HUKMU YA MTU KUSHEREHEKEA SIKU ALIYOZALIWA (BIRTHDAY)

 

Suali: Ni ipi hukumu ya mtu kusherehekea siku yake aliozaliwa,na je mtu akikualika kuhudhuria sherehe hiyo yafaa kwenda?

Jawabu: Muislamu hafai kusherehekea siku aliyozaliwa kwa sababu sherehe hizi ni za uzushi na dini yetu imekuja kututahadharisha na mambo yote yauzushi yanayo fanywa,na vile vile haifai kuitikia mwito wa jambo hilo kwa sababu kufanya hivyo ni katika kulitilia nguvu jambo la Munkar ,na Mwenyezi Mungu anasema:

 

أم لهم شركاء شرعوا لهم من الدين ما لم يأذن به الله}    الشورى:21}

 

[Au hao wana miungu ya kishirikina walio watungia dini asiyo itolea idhini Mwenyezi Mungu?]    [Al-Shuraa:21]

Na Amesema tena katika aya nyingine:

ثم جعلناك على شريعة من الأمر فاتبعها ولا تتبع أهواء الذين لا يعلمون . إنهم لن يغنوا عنك من الله شيئاً وإن الظالمين بعضهم أولياء بعض والله ولي المتقين          الجاثية:18-19

 

[Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasio jua kitu.Kwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hakika wenye kudhulumu ni marafiki wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni rafiki wa wamchao.]   [Al Jaathiya:18-19]

Na imesihi kutoka kwa bwana Mtume ﷺ:

 

من عمل عملاً ليس عليه أمرنا فهو رد]     رواه مسلم]

 

[Yoyote mwenye kufanya kitendo ambacho hakuna maamrisho yetu basi ataregeshewa mwenyewe.]    [Imepokewa na Muslim.]
Na amesema Mtume  katika hadithi nyengine:

 

خير الحديث كتاب الله وخير الهدي هدي محمد صلى الله عليه وسلم ، و شر الأمور محدثاتها وكل بدعة ضلالة]    رواه مسلم]

 

[Mazungumzo yalio bora ni kitabu cha Mwenyezi Mungu na Muongozo ulio bora ni Muongozo wa Bwana Mtume Muhammad na Mambo maovu ni Uzushi na kila uzushi ni upotevu].   [Imepokewa na Muslim]
Kisha pamoja yakuwa ni Uzushi katika dini na kuwa halina msingi na vile vile ni katika kuwaiga Mayahudi na wakristo katika mila zao,na Sheria imetahadharisha waislamu kuwaiga wasio kuwa waislamu katika mila zao na ada zao, asema Mtume akitahadhirisha kuwaiga walio Mayahudi na Manaswara:

لتتبعن سنة من كان قبلكم حذو القذة بالقذة حتى لو دخلوا جحر ضب لدخلتموه : قالوا  يا رسول الله : اليهود و النصارى ؟  .. قال : فمن     رواه البخاري ومسلم

 

[Mutafuata mienendo ya watu walio kuwa kabla yenu unyoa kwa unyoa hata wakiingia katika shimo la burukenge na nyinyi mutaingia, wakasema Ewe Mtume wa Mwanyezi Mungu Mayahudi na Manaswara? Akasema basi ni nani?]  (ikiwa si hao)    [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na katika hadithi nyingine asema Mtume ﷺ:

 

من تشبه بقوم فهو منهم]   رواه أبوداود]

 

[Mweye kujifananisha na watu na yeye ni katika wao].    [Imepokewa na Abuu Daudi].
Kwa hivyo Mislamu anatakikana awe mbali na mila kama hizi na ajaribu kutoa nasaha kwa jamaa zake walio athirika na mila kama hizi ili wajiepushe nazo
Na Allah ndie Mjuzi zaidi


comments