ATAFANYA NINI MTU ALIENUNUWA KITU KISHA AKAJUWA KUWA ALICHOKINUNUWA NI CHAKUIBWA?
Suali: Ni ipi hukmu ya mtu alienunuwa kitu kwa mtu kisha akajua kuwa ni kitu cha kuibiwa?
Jawabu: Ni haramu kwa mtu kununuwa kitu cha kuibiwa kwa sababu kufanya hivyo ni katika kusaidia kuzidisha wezi na kuwapa nguvu na kuendelea na kuiba kwa sababu ikiwa hatopata mtu wa kununuwa huenda akakomeka na kuiba lakini akijuwa kuwa wako wanunuzi basi ataendelea kuiba,na dini yetu imekataza kusaidia katika dhambi na uadui asema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
وَلا تَعَاوَنُوا عَلَى الْأِثْمِ وَالْعُدْوَانِ } المائدة:2}
[Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui.] [Al Maaida:2]
Na mtu anapo nunuwa kitu kisha akajuwa kuwa alichonunuwa ni chakuibwa ikiwa anamjua alie ibiwa basi atamregeshea Mwenywe kisha akafuatilie pesa zake kwa yule aliemuuzia, kwa neno lake Mtume ﷺ:
إذا سُرق من الرجل متاعٌ، أو ضاع له متاع، فوجده بيد رجل بعينه، فهو أحق به، ويرجع المشتري على البائع بالثمن. رواهأحمد، وحسنه الشيخ شعيب الأرناؤوط.
[Mtu anapo ibiwa kitu chake au akapoteza kisha akakipata kwa mtu mwengine kitu kile basi ni haki yake (achukuwe) na alie uza amrudishie alie nunuwa thamani yake] [Imepokewa na Ahamad na kuhasinishwa na sheikh Shuayb Al Arnaut.]
Na ikiwa hamjui mwenyewe basi ajitahidi kumtafuta,na akishindwa kumpata kile kitu au mali aitoe sadaka na wala asitumie kwa sababu si haki yake.