SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Suala: Ni nini Maana ya Hijja kilugha na Sheria?

Jawabu: Maana ya Hijja kilugha ni Kukusudia na kuelekea.

Ama maana ya Hijja kisheria
Ni kukusudia kwenda Makka katika kipindi maalumu ili kutekeleza ibada ya Hijja.

 

Suala: Ni ipi Hukumu ya Hijja

Jawabu: Hija ni fardhi kwa kila Muislamu mwenye uwezo, ni nguzo ya tano miongoni mwa nguzo tano za Uislam. Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Alioyetukuka:

 

وَلِلَّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ}    آل عمران:97}

 

[Ni haki ya Mwenyezi Mungu kwa watu waihiji Alkaba, kwa anayeweza kwenda huko. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi Hawahitajii walimwengu]    [3: 67]

Na amesema Mtume ﷺ:

 

 

 بُنَي الإسلامُ على خَمْسٍ : شهادَةِ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمَّداً رسولُ اللهِ، وإقَامِ الصَّلاةِ، وإيتَاءِ الزَّكاةِ، وحَجِّ البَيْتِ، وصَوْمِ رَمَضَانَ


رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ

[Uislamu umejengwa juu ya misingi mitano: Kukubali kuwa hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake, kusimamisha Swala, kutoa Zaka, kuikusudia Alkaba kwa Hija na kufunga mwezi wa Ramadhani]   [Imepokewa na Bukhari.]

 

[مَنْ حَجَّ فَلَمْ يَرْفُثْ وَلَمْ يَفْسُقْ رَجَعَ كَمَا وَلَدَتْهُ أُمُّهُ ]

وفي رواية للترمذي  : [ غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبه ] . صححه الألباني في صحيح الترمذي

Na amsema Mtume wa Mwenyezi Mungu : [Mwenye kuhiji asiseme maneno machafu na asitoke kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu atarudi kama siku alio zaliwa na mamayake] Na katikwa riwaya ya Tirmidhiy [Atasamehewa dhambi zake zilizotangulia]  [Imepokewa na Tirmidhi na kusahihishwa na Al-Baniy]

[Rafath: ni neno linalotumika kumaanisha maneno machafu.] 

[Fusuuq: maasia.]

 

Suali: Je Ibaada ya hijja ni faradhi ya kila Mwaka?

Jawabu: Wameafikiana wanachuoni kuwa ibaada ya hijja ni faradhi ya umri mara moja.

kama ilivyo kuja kwenye Hadithi:

 

عن ابْنِ عَبَّاسٍ أَنَّ الأَقْرَعَ بْنَ حَابِسٍ سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ : يَا رَسُولَ اللَّهِ الْحَجُّ فِي كُلِّ سَنَةٍ أَوْ مَرَّةً وَاحِدَةً ؟ قَالَ : بَلْ مَرَّةً وَاحِدَةً ، فَمَنْ زَادَ

فَهُوَ تَطَوُّعٌ )     رواه أَبُو دَاوُد  وصححه الألباني

 

Kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba Aqra'i bin Habis alimuliza Mtume rehma na amani zifikie yeye akasema: Ewe Mtume wa Mwenyzi Mungu Hijja ni kila Mwaka au ni mara moja? Akasema [Ni mara moja na mwenye kuzidisha hiyo ni Sunna]  [Imepokewa na Abuu Daud na kusahihishwa na Al-Baniy]


comments