريك له ، له الملك ، وله الحمد ، وهو على كل شيء قدير      رواه الترمذي

 

[Dua bora ni dua ya siku ya Arafa, na maneno bora niyale niliyo yasema mimi na manabii kabla yangu: hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi mungu pekeyake hana mshirika ufalme ni wake, na kusifiwa ni kwake yeye, na yeye ni muweza wakila kitu] [Imepokewa na Tirmidhi]

na afanye pupa kuomba dua zilizopokelewa kwa Mtume na ajiepushe na dua ya kujikalifisha, na asome Qur’ani kadiri anavo weza, na akithirishe kumswalia Mtume .

4. Baada ya jua kuzama muhujaji wataondoka kutoka arafa wakielekeya Muzdalifa na haifai kuondoka kabla ya kuzama kwa jua, na akiondoka kabla kuzama kwa jua itamlazimu arudi hata kama ni usiku na asiporudi itamlazimu yeye damu kuchinja nayo ni kuchinja mbuzi au fungu la saba la ngamia ama fungu lasaba la ngombe

na nisunna kwa mahujaji kuondoka kwa utulivu na upole bila ya kuwaudhi watu, na aondoke hali ya kuleta talbiya na kumtaja mwenyezi mungu  .


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6575072
TodayToday3139
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 6

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_682927821776c562094561747527554
title_68292782178568607291911747527554
title_682927821794721454191621747527554

NISHATI ZA OFISI

title_6829278218f46561391971747527554
title_682927821903618003030801747527554
title_68292782191173186941631747527554 Add content here

HUDUMA MPYA

: 10 + 5 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com