HUKMU YA KUSHEREHEKEA CHRISTMAS
Suali: Ndugu yetu anasema :anaona yakwamba baadhi ya Waislamu wanashirikiana na Wakristo katika sherehe za Christmas au sherehe za kuzaliwa Yesu kama wanavyoita na anaomba maelekezo.
Jawabu: Haifai kwa Muislamu wa kiume au wa kike kushirikiana na Manaswara au Mayahudi au wengine katika Makafiri katika sherehe zao, bali ni wajibu kuwacha hilo kwani,
[من تشبه بقوم فهو منهم]
[Atakaejifananisha na watu basi yeye ni katika wao]. Na Mtume Muhammad ﷺ ametutahadharisha kujifananisha na wasiokua Waislamu na kuiga tabia zao. Basi inampasa Muumini wa kike na wa kiume kujihadhari na jambo hilo na asisaidie kufanyika kwa sherehe hizi kwa jambo lolote, kwa sababu sherehe hizi ni sherehe ambazo ziko kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu, na wanaozisherehekea ni Maadui wa Mwenyezi Mung hivyo basi haifai kushiriki katika sherehe hizo wala kuwasaidia wenye kusherehekea kwa jambo lolote, sio kwa Chai wala Kahawa wala kwa jambo lolote kama vile vyombo na mfano wake.
Na pia Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ} المائدة:2}
[Na saidianeni katika wema na Ucha Mungu wala musisaidiane katika Maovu na Uadui] [Al Maidah: 2.]
Hivyo basi kushirikiana na Makafiri katika sherehe zao ni sampuli ya kusaidiana katika Maovu na Uadui, ni wajibu kwa kila Muislamu kuwacha hilo la kusherehekea sherehe zisizokua za Kiislamu, na haifai kwa mwenye akili kughurika na watu katika matendo yao, la wajibu ni yeye kuangalia Sheria ya Kiislamu na iliyokuja katika Sheria, na afwate maamrisho ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake ﷺ na asiangalie mambo ya watu kwani watu wengi hawajali Sheria za Mwenyezi Mungu kama alivyosema Mwenyezi Mungu katika kitabu chake kitukufu:
إِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّه} الإنعام:116}
[Na ukiwat'ii wengi katika hawa waliomo Duniani watakupoteza na Njia ya Mwenyezi Mungu]. [Al An'aam: 116.] Na anasema Mwenyezi Mungu alietukuka:
وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ} يوسف:103}
[Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi] [ Yusuf: 103]
Mambo ya kukhalifu Sheria haifai kuyachukua hata kama Watu wanayafanya.
Na Muumini analinganisha Matedo yake na kauli zake na analinganisha matendo na kauli za watu na Qur'ani na Sunna zikiafikiana hiyo ndio yenye kukubaliwa hata kama wataiacha watu, na yakikhalifiana Maneno na matendo yake na Kitabu na Sunna basi hayatokubaliwa hata wakayafanya watu. Mwenyezi Mungu awaruzuku wote tawfiiq na uongofu.
*Chanzo: Fatawa ya Sheikh Ibnu Baaz
Imefasiriwa na Mahamd Fadhil El Shiraziy