HUKMU YA MUISLAMU KUSHEREHEKEA KRISMASI

 

Suala: Ni ipi hukmu ya Muislamu kusherehekea siku ya krismasi?

Jawabu: Haifai kwa Muislamu na niharamu kusherehekea siku ya kisrmasi kwa sababu siku hii inafungamana na itikadi potofu ya wakristo ya kudai kuzaliwa kwa Nabii Issa (Alayhi salaam),na itikadi hii ni itikadi potovu na ni katika madhambi makubwa sana, kudai kuwa Mwenyezi Mungu ana mtoto, Mweyezi Mungu anasema:

 

وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَٰنُ وَلَدًا  لَّقَدْ جِئْتُمْ شَيْئًا إِدًّا  تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا أَن دَعَوْا لِلرَّحْمَٰنِ وَلَدًا  وَمَا يَنبَغِي لِلرَّحْمَٰنِ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا إِن كُلُّ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِلَّا آتِي الرَّحْمَٰنِ عَبْدًا     مريم:88-93

 

[Na wao ati husema kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana!Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno!Zinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande.Kwa kudai kwao kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana.Wala hahitajii Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa na mwana.Hapana yeyote aliomo mbinguni na ardhini ila atafika kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni mtumwa wake.]     [Maryam:88-93]


Kisha dini yetu imekuja kutukataza na kututahadharisha kuwaiga wasio kuwa waislamu hasa katika mambo amabayo yanafungamana na dini zao. Na Muislamu anapo sherehekea siku hii huwa amejifananisha na wao, na kudhihirisha mapenzi juu yao, Mwenyezi Mungu anasema:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ   المائدة:51 

 

[Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.]    [Al Maaida:51]

Na Mtume alipofika Madina alikuta watu wa madina wakisherehekea siku mbili katika masiku za kijaahilia mtume akawakataza na kuwaambia kuwa:

 

إن الله قد أبدلكم بهما خيرا منهما يوم الأضحى ويوم الفطر]    رواه أبوداود]

 

[Hakika Mwenyezi mungu amewabadilishia na siku bora kuliko hizo nayo ni siku ya eid-ul-fitr na eid-ul-adh'haa.]     [Imepokewa na Abuu Daud].

Na Mtume asema:

من تشبه بقوم فهو منهم]    رواه أحمد]

 

[Mwenye kujifananisha na watu na yeye ni katika wao]    [Imepokewa na Ahmad]

Kwa hivyo Muislamu hafai na ni haramu kusherehekea siku ya krismasi na kushirikiana na wao katika jambo hili sawa katika kupeana au kuchukuwa zawadi, au kwenda kwenye sherehe zao, au kuwavisha watoto nguo mpya. 
Na Muislamu yatakikana asione haya katika Mas'ala yanayo ambatana na Itikadi yake, na lau jirani yako mkiristo atakuletea zawadi ya munasaba kama huu ni uwe wazi na umfahamishe kwa njia mzuri ya kuwa dini yetu imetukataza kukubali kushiriki katika ibada za dini nyingine.

Na la wajibu kwa Muislamu ni kuwa mbali na kujiepusha na kusherehekea masiku kama haya na kuwafunza watoto wake na jamaa zake uharamu wa jambo hili ambalo leo Waislamu wengi wamelichukulia kuwa ni jambo dogo sana na ilhali ni jambo kubwa.

Na Allah ndie Mjuzi zaidi.


comments