SOMO LA FIQHI
Suali: Ni ipi hukumu ya Hijja na fadhla zake ?
Jawabu: Hijja ni mojawapo ya nguzo za Kiislamu. Mwenyezi Mungu Alioyetukuka Ameilazimisha kwa waja wake. Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu:
وَلِلَّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ} سورة آل عمران:97}
[Ni haki ya Mwenyezi Mungu kwa watu waihiji Alkaba, kwa anayeweza kwenda huko. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi Hawahitajii walimwengu] [Al Imraan: 97]
Na amesema Mtume ﷺ:
بني الإسلام على خمس شهادة أن لا إله إلا الله وأن محمدا رسول الله وإقام الصلاة وإيتاء الزكاة وحج البيت وصوم رمضان] متفق عليه]
[Uislamu umejengwa juu ya misingi mitano: Kukubali kuwa hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake, kusimamisha Swala, kutoa Zaka, kuikusudia Alkaba kwa Hija na kufunga mwezi wa Ramadhani] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Na amsema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ:
مَنْ حَجَّ فَلَمْ يَرْفُثْ وَلَمْ يَفْسُقْ غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبه] رواه الترمذي]
[Mwenye kuhiji asiseme maneno machafu [ Rafath: ni neno linalotumika kumaanisha maneno machafu.] na asitoke kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu [ Fusuuq: maasia.], atasamehewa dhambi zake zilizotangulia] [Imepokewa na Tirmidhi.].
Na Hijja ni lazima kwa umri mara moja.