MAELEZO KUHUSU SOMO LA FIQHI
Fiqhi ya ibaada
Fiqihi katika lugha : Ni Ufahamu au ilimu,
Katika istilahi : Nikujuwa hukumu za kisheria kutokamana na ufafanuzi wa Dalili. Kuambatana na Manhaj ya somo la Usuul-Alfiq na fiqihi ya ibada ndicho kigawanyo cha kwanza katika ilimu ya vitagaa vya fiqihi.
Kisha inafuatia fiqhul-Muamalaat (fiqihi ya kuamiliana): Inaregelea maudhui ya fiqihi ya ibaada katika vigawanyo vitano vya msingi nazo: Twahara,Swala,Zakaa,Saumu na Hajji
Maana ya Fiqihi
Fiqihi katika Lugha
Ni kukijua kitu na kukifahamu, sawa kitu ambacho kilikuwa kimefichika au kiko wazi,na miongoni mwa hayo ni dua ya Mtume kumuombea Ibn Abbas "Ewe mola mfahamishe dini na umfunze tafsiri"
Kisha likatumika neno la fiqihi hasa katika ilimu za Sheria kwa sababu ya cheo chake, utukufu wake, fadhla zake kuliko ilimu zote nyingine.
Fiqihi katika istilah
Ni kujua hukumu za kisheria katika ibada ya vitendo kutokamana na ufafanuzi wa dalili swahihi kuamabatana na misingi iliosalimika ya fiqihi.
Kuanzia kwa ilimu ya Fiqhi
Ilianzia fiqhi ya kiislamu kwanzia uislamu ulipo anza na kutumilizwa kwa bwana Mtume Muhammad ﷺ na zimepita awamu nyingi tofauti,na awamu muhimu zaidi ni kipindi alipo tumilizwa Mtume ﷺ Mpaka kufa kwake. Na kipindi hiki wahyi (Ufunuo) ndio chanzo cha Fiqh ya kiislamu katika awamu hii na yale yalio kuja kutoka kwa Qur'ani tukufu au katika mambo alio jitahidi bwana Matume ﷺ kutokamana na hukumu ambazo wahyi ndio msingi wake. Ama kwa yale alioyafanya na kusawazishwa na wahyi pia vile vile ijtihadi ya mwashaba wakati wa uhai wake maregeleo yake ni Mtume ﷺ. Kwa jinsi ya kulikubali au kwa kulikata. Katika awamu hii wahyi ndio ilikuwa chanzo cha sharia na baada ya kufa Mtume kulifuatiwa na awamu tofauti.
Fadhla ya kujifunza ilimu ya fiqhi
Mtu kujifunza dini ya huwa yahisabiwa ni katika amali bora na ni Alama ya kheri.
Amesema Mtume rehema na amani zimfikie yeye [Mwenyezi Mungu anapomtakia mja wake kheri humfahamisha dini]
Na Mwenyezi Mungu anasema [Wala haiwafalii Waumini kutoka wote. Lakini kwa nini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini na kisha waje kuwaonya wenzao watakapo warejea, ili wapate kujihadharisha? ] Al-Ttawba :122
kwa sababu mtu anapo jifunza katika dini atapata ilimu yenye manufaa yenye kusimamia matendo mema na niwajibu kwa kila muisalmu ili matendo yake yawe ni sahihi ajifunze yale ambao yatakayo sahihisha swala yake na funga zake na hija yake na kujifunza hukumu ya zaka,na hukumu za kuamiliana, na mangineo.
Matawi ya Fiqhi
Somo la fiqhi kulingana na maudhui yanao funzwa linato vitagaa vingi sana, muhimu katika hivyo ni :
Fiqhi ya ibaada
Na milango muhimu katika ibaada ni Mlango wa Twahara, Swala,Zakaa, Hijja na Umra, Kufunga na kuna milango mengine inayo tokamana na milango mitano hii.
Fiqhi ya Kuamiliana
Kwa mafunzo zaidi tazama fiqh ya kuamilana
Fiqhi hii inahusu katika milango ya kuamiliana; Mfano Kuajiri,Rahani, Ribaa,Waqfu,Kuuaza na kununuwa na kushirikiana.
Na kuna milango mengine Mfano : Wa jinai na hukumu za familia,Twalaka na Kurithiana, vyakula na vinywaji, kuhukumiana na kutoa Ushahidi.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.