HUKMU YA KUVUTA SHISHA
SUALI: Ni ipi hukmu ya kuvuta shisha?
JAWABU: Kuvuta shisha ni haramu kama vile kuvuta sigara, kwa kupatikana madhara mengi,kwanza kujidhuru katika nafsi yake,na kwa kupoteza mali yake,na kwa kuwadhuru wenzake. Sharia yetu imekuja kuharamisha kila baya na lenye na madhara.
Mwenyezi Mungu anasema kuhusu hikma ya kumtumiliza Mtume:
وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ} الأعراف:157}
"Na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu." [Al-A'araaf:157]
Na imethubutu kiilimu kuwa uvutaji wa shisha na sigara,kunasababisha maradhi mabaya yenye kuamgamiza, na Mwenyezi mungu amesema:
وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا} النساء:29}
"Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni. [Al-Nnisaa:29
Na yoyote mwenye kutumia uraibu huo huhesabiwa amejidhulumu nafsi yake,na kuwadhuru wanao kaa karibu na yeye. Kwa hivyo uvutaji wa sigara na shisha ni katika madhambi makubwa ni lazima kwa anae tumia uraibu huu uraibu afanye bidii kuwacha na kutubia kwa Mwenzi Mungu, na kumuomba Allah amsaidie kuweza kuwacha.
Na bila shaka uvutaji wa sigara ni katika mitihani mikubwa ilio wakumba waislamu. Kiasi ya kuwa asilimia kubwa katika waislamu hutumia sigara na kuonekana ni jambo la kawaida.
Na allah ndie mjuzi zaidi.