HUKMU YA MWANAMUME KUVAA CHENI

Suali: ni ipi hukmu ya Mwanamume kuvaa cheni ya Fedha? 

Jawabu: Mwanamume kuvaa cheni au vipuli kwa ajili ya mapambo haifai na ni haramu kuvaa mapambo kama hayo, sawa iwe ni za fedha au madini mengine yoyote kwa sababu ni kujifananisha na wanawake na Mtume amemlaani mwanamume mwenye kujifananisha na wanawake na mwanamke mwenye kujifananisha na mwanamume kama ilivyo kuja kwenye hadithi iliyopokelewa na Imamu Al Bukahri:

 

[لَعَنَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمُتَشَبِّهِينَ مِنْ الرِّجَالِ بِالنِّسَاءِ وَالْمُتَشَبِّهَاتِ مِنْ النِّسَاءِ بِالرِّجَالِ]

 

[Amemlaani Mtume wa Mwenyezi Mungu wanaume wanao jifananisha na wanawake,na wanawake wanao jifananisha na wanaume]

Na imekuja Hadithi iliyopokelewa na Abuu Hurayra radhi za Allah ziwe juu yake asema:

 

لَعَنَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الرَّجُلَ يَلْبَسُ لِبْسَةَ الْمَرْأَةِ وَالْمَرْأَةَ تَلْبَسُ لِبْسَةَ الرَّجُلِ]    رواه أبوداود]

 

[Amemlaani Mtume wa Mwenyezi Mungu Mwaname anaevaa vazi la wanawake na Wanawake wanao vaa mavazi ya wanamume].    [Imepokewa na Abuu Daud].

Na wanazuoni wameweka qaaida maluum kuhusu mavazi na mapambo wakasema chochote kinacho julikana kuwa ni katika matumizi ya wanawake peke yao basi ni haramu kwa mwanamume kutumia kama kuvaa mkufu bangili, vipuli na kadhalika.

Na mwanamume anaruhusiwa kuvaa pete ya fedha kama ilivyo pokelewa katika sahih Al Bukharin a Muslim kuwa mtume alikuwa na pete ya Fedha.
Na Allah ndie mjuzi zaidi


comments